kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,745
Katika Taarifa ya Habari ya saa 2 usiku StarTV nimeona na kusikia habari inayohusu Polisi 3 kutaka kumbambikia kesi mfanya Biashara kumuhusisha na Fuvu la binadamu kilichonishangaza ni huyu afisa wa Polisi aliyekuwa akitoa habari kwa kusema uchunguzi unafanyika ili kujua kama Fuvu lile ni la binadamu au Mnyama, hivi kweli Watanzania wote tulishuhudia siku ya tukio likionyeshwa fuvu la Binadamu lililokuwa likitoa harufu kwani watu walikuwa wakishika pua na nzi walikuwa wengi. kwa kauli hii ya huyu afisa wa polisi anataka kutuambia nini watanzania uchunguzi upi unafanyika wakati uhalisia wa lile fuvu ulionekana, cha muhimu wangefanya uchunguzi kujua lile fuvu ni la nani aliyekufa na alikufaje na wapi?Nawasilisha!