Polepole kazungumza, J.Makamba Je!

Sikia nikuambie,
Hata mimi ninatamani sana uhai wa serikali hii uwe ukingoni, ila nachokuambia huo ukingo hauko mwaka huu wala muongo huu. Madudu waliyoyafanya wanajua fika kua wakitoka tu madarakani hawatobaki salama. Pia kingine hii nchi ina rasilimali nyingi tu ambazo serikali hii inataka iendelee kuzifaidi milele na milele. Ndio maana kwa gharama na mbinu zozote zile wanahakikisha wanaendelea kubaki madarakani.

Sioni mikakati yoyote ya kuitoa hii serikali ikifanikiwa kwa sasa au hivi karibuni. Serikali hii inafanya chochote kile inachoweza kuhakikisha inabaki madarakani. Polepole anachoongea sio kitu kipya. Humu JF tuna misemo kama Policcm tukimaanisha CCM na Police lao ni moja. Kwamba NEC inaibeba CCM pia sio kitu kipya, tumeanza kuongea miaka na miaka, kuna lililobadilika??

Kwamba kuna waliokua wakijumlisha matokeo pale KIitonyama wakakamatwa na Computer zao kuchukuliwa sio kitu kipya, tumeongea na kuongea, tukaandika na kuandika, wale walionekana watatoa matokeo sahihi yanayokinzana na tume wakawekwa ndani kwanza uchaguzi upite.

Uchaguzi utafika, wataingia tena chama kile kile, miaka na miaka. Yaani tunapita, wanakuja wengine styles ni zile zile, hakutakua na matokeo mapya. Albert Einstein bado anasifika kwa kutukumbusha kua huwezi kurudia kuweka "inputs" zile zile ukategemea kupata "Outputs" tofauti.
 
Following… interesting kwa kweli
 
....kuliko achokoze...
Blackmailing ni hatari sana....! Unadhani, 'absa' kuchukua kipande cha mfuko wetu wa ngawila kilimuacha salama ukichichimama ukikaa mchale...? Kwa hiyo, omba usikumbane na blackmailing...hutoboi kama huna namna ya 'kusukua' mtego huo.
 
January Makamba mwepesi sana, kama kuna mtu ana hotuba yoyote ya Makamba akiwa bungeni au nje akizungumza kuhusu ishu yoyote inayogusa mwanachi wa kawaida.

Makamba na Halima Mdee wakiwa kwa debate Makamba ataonekana kilaza. Huu ni mfano tu.
 
Mkuu 'Doubleg Malafyale', asante sana kwa hiyo taarifa ya Makamba uliyo iweka hapa; lakini hiyo 'version' ya "Coming to America" ni tofauti sana na ile aliyo iwasilisha JF wakati ule, miaka kadhaa nyuma. Ile 'version' ilizungumzia Tanzania 'specifically' na matumaini ya nchi na uongozi wake katika maendeleo ya wananchi wake.

Sijui kama 'version' ile bado watakuwa nayo JF; au pengine ni kati ya yaliyopotea wakati JF ilipopata misuko suko yake huko nyuma..

Nimesoma sehemu kubwa ya habari zake huyu Januari katika andiko uliloliweka; na sasa nimeelewa zaidi kwa nini amepata shida sana kushikilia nafasi zake katika serikali alizozitumikia. Nimepata mwanga zaidi kumhusu yeye; pamoja na makonakona mengi yasiyokuwa na maelezo sahihi ndani ya "stori" yake hii.

Kiujumla; baada ya kumsoma hadi nilipoishia; ni dhahiri kabisa kwamba yeye ndiye mtu sahihi zaidi wa kuyazungumzia aliyo yasema Polepole.

Namsihi sana aitazame Tanzania kwa wivu mkubwa zaidi ya ubinafsi wake na hayo makundi aliyo husika nayo ambayo baadhi ndiyo yaliyo tufikisha hapa tulipo fikia sasa hivi.

Ni wakati mzuri sana wa kujisafisha.
 
January Makamba mwepesi sana, kama kuna mtu ana hotuba yoyote ya Makamba akiwa bungeni au nje akizungumza kuhusu ishu yoyote inayogusa mwanachi wa kawaida.

Makamba na Halima Mdee wakiwa kwa debate Makamba ataonekana kilaza. Huu ni mfano tu.
Very interesting observation; ambayo nami ninge amini hivyo hivyo kabla ya kusoma bandiko lake hapo juu aliloweka mkuu 'Doubleg Malafyale'.
Sidhani kuwa Januari atakuwa ameandikiwa na mtu mwingine 'stori' yake hiyo. Kwa hiyo uwezo wa kujieleza anao; hata kama kuna mambo mengi yanaonyesha kuwa ya kupindapinda sana.

Inawezekana kabisa asiwe na uwezo wa kuzungumza; lakini uwezo wa kufikiri na kupanga vizuri anayoyafikiri katika uandishi wake inaonyesha uwezo huo anao.
 
Sasa tumeelewana vizuri mkuu 'Shark'; kwamba wewe na mimi tunayo tofauti kubwa sana juu ya hili.

Serikali ya Samia na Genge lake haina uhai zaidi wa kuendelea kuongoza nchi hii.
Tofauti kati yetu ipo hapa.
 
Inawezekana kabisa asiwe na uwezo wa kuzungumza; lakini uwezo wa kufikiri na kupanga vizuri anayoyafikiri katika uandishi wake inaonyesha uwezo huo anao.
Kwenye kuandika yuko vizuri sana, alikuwa anaandika hotuba za Kikwete, ishu anaandika kuhusu nini?

Mzee Ulimwengu, Askofu Bagonza ni waandishi wazuri sana, ila tofauti na Makamba maandiko yao yanaFocus kwenye upande ambao Makamba hawezi kuusemea hata pamoja na kuwa mwakilishi wa wananchi.

Kuzungumza na kujenga hoja ni jambo muhimu sana kwa mwanasiasa, msikilize Bashe kwa mfano.
 
Please do the right thing for your country, which is in a worse situation than it has ever been.
 
Sasa tumeelewana vizuri mkuu 'Shark'; kwamba wewe na mimi tunayo tofauti kubwa sana juu ya hili.

Serikali ya Samia na Genge lake haina uhai zaidi wa kuendelea kuongoza nchi hii.
Tofauti kati yetu ipo hapa.
Sawa mkuu,
Labda tukubaliane hivyo. After 5 years tutakuja kuhakikisha hili. Pengine Mimi nachukulia utaratibu wa siku zote ulivyo (by default) kumbe kuna jipya ambalo silijui.
 
Sawa mkuu,
Labda tukubaliane hivyo. After 5 years tutakuja kuhakikisha hili. Pengine Mimi nachukulia utaratibu wa siku zote ulivyo (by default) kumbe kuna jipya ambalo silijui.
Tuliachie hapa hili.
Itakuwa ni msiba wa kipekee kabisa kwa Tanzania kuwa chini ya utawala wa Samia na Genge lake kwa miaka mitano mingine.
Italazimu waendelee kuua waTanzania sana kulifanikisha hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…