Polepole unaikumbuka ‘Legitimacy

Polepole unaikumbuka ‘Legitimacy

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,291
pic+polepole.jpg


Legitimacy inaweza kutafsiriwa katika muktadha wa kisheria au uhalali wa kisiasa. Kwanza ni ile hali ya mwanasiasa anavyotazamwa katika jamii, uhalali wake kwa watu. Anakubalika vipi kimaadili, uongozi na vigezo vingine vinavyoshawishi kiongozi anayefaa.

Muktadha wa pili ile hali ya kiongozi kuwa na mamlaka ya kuamua jambo au mambo kisheria. Katika Makala haya, nitazungumzia Legitimacy katika muktadha wa uhalali wa kisiasa kwa watu anaowaongoza.

Tafsiri hii ilielezwa kwa kinaga ubaga na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alipokuwa akiendesha vita ya kumwangusha Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa asipate nafasi ya kuiona Ikulu.

Polepole aliyejizolea umaarufu zaidi katika mchakato wa Katiba mpya, baadaye aligeuka mkosoaji wa Chadema na Ukawa baada ya kumpitisha Lowassa kuwa mgombea urais wake. Lowassa alihama CCM baada ya jina lake kukatwa kwa madai ya kuwa na madoa kisiasa.

Agosti 9, 2015, saa tatu usiku kupitia kipindi cha Mada Moto, kinachorushwa na Channel Ten, Polepole alikutana meza moja na mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kujadili mada iliyohusu ‘Edward Lowassa ndani ya Ukawa’.

Polepole alijenga hoja kwa kutumia msamiati wa Legitimacy na alitumia njia zote za mawasiliano katika mjadala ule, kuanzia hisia hadi kauli ambazo ziliingia kwenye kumbukumbu yangu.

Polepole alijenga hoja kwamba Lowassa ana madoa na hana uhalali wa kupewa dhamana na Watanzania kuongoza Taifa hili. Polepole akasema kama CCM ingeendelea na watu wenye madoa wangeambukiza na wengine. “Mtu huyu hafai kuwa kiongozi wa Taifa letu (Lowassa) kwa sababu ya maadili na huwezi kusema tunasuburi mahakama ithibitishe. Kuna tofauti kati ya Legality na Legitimacy, kwenye siasa kuna Legitimacy, haihitaji wewe tukusafishe kisheria ili tuseme wewe ni muadilifu, Legitimacy ni namna unavyoishi, Legitimacy haipimwi mahakamani.” mwisho wa kunukuu.

Hata hivyo, ni miezi 26 tu imepita tangu Polepole alipozungumzia Legitimacy kwa kiongozi. Siku chache zilizopita wateule watatu wa Rais John Magufuli na kada wa CCM katika halmashauri mbili mkoni Arusha wameingia kwenye kashfa ya tuhuma za rushwa.

Lakini, Polepole amenukuliwa na baadhi vyombo vya habari akiwataka wanaotuhumu CCM kutumia rushwa kununua madiwani watoe ushahidi hadharani.

Polepole anasisitiza madiwani hao wanahamia CCM kwa ushawishi wa Rais Magufuli kupitia utekelezaji wa sera na ilani ya chama.

Hata hivyo, video na sauti zilizoonyeshwa hadharani na wabunge Joshua Nassari na Godbless Lema zimeonyesha na kusikika wateule hao wakiwashawishi madiwani kuhama Chadema ili wajiunge CCM na baadhi waliahidiwa wangelipwa posho za vikao vyao vilivyobaki hadi 2020 na kukamilishwa miradi yao.

Kinachonishtua ni hii tafsiri ya Legitimacy aliyotumia kama silaha katika kipindi cha kumpata kiongozi wa Taifa na kuacha kutumika baada ya video kuwaonyesha wateule hao wakishawishi madiwani.

Sijamsikia Polepole akizungumzia au kukemea au kuahidi kuchukua hatua yoyote ile na kuhoji nini kimemkuta?

Kilichoshangaza mmoja wa wanaodaiwa kuhusika na kashfa ya kununua madiwani kashinda uongozi kwenye uchaguzi wa CCM. Hii ndiyo Legitimacy uliyokuwa unataka kuwaaminisha Watanzania? Ni wewe Polepole uliyekuwa unakemea rushwa uchaguzi wa ndani?

Ni heri kushauri ukweli ukanusuru chama kuliko kukaa kimya ukapoteza uaminifu kwa chama hapo baadaye. Siasa ni hesabu ya utafutaji uhalali wa kisiasa na ukusanyaji wa mitaji. CCM inapoharibu, upinzani unahesabu mtaji imara katika uchaguzi ujao 2020. Itafakari upya Legitimacy.
 
yule ni mnafki ata asikusumbue anabadilika kama kinyonga.

aliwai kusema cheo cha ukuu wa wilaya kifutwe alivyokipata akafunga bakuli.

humphrey Pole Pole anaweza akatapika na akala matapishi yake MPUUZE.
 
Hatuna loyalty kwa mawazo na misimamo yetu.

Uko upande A una interests hizi hapa, je ukifika upande C ukawa na interests zile kule utaendelea kua muumini na loyal kwa mawazo na misimamo yako?

Hiki kinamkumba kila mwenye lengo la kuhakikisha kitumbua chake hakitiwi mchanga.
 
Lowassa alihukumiwa na kamati ya bunge...
Usifananishe ya lowassa na hizi comedy za kina lema.

Usitake kutuhalalishia ufisadi uliokataliwa 2015.
 
Akili za polepole ni matunda ya serikali ya awamu ya tano na chama cha mapinduzi
 
Hii ndiyo ile kitu inayoitwa NGUMU KUMEZA.
Hata uwaziri wa KANGI LUGORA chini ya LEGITIMACY ya bwana POLEPOLE hapati nafasi.

Lakini kwa mwenye ufahamu hapa ndo unapata kipimo halisi cha WIVU,UNAFIKI,UONGO,POROJO ,VISASI, na USOKOROKWINYO huku mtetea hoja akijidai ni mzalendo kupita wananchi wengine.

Ahsante saana kwa kunifundisha ,ulilojifunza toka kwa Mwl Polepole matumizi ya neno LEGITIMACY.
 
Lowassa alihukumiwa na kamati ya bunge...
Usifananishe ya lowassa na hizi comedy za kina lema.

Usitake kutuhalalishia ufisadi uliokataliwa 2015.

Kwani hata muhongo kipindi cha escrow mlikubali kuwa anahatia? Magufuli alimpa tena uwazir licha ya kutolewa kwa ufisad bado jinamizi lilelile lilimrudia.
Kafulila nae aliambiwa analeta comedy kwa sasa magufuli anamtambua kama shujaa hiyo ndio ccm sasa muda utaingea suala la lema na nasar
 
Tutayaona mengi..Ubunifu unaendelea.
Kusimamishwa barabarani na wananchi (Hapo kuna hadi vipaza sauti vishafungwa0...
Kuandikiwa mabango....
Madiwani kuhama...
Dangote hajui sera za uwekezaji.....
Tuhamie Dodoma ofisi UDOM....

UBUNIFU UNAENDELEA
 
Back
Top Bottom