Police trafiki Arusha mtusaidie

Police trafiki Arusha mtusaidie

Gerad2008

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2009
Posts
583
Reaction score
287
Arusha ni mkoa ambao kwa kiasi kikubwa watumia vyombo vya usafiri wamekuwa wakijiendeshea vyombo hivyo kiholela bila kujali taratibu za uendeshaji na hii inasababisha traffic jam ambayo siyo ya lazima.
Mfano:
A:
Wakati wa jioni kuanzia saa 11 hadi saa 2.00 usiku maeneo ya kuanzia Christ church hadi jakaranda kwenye barabara ya Kijenge - Impala - Moshono, Hiace za abiria zimekuwa na tabia za kutanua na kwenda kuchomekea magari mengine yaliyoko njia kuu na kusababisha jama eneo la Gold crest yaani junction ya barabara ya Haile selasie.
Pamoja na kuwa hii imekuwa kero kubwa huwezi mwona askari yoyote anayesimamia kuhakikisha vurugu hizi zinakomeshwa.

B:
Kwenye hii hii barabara asubuhi kuanzia kituo cha mafuta cha Lalaa hadi junction ya kutoka Kijenge Juu kunamsongamano mkubwa wa magari na hii inatoka na matumizi mabaya ya barabara ya magari kuchepuka kushoto lilipo kanisa la Katoliki na wengine kuchepuka kulia mbele ya bonite na magari yote kujichomeka tena ilipo junction ya kijenge juu.
Hali hii inasababisha magari yaliyoko njia kuu ya lami toka Moshono kuja mjini kushindwa kutembea na wakati mwingine kutoka kwa lalaa hadi daraja la kijenge inaweza chukua hata dakika 20.
Tunatoa ombi lifuatalo:
1. Tunaomba trafiki wasimamie watumia vyombo vya usafiri waweze ku-comply na taratibu za barabarani bila kuwaumiza na kuwachelewesha wanaofuata sheria za usalama barabarani ikiwamo kuzuia Hiace zinazotanua kutoka Christ church hadi Jacaranda.
2. Tunaomba wale trafiki wanaosimama pale impala na kujikamatia magari asubuhi wasogee hadi pale kijenge chini watakamata wahalifu wengi wanaovunja sheria za usalama barabarani na kwa kusababisha msongamano usio na maana.

3. Trafiki wakisimamia vizuri magari barabarani nyakati za jioni na asubuhi wataweza kuingiza kipato kikubwa kupitia faini halali kuliko kuonekana barabarani tu kuanzia saa nne hadi saa 8 na kukamata makosa ambayo hayana hata madhara makubwa kwa watumiaji wengine wa barabara.

4. Trafiki wa Arusha mjini uwepo wenu na umuhimu wenu unatakiwa uonekane asubuhi na jioni mkishughulikia waendeshao magari ovyo na hapo kama ni mapato ya serikali yangeongezeka kwa kiasi kikubwa.

5. nawashauri pia trafiki washughulikie makosa yenye substance na yatakayorudisha heshima ya trafiki na si vitu vidogo vidogo vinavyoweza kuwavunjia heshima.
 
Daah Chuga kunakuaga na matrafiki wengi balaa,mpk maguta wanakamata tu aisee
 
Kareport traffic makao makuu hapo arusha unaweza ukasaidiwa mkuu!!!

Ila co kwa msharaha huu mtu akae mpaka saa mbili usiku
 
Namuunga mkono mleta mada. Wiki mbili sasa ninatumia dakika zaidi ya ishirini kutoka sheli ya lala mpaka round about ya impala umbali usiozidi 1.5km. Madereva na sio wa hiace tu, wanakiuka sheria wanaendesha kwenye service road pande zote mbili kuchelewesha madereva wanaofuata sheria.

Juzi niliwaeleza hao traffic wanaosimama hapo impala nikadhani wangeshughulikia hili tatizo lakini hali iko hivyo hivyo jana na leo.
 
5. nawashauri pia trafiki washughulikie makosa yenye substance na yatakayorudisha heshima ya trafiki na si vitu vidogo vidogo vinavyoweza kuwavunjia heshima.

MAKOSA YENYE SUBSTANCE NI YAPI MKUU, TUJUZE
 
Vitu vingine ni vigumu Kwa Trafic kumkamata na kosa Dreva , maana uanzia barabara ya Kijenge juu hadi sheli ya Kwa lala kuna maduka Na huduma nyingine hivyo wenye magari wanauamuz wa kutumia hiyo nia kupata huduma zao kitu ambacho sio kosa kisheria
 
Boda boda wanaachwa wapite kwenye vivuko vya waenda kwa Miguu ....yaani kwa ufupi utumiaji wa barabara uko kiholela sana
 
Pia watoe elimu kwa madereva wanapotumia hizi barabara mpya za double road kuwa, upande wa kulia ni magari yaendayo speed kidogo na kushoto ni kwa magari yaendayo taratibu .Sasa unakuta Leyland au fiat la magogo liko kulia limejaza mbao speed 5 na kusababisha jam. Muwe waelewa madereva wa Arusha huruhusiwi Ku overtake kushoto.
 
Nawashauri tu mm waache uonevu,askari anakukamata kwa kosa ka shockp wakati kuna watu wana over rap wanasababisha jam
 
Back
Top Bottom