Polisi Dar wakusanya milioni 440 za makosa ya barabarani kwa siku tano

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,786
Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es salaam kimekusanya Tsh. 440,000,000 za makosa ya Barabarani kuanzia May 16 hadi 21, 2017.

trafiki.jpg
 
Kwa utaratibu huu hata mtoto atatambua kua jeshi la polisi ni wanyanyasaji.
Atakae bisha namsubiri, sina kazi Leo.
 
Naona wanaokoa jahazi la ukata mahali hawa sio bure mihera yote hiyo siku tano !!!!!!!!
 
Lazima wapate nyingi Jana nimewakuta kwa sokota saa nne na nusu usiku, sijui nao wameambiwa wafanye 24 hrs
 
Wajumlishe na rambi rambi. PolisiTRA. Hawa jamaa wako vizuri. Ndiyo watakuwa wanakusanya mapato. TRA ivunjwe
 
juzi kati walinikamata nikiwa napeleka gari gereji ....uwii nilijuta maana sio kwa kushambuliwa kule!! kibaya zaidi gari alikua anendesha Fundi makanika mie nimejikalia siti ya nyuma nachat kumbe kijana hana leseni!!! Mtumee!! hamna rangi nliacha ona...sitakaa nisahau nilivyoacha 70,000 cash ili kukwepa kwenda mahakamani na pia kukwepa faini 5 za 30k each !!! alaaniwe trafic yule wa mbez mwisho...nlikua natokea Goba
 
utii wa sharia bila shuruti unahitajika, dawa yao ni kuacha kufanya makosa ambayo yanapeleka kutozwa hizo pesa! All in All inasikitisha kuona kitengo cha Police kikikaa Barabari kwa lengo la kukusanya kodi badala ya kurekebisha makosa!
 
Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es salaam kimekusanya Tsh. 440,000,000 za makosa ya Barabarani kuanzia May 16 hadi 21, 2017.


Mimi nafikiri sio jambo la kufurahia sana ingawa inaonekana wanafanya kazi kwa bidii lakin ni lazima tuwe Wa kweli kwamba hawa matrafik siku hizi wamekuwa waonevu sana barabaran lengo likiwa moja tu kwa namna yoyote ile lazima ulipe fain hata kama kosa halistahili kulipishwa fain: mfano uliowazi ni kwamba serikali yetu imeruhusu magari yatokayo nje kuwa ni used sasa unapoongelea gari mtumba kutoka Japan inamaana hilo gari tayar limeshatumika na hivyo linapoteza sifa ya kuwa limekamilika kila kitu, sasa wewe unataka Mimi gari langu liwe na kila kitu Mimi ukamilifu wa gari ntautoa wapi wakat nimelipokea likiwa katika hali ya upungufu? Hapa inabidi serikali iangalie hili suala vizuri maana kwa asilimia kubwa ni uonevu ingawa wapo madereva wazembe
 
Mimi hii wiki nimeshakamatwa mara mbili pale taa za salender bridge karibu na kituo chao cha polosi kwa kosa la kuwakiwa na taa ya njano kabla sijavuka. Nilijaribu kuwaelewesha kuwa taa zetu hazina timer kwa hiyo huwezi jua ni muda gani taa ya njano itawaka lakini hawajanielewa. Utetezi wao ni kuwa kama hukubali kosa wakupeleke mahakamani ukajitetee huko. Yaani ni either ungarishe viatu au elfu 30 iende.
 
Back
Top Bottom