POLISI ARUSHA WAINGIA LAWAMANI

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
180
MADUDU YAIBUKA POLISI ARUSHA,OFISI YA RCO YAINGIA LAWAMANI. (PART 1)

Mwandishi wetu,Arusha

Hali ya sintofahamu imeibuka katika ofisi ya mkuu wa upelelezi mkoani Arusha mara baada ya ofisi hiyo kudaiwa kushikilia hatimiliki ya kiwanja cha mfanyabiashara maarufu wa utalii jijini Arusha,Mathew Mollel kwa kipindi cha miaka miwili kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi hadi sasa.

Hatimiliki hiyo ni ile yenye nambari za usajili 22906 mali ya mfanyabiashara huyo mkazi wa jijini Arusha ambayo ilikabidhiwa polisi kwa sababu za kiuchunguzi na wakili wa mfanyabiashara huyo ,Duncan Oola mnamo …..mwaka 2014 mbele ya ofisi hiyo.

Vyanzo vya habari vimedai ya kwamba kushindwa kuachiwa kwa hati hiyo kunatokana na kigogo mmoja(jina limehifadhiwa) kutoka ofisiya mkuu wa upelelezi mkoani Arusha ambaye anatajwa kuwa na maslahi katika sakata hilo.

KIGOGO HUYO NI NANI?

STELLA-huyu ndiye kigogo anayetajwa anaitwa STELLA ni mweusi kwa rangi ya mwili mrefu kwenda juu,cheo chake ni mkuu wa upelelezi msaidizi mkoani Arusha(ASS,RCO ARUSHA)..kwa muda mfupi amepata utajiri wa kushtukiza,amejenga nyumba kubwa ya kifahari maeneo ya anaendesha gari aiana ya Toyota Prado new model rangi nyeusi ,ni mwanamke anayejiamini katika utendaji wake wa kazi lakini utajiri wake wa ghafla unatia shaka.

Ni mwanamke pekee katika ngazi ya jeshi la polisi mkoani Arusha anayeshikilia nyadhifa kubwa… ni mpole lakini ni hatari ni vyema vyombo husika vikatoa nafasi ya uchunguzi dhidi yake kwa kuwa ni mtumishi wa umma lakini pia kwa maslahi ya taifa na jeshi la polisi.

ENDELEA NA HABARI….

MAELEZO YA MATHEW MOLLEL.(huyu ni mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya shuttle ya Raimbow tours & shuttle) ambayo ipo maeneo ya hoteli ya New Safari Hotel kwa watu wake wa karibu wanasema ni mtu mpole,mcheshi na mchangamfu,kuna taarifa kwamba ameoa nyumba moja na DANHI MAKANGA ambaye ni mkuu wa wilaya na mbunge mstaafu yaani wameoa nyumba moja huko wilayani Bariadi mmoja ameoa mkubwa na mwingine ameoa mdogo mtu.





Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha mfanyabiashara huyo alilalamikia kitendo cha kupigwa“danadana” na ofisi hiyo muda wote anapofika mbele ya ofisi hiyo kuchukua hati yake kitendo alichodai anamwomba mwanasheria mkuu wa serikali,George Masaju kuingilia kati.

Akisimulia chanzo cha kushikiliwa kwa hati hiyo Mollel alisema kwamba mnamo mwaka 2014 alishikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa kosa la kughushi mukhtasari wa serikali ya kijiji cha Levolosi kwa lengo la kujipata hatimiliki ambapo ofisi hiyo ilimuamuru kuiwasilisha hati hiyo mezani.

Hatahivyo,alisema kwamba mara baada ya tukio hilo alifunguliwa kesi ya jinai na jamhuri nambari 1611 ya mwaka 2014 katika mahakama ya wilaya ya Sekei ambapo alishinda kesi hiyo iliyoamriwa na hakimu mkazi Chrisanta Chitanda.

Hatahivyo,alisema kwamba mara baada ya kushinda kesi hiyo aliwasilisha ombi la kupatiwa hati miliki hiyo kupitia kwa wakili wake lakini hatahivyo polisi walimwambia bado wanafanya uchunguzi kuhusu suala hilo.

Mollel,alisema kwamba mnamo mwezi Novemba mwaka jana alifunguliwa tena kesi katika mahakama ya ardhi na nyumba yenye nambari za usajili 160 ya mwaka 2015 lakini alishinda tena katika hukumu iliyotolewa na mwenyekiti wa mahakama hiyo,Cyriacus Kamugisha.

“Nimewashinda kesi mara mbili katika mahakama tofauti tofauti lakini cha ajabu kila nikienda polisi kuomba hati yangu wananipiga kalenda sijui wana malengo gani naomba serikali inisaidie”alisema mkazi huyo

Hatahivyo,alisema kwamba mara baada ya “danadana”hiyo yeye pamoja na wakili wake waliamua kwenda kulalamika kuhusu kitendo hicho katika ofisi ya mwanasheria mkuu wa kanda ya kazkazini ambapo walipewa barua iliyowaelekeza kwenda kuchukua hati yake polisi.

Huku akionyesha barua hiyo yenye Kumb Nambari AGC/AR/PCF.VOL.I/2015/100/6 ya mnamo desemba 18 mwaka huu iliyosainiwa na wakili wa serikali mfawidhi Elizabeth Swai kwa niaba ya mwanasheria mkuu wa kanda mfanyabiashara huyo alisema kwamba pamoja na kuiwasilisha barua hiyo polisi lakini amekuwa akiambiwa asubiri atapewa hati yake.

“Kwa sasa unaweza kwenda kuchukua hati miliki ya kiwanja iliyochukuliwa kwa mteja wako ambayo iko polisi kwa hatua zako muhimu”ilisema sehemu ya barua hiyo ambayo gazeti hili lina nakala yake

Akihojiwa na gazeti hili wakili wa mfanyabishara huyo,Oola alisema kwamba mara baada ya kupokea barua hiyo walifuata maelekezo na kisha kufika mbele ya jeshi hilo kuchukua hati hiyo lakini hawakupewa ushirikiano na ofisi ya mkuu wa upelelezi mkoani Arusha.

MAELEZO YA DPP ARUSHA.

JUMANNE RAMADHAN ambaye ni mwanasheria mkuu wa serikali mkoani Arusha mara kwa mara ameulizwa suala hili na kusema kwamba ofisi yake ilitoa barua kwa wakili wa Mollel(DUNCAN OOLA) lakini majibu yake ni kwamba ofisi yake inafuatilia utekelezaji wa barua iliyotumwa polisi.


MAELEZO YA RPC ARUSHA.

LIBERATUS SABAS-Huyu ni kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha ni mchapakazi sana kamanda huyu lakini kiumri hawezi kumudu kasi ya kudhibiti uhalifu na wahalifu mkoani Arusha.

Sabas kwa taarifa za ndani yuko mbioni kustaafu utumishi serikalini lakini hata kama angekuwa hastaafu hasingeweza kuingilia kati sakata hili kwanza ni kwasababu analindwa na mfumo alioutengeneza polisi Arusha wa kulindana.

Hatuwezi kusema kwamba hatambui suala hili lakini ni kwamba taarifa za maandishi ya barua zilizofikishwa polisi alipatiwa nakala ya kila barua lakini taarifa zinasema kwamba zilikuwa zikifikishwa ofisini kwake wasaidizi wake wanazificha kwa maslahi yao binafsi.

USIKOSE PART 11 KESHO TENA.

(Katika sehemu ya pili kumbuka tutakuletea kwanini DANHI MAKANGA mkuu wa wilaya ya zamani na mbunge mstaafu anahusishwa na sakata hili).

Lakini pia tutakuletea maelezo ya kamishna wa ardhi msaidizi na msajili wa hati kanda ya kazkazini katika sakata hili…wanazungumziaje suala hili lakini pia namna wanavyotambua sheria zinatumikaje katika sakata hili.

Kumbuka pia jambo la muhimu katika sakata hili tutabandika barua ya mwanasheria mkuu wa serikali kwenda jeshi la polisi mkoani Arusha ili na wewe ujishuhudie namna mvutano ulivyo baina ya polisi na ofisi ya DPP Arusha.

ALAMSIKI…………..
 
Back
Top Bottom