Polisi Dar waijibu Sumatra | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Dar waijibu Sumatra

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Mar 25, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Polisi Dar waijibu Sumatra


  Geofrey Nyang’oro
  SIKU moja baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kulishtaki Jeshi la Polisi kwa Rais Jakaya Kikwete, kuwa ndiyo kiini cha uvunjaji wa kanuni, sheria na taratibu za usafiri za barabarani, jeshi hilo katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekana tuhumu hizo.

  Kukanushwa kwa tuhuma hizo, kulifanywa jana na na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani katika kanda hiyo, Vitus Nikata.Nikata aliliambia Mwananchi kuwa tuhuma hizo hazina ukweli na kwamba Jeshi la Polisi, limekuwa likijitahidi kufanya kazi za Sumatra.

  "Sio kweli kuwa polisi ndio wamiliki wa daladala,mimi ninachofahamu ni kwamba kuna baadhi ya maofisa wastaafu wanafanya biashara hiyo. Lakini si kweli kama hiyo ndiyo sababu za kuvunjwa kwa kanuni, taratibu na sheria za usafirishaji zinazoratibiwa na Sumatra,"alisema Nikata.

  Kamanda Nikata alikuwa akijibu tuhuma zilizotolea na Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Israel Sekrasa, kuwa mamlaka yake inashindwa kufanya kazi sababu watu waliopewa jukumu la kusimamia sheria, wana ubinafsi unaosababishwa na kuhusika kwao katika biashara ya daladala.

  Nikata alisisitiza kuwa tuhuma hizo si za kweli na kwamba vinginevyo Mkurugenzi huyo wa Sumatra atoe orodha ya polisi wanaomiliki daladala hizo.
   
 2. marshal

  marshal JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hata aibu hawana.Yaani Trafic wa Dar utafikiri wameajiliwa kukusanya pesa barabarani hata aibu hawana.Sometimes unatafutiwa kosa ambalo halipo ili mradi tu utoe kitu kidogo.Sema kwani kikwete hajui hata wakishtaki trafic hawaachi kamwe.Kwanza kuupata tu u trafic lazima watu walambe kidogo!!
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  sitaki kupingana na Nikata ila simuungi mkono.....WAWE WAKWELI......! WANAHUSIKA
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  POLISI WETU KWELI NI WAWEKEZAJI MAARUFU WA NDANI YA NCHI KWA BIASHARA
  ZA DALADALA VIKWECHE NA MI-LENDIROVA FISI ZENYE MAKOSA YA BARABARANI
  50 KIDOGO JIJINI DAR NA MIKOANI BILA KUKAMATWA KITU WALA NINI


  Jamani kwani SUMATRA wamekosea wapi hapo wakati ni kweli polisi Dar wanajulikana kuwa ni KUNDI LA WAWEKEZAJI WA NDANI YA NCHI katika sekta ya usafirishaji mjini KWA KUJAZA VIKWECHE kila kona ya jiji???

  Mweh, vitu vingine jamani watu tujisemeage tu ukweli kwamba JK wala Mzee Sekirasa hakukudanganya kitu wala kumkandia mtu chochote hapo. Tuulize sisi wananchi ndio kabisaa tutawataja hadi kwa majina yao. Tena kuna KA-SHOTI mmoja hivi anaitwa Mzee Kimti nakwambia yule baba ni noma kwa rushwa barabarani na utaalamu wake wa kuupokea bila hata mkono wa pili kugundua kinachoendelea ndio kabisaaa usipime!!!!

  Tena kabla zile biashara ya kuvuta magari yalioegeshwa vibaya maeneo mbali mbali ya jiji haijapigwa marufuku mbona maafande ndio walikua wawekezaji wakubwa kwenye mi-landrover kuu kuu (tena ukimuuliza rafiki yako Lowassa atakuambia kwamba kule kwao machalii wanaziita mbauda) maarufu kwa jina la FISI hapa Dar???

  Jamani polisi kubalini tu ukweli huu mambo yaishe; huwezi jua rais hakucheka kwa ubaya juu ya taarifa hizi pengine kwa kukubali mnaweza hata mkapigwa jeki ya kupata mikopo nafuu ya biashara ya Daladala Mayai yale yenye kiyoyozi na zulia ndani!!
   
 5. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,089
  Likes Received: 885
  Trophy Points: 280
  bora umekuwa muwazi mr sekirasa. na kama ikiwezekana waorodheshwe askari wote wanaomiloiki hivyo vidaladala. mmbona wapo wengi tu.
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Maslahi yao ni madogo sana, wanastahili "kula kwa jasho lao" lakini pia wanakashfa ya kipindi flani hivi kuwa askari wa dar (traffic) wana saccoss yao baada ya kupiga mabao na kama traffic akiwa haleti mgao unaoeleweka basi anapangiwa njia ambazo hazina mshiko, yaani daladala ni chache na magari mengi huko ni ya viongozi na mabalozi ambao kuwapiga bao yataka moyo :_'+++
   
 7. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Labda wawekewe sheria ya kutokuwa na magari ya biashara
   
Loading...