Jamani hii Taasisi ya Police Tanzania siilewi kabisa. Naiita Taasisi maake mi siamini kama ni Jeshi kama wanavyojiita. Jana nilikuwa ndo naingia katika Gate la leaders club kumshuhudia mzee wa burrudani Kofii nilikutana na FFU kama 20 hivi wanamshambulia mtu na marungu bila hata huruma ya kibinadamu kama wanaua Nyoka. kww imani nyoka ni shetani sasa cjui yule bwana naye alikuwa shetani pale kwenye tulip.POLISI HAMNA MBINU MBADALA KWA KUKABILIANA NA WAKOSEFU KULIKO KUPIGA MTU MITHILI YA SHETANI. HAYO NDO MNAFUNDISHWA CPP MOSHI? SAIDI MWEMA kweli polisi imekushinda kunyoosha nidhamu ya utu kwa watanzania. kumbukeni mishahara yenu, mavazi yote ni kodi zetu wote.