Polisi ajiua kwa risasi kituoni

Polisi ajiua kwa risasi kituoni

G 4real

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
454
Reaction score
212
Tabora. Polisi aliyefahamika kwa jina la Charles mwenye namba H 3416 wa Kituo cha Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, amejiua kwa kujipiga risasi akiwa ndani ya kituo.

Kwa mujibu wa taarifa, Charles alikuwa kazini na alijiua Jumamosi usiku na sababu za kujiua kwake hazijafahamika.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi walio jirani na kituo hicho, walisema tukio hilo lilitokea saa moja jioni.

"Nilikuwa nyumbani ghafla nikasikia mlio wa risasi katika kituo cha polisi na nilipokwenda nilimkuta askari Charles amekufa kwa kujipiga risasi," alisema Furahisha Felix.

Wananchi hao walisema kutokana na hali hiyo walilazimika kuwauliza baadhi ya askari waliokuwa naye zamu, ambao nao walidai hawajui sababu za mwenzao kuchukua uamuzi huo.

"Haiwezekani polisi ajiue na isijulikane sababu, hilo halipo, lazima kuna jambo limejificha,"alidai mkazi mwingine Amani Ibrahim.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda alisema: "Ni kweli askari huyo amejiua wakati akiwa kituoni saa moja usiku, tunaendelea na uchunguzi kujua sababu za kifo chake,"alisema Kaganda.

Kamanda Kaganda alisema askari huyo hakuacha ujumbe wowote kueleza sababu za kujiua.

Kutokana na tukio hilo, alitoa wito kwa askari wote kwamba wanapokuwa na matatizo wayawasilishe kwa viongozi wao badala ya kujichukulia sheria mkononi.

Matukio ya polisi kujiua

Hili ni tukio la pili la askari kujiua ndani ya kituo kwa mwaka huu, huko wilayani Mbozi mkoani Mbeya, polisi mwenye cheo cha Sajenti, D 4179 Partick Gondwa (54), alijiua kwa kujipiga risasi akiwa ndani ya kituo.

Askari huyo ambaye, pia alikuwa ni mtunza vielelezo kwenye kituo hicho cha Polisi Wilaya ya Mbozi, inasemekana alijipiga risasi kwa kutumia bastola ambayo nayo ni kielezo kilichokuwamo ndani ya chumba hicho.

Katika miaka ya karibuni, askari wa Kituo cha Polisi Karagwe mkoani Kagera, G 901PC Abel Mwakivamba (33) alijiua kwa kujipiga risasi akiwa lindoni kwenye Benki ya CRDB-Karagwe.

Jijini Dar es Salaam, polisi mmoja alijiua kwa kujipiga risasi kichwani akiwa na wenzake kwenye lindo.

Taarifa zilidai kuwa askari huyo kabla ya kuchukua hatua hiyo alikuwa akilalamikia kitendo cha wabunge kujipandishia posho hadi Sh200,000 kwa siku, wakati yeye anaipata kwa mwezi, tena baada ya kulala sana nje na mapambano kadhaa ya risasi dhidi ya wahalifu.

Chanzo:Mwananchi
 
desperate non corrupt cops,wakina mahita wqlikuwa wanapiga dili na majambawazi!
 
Naam alikua na akili sana huyu, kaona Bora atangulie kuliko kutumwa kwenda kuwapiga ndugu zake kila siku bila kosa lolote
 
Ndio maana hawa jamaa si wa kujibizana nao wakiwa na silaha... Anaweza kukuua na akajiua kumbe alikua na stress zake.. Mi nilishakoma tangu ninusulike kisa parking eti nimepaki vibaya
 
Ndio maana hawa jamaa si wa kujibizana nao wakiwa na silaha... Anaweza kukuua na akajiua kumbe alikua na stress zake.. Mi nilishakoma tangu ninusulike kisa parking eti nimepaki vibaya
Angekuwa rubani wa ndege ya rais.....na hivi hapa kwetu hakuna utaratibu wa kuwapima afya ya akil.
 
Dah! Huyu jamaa namfahamu, nimegraduate nae chuo kimoja japo yeye alienda kuwa askari na mimi kuajiriwa sekta nyingine! R.I.P Charles
 
Hivi viongozi wanajiamini nini kulidwa na watu wenye maamuzi magumu kama hawa!!!,naamini ipo siku tutasikia mmoja kamla kichwa kiongozi muhimu wa nchi.

Unalindwa na mtu mwenye kinyongo na wewe kama huyu,halafu umebweteka unacheka cheka tu.
 
Dah! Huyu jamaa namfahamu, nimegraduate nae chuo kimoja japo yeye alienda kuwa askari na mimi kuajiriwa sekta nyingine! R.I.P Charles
 
Ndio maana hawa jamaa si wa kujibizana nao wakiwa na silaha... Anaweza kukuua na akajiua kumbe alikua na stress zake.. Mi nilishakoma tangu ninusulike kisa parking eti nimepaki vibaya

ilikuwaje huyo mkuu...nikiwa nimemaliza kidato cha nne miaka hiyo ya mwanzoni mwa 90 nilikutana na askari wa patrol usiku kama saa 2,ile napisha nao nikashangaa mmoja amenichapa kiboko eti napishana naye karibu namna hiyo ninataka kumnyang'anya bunduki...niliishiwa nguvu na toka siku hiyo siwapendi!!!!
 
Ndio maana maaskari ya zamani yalikuwa hayapolwi bunduki,sasa hawa wa siku hizi unapishana nae karibu anacheka cheka tu,unategemea nini?
 
Ndio maana maaskari ya zamani yalikuwa hayapolwi bunduki,sasa hawa wa siku hizi unapishana nae karibu anacheka cheka tu,unategemea nini?

mkorinto...umeniongeza hasira zangu...
 
Last edited by a moderator:
Isijekuwa ameuliwa na polisi wenzake kisha wakatengeneza picha kuwa amejiua.

Uchunguzi wa kina unahitajika
 
ilikuwaje huyo mkuu...nikiwa nimemaliza kidato cha nne miaka hiyo ya mwanzoni mwa 90 nilikutana na askari wa patrol usiku kama saa 2,ile napisha nao nikashangaa mmoja amenichapa kiboko eti napishana naye karibu namna hiyo ninataka kumnyang'anya bunduki...niliishiwa nguvu na toka siku hiyo siwapendi!!!!

Hii yako kali mkuu... Pole sana
 
Back
Top Bottom