Polisi bado hawajaona kama kutatokea uvunjifu wa amani?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Malisa Godlisten

Kama tungekua na jeshi la Polisi lenye weledi, hadi kufikia leo ilitakiwa mkutano mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika July 23 uwe umeshazuiwa.

Kitendo cha UVCCM kujibu kauli ya BAVICHA ni ishara ya wazi kuwa siku hiyo kutatokea "machafuko".

Wakati BAVICHA wanajipanga nchi nzima kwenda kuzuia mkutano huo, wenzao UVCCM wanajipanga kwenda kuwadhibiti BAVICHA.

So haihitaji intelijensia kujua kwamba lazima kutatokea vurugu. Sasa kwanini Polisi wasitumie busara kuzuia mkutano hadi maridhiano yafikiwe?

Au Polisi bado hawajaona kama kutatokea uvunjifu wa amani? Intelijensia yao ipo likizo?
 
Attachments

  • 13438884_1078178538940504_5837099722414862793_n.jpeg
    13438884_1078178538940504_5837099722414862793_n.jpeg
    11.9 KB · Views: 36
Intellijensia yao inagundua zaidi uvunjifu wa aman pindi ukawa wanapotaka kufanya mkutano.polis kaz yao kulinda aman sio kuzuia,nadhan IPO haja kibali cha mkutano kitolewe na mahakamana sio policeccm
 
Busara na hekima zinahitajika kutatua haya.
Viongozi wetu wakat mwingine wanatoa kauli na maagizo halaf mwisho wa siku wanaenda kinyume.
Huwez kuwaambia watoto wako leo hatulii, tumefunga halafu ww baba unakula. Hiv, unafikiri watakuelewa?
Viongoz mchunge kauli zenu na pia mabavu hayaleti suluhu.
 
RIP BAVICHA katika safari yenu ya kwenda kuzimu. Lkn ni bora mtumie mbinu nyingine hii inawapoteza.
 
Maraisi wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu, Raisi, Waziri mkuu, waziri wa ulinzi, waziri wa mambo ya ndani wote wapo pale nyie tieni timu tu kitajulikana hapo hapo
 
Ndugu zangu hali ya kiusalama kwa sasa ni tete hapa nchini kwani kumekuwepo vitendo vingi vya uvunjifu wa Amani vinavyo fanywa na walifu hatari.

Huko Kagera juzi tuu magaidi wamezingira kijiji na kufanya uhalifu pamoja na kupora Mali za RAIA na kuwajeruhi. Interejensia ya polisi haikuweza kujua kutokea kwa uhalifu huo mpka umetendeka.

Ukiachilia mbali tukio hilo, lile gaidi hatari lililokuwa likishikiliwa na polisi huko Mwanza likihusishwa na mauaji ya msikitini na huko Tanga limetoroka mikononi mwa polisi na halijulikani liko wapi na linapanga uhalifu wapi.

Kwa hali kama hii sio busara kabisa kuruhusu mikusanyiko ya watu Kama jeshi la polisi lilivyo tangaza kwani hawa magaidi hupendelea sana kufanya uhalifu maeneo ambayo wanasiasa tu wanapo kusanyika na sio kwingineko.

Na tunashukuru Mungu haya magaidi kufanya uhalifu kwa wanasiasa tuu, maana wangekuwa wanashambulia hata mikusanyiko ya kidini au michezo tungeumia wengi sana. Tunaomba Mungu waendelee kushambulia mikusanyiko ya kisiasa tuu hivi hivi.

Kwahiyo nimeona maamuzi ya BAVICHA ya kuungana na jeshi la polisi kuzuia mkutano Wa cccm yamejaa uzalendo Wa kweli na wa kishujaa kwa taifa Lao. Jukumu la ulinzi Wa nchi hii ni letu sote BAVICHA wameonesha mfano tuwaunge mkono.

Tukiwaacha ccm wafanye mkutano haramu halafu wakavamiwa na magaidi sisi sote tutalaumiwa kwa kuto kuchukua hatua za kuzuia uhalifu kutendeka. Tusingependa wenzetu wayapate madhara kwani sisi ni ndugu na tunawapenda sana waendelee kuishi..

Ccm waelewe tuu BAVICHA pamoja na jeshi la polisi hawazuii mkutano wao kwa nia mbaya bali ni kulinda usalama wao na mali zao wakiwa kama RAIA wema.
 
A Town tumejipanga TUMEJIANDIKISHA 2354 na TUKO NA MABASI TUNATEGEMEA KUANZA SAFARI TAREHE 21 MABASI YAMEISHALIPIWA.TUNAKUJA KUWASAIDIA POLICE.

swissme
 
Utasikia intelijensia ni salama kabisa hivyo kila kitu kitaendelea kama kilivyopangwa
 
Inaonekana wewe undo upend wa Agape ambayo kwa bahari mbaya sana wao hawana. Mungu akubariki sana
 
Ndugu zangu hali ya kiusalama kwa sasa ni tete hapa nchini kwani kumekuwepo vitendo vingi vya uvunjifu wa Amani vinavyo fanywa na walifu hatari.

Huko Kagera juzi tuu magaidi wamezingira kijiji na kufanya uhalifu pamoja na kupora Mali za RAIA na kuwajeruhi. Interejensia ya polisi haikuweza kujua kutokea kwa uhalifu huo mpka umetendeka.

Ukiachilia mbali tukio hilo, lile gaidi hatari lililokuwa likishikiliwa na polisi huko Mwanza likihusishwa na mauaji ya msikitini na huko Tanga limetoroka mikononi mwa polisi na halijulikani liko wapi na linapanga uhalifu wapi.

Kwa hali kama hii sio busara kabisa kuruhusu mikusanyiko ya watu Kama jeshi la polisi lilivyo tangaza kwani hawa magaidi hupendelea sana kufanya uhalifu maeneo ambayo wanasiasa tu wanapo kusanyika na sio kwingineko.

Na tunashukuru Mungu haya magaidi kufanya uhalifu kwa wanasiasa tuu, maana wangekuwa wanashambulia hata mikusanyiko ya kidini au michezo tungeumia wengi sana. Tunaomba Mungu waendelee kushambulia mikusanyiko ya kisiasa tuu hivi hivi.

Kwahiyo nimeona maamuzi ya BAVICHA ya kuungana na jeshi la polisi kuzuia mkutano Wa cccm yamejaa uzalendo Wa kweli na wa kishujaa kwa taifa Lao. Jukumu la ulinzi Wa nchi hii ni letu sote BAVICHA wameonesha mfano tuwaunge mkono.

Tukiwaacha ccm wafanye mkutano haramu halafu wakavamiwa na magaidi sisi sote tutalaumiwa kwa kuto kuchukua hatua za kuzuia uhalifu kutendeka. Tusingependa wenzetu wayapate madhara kwani sisi ni ndugu na tunawapenda sana waendelee kuishi..

Ccm waelewe tuu BAVICHA pamoja na jeshi la polisi hawazuii mkutano wao kwa nia mbaya bali ni kulinda usalama wao na mali zao wakiwa kama RAIA wema.
Basi bora bavicha na uvccm waafikiane kulindana kipindi wanapokuwa kwenye mikutano kama ilivyokuwa kwa waislam na wakristu dhidi ya boko haram.
 
Back
Top Bottom