Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa, bado linaendelea kumsubiri Ndg. Humphrey Polepole aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.
Ndg. Humphrey Polepole alitumiwa barua ya wito kwa mujibu wa Sheria za nchi aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili atoe maelezo kuhusiana na tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia Mitandao ya Kijamii lakini hadi leo hajatekeleza maelekezo hayo kwa mujibu wa Sheria.
Jeshi la Polisi limeona taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii na ndugu zake kuwa ametekwa, tayari tumeanza kufanyia kazi taarifa husika ili kupata ukweli wake.
Imetolewa na:
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania
Pia soma
- Tetesi: - Humphrey Polepole ametekwa leo asubuhi Oktoba 6
- Kaka yake Humphrey Polepole athibitisha kutekwa kwa ndugu yake (Polepole) na mtu anayefahamika kama Mafwele