Uchaguzi 2020 Polepole acha kuruka viunzi, tunataka utuambie kwa nini maisha yamekuwa magumu uraiani

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
3,166
4,581
Unazungumzia mambo ambayo yapo wazi kama ukaguzi wa ATCL, deni la taifa, sera za majimbo za CHADEMA hizi ni hoja zipo wazi. Na mwananchi wa kawaida sasa ambae maisha yake yamekuwa duni haya masuala uliofafanua hayana msaada kwake.

Tunataka utuambie kwa nini maisha yamekuwa magumu uraiani na kwa nini CCM haisadii wananchi?

Watu wana maisha magumu wanashindia mihogo ya kukaanga. Biashara zimefungwa na watu wanashindwa kujiajiri maana hamna uwezo wa watu kununua, ndio maana biashara zinakufa. Mbona haya hujafafanua na kutoa majibu maana wananchi wana hali mbaya sana. Alafu unaleta tabasamu la kinafiki sababu wewe una uhakika wa maisha.

74mntJbO_400x400.jpg
 
Baada ya makamanda kuonyeshwa "dokumenti" za bunge zinazohusu kupitishwa kwa bajeti za ujenzi wa Chato international airport, ununuzi wa ndege, ujenzi wa bwawa la kufua umeme la JK Nyerere nk sasa mmeamia kwenye "hela mfukoni" hahaha
 
Maisha yashakuaga maraisi lini? We unadhan tanzania kuna maisha magumu? ulishawahi kufanya kazi anywhere kwenye states za marekani? ushawahi kulipishwa kodi 60% wewe? maisha magumu yaskie tu.
 
Baada ya makamanda kuonyeshwa "dokumenti" za bunge zinazohusu kupitishwa kwa bajeti za ujenzi wa Chato international airport, ununuzi wa ndege, ujenzi wa bwawa la kufua umeme la JK Nyerere nk sasa mmeamia kwenye "hela mfukoni" hahaha

Jamaa polepole amejibu vizuri sana maswali leo, anatoa maelezo vizuri mtu unaelewa , sasa yule bwana amenikosha anasema mazao sio maendeleo.
 
Baada ya makamanda kuonyeshwa "dokumenti" za bunge zinazohusu kupitishwa kwa bajeti za ujenzi wa Chato international airport, ununuzi wa ndege, ujenzi wa bwawa la kufua umeme la JK Nyerere nk sasa mmeamia kwenye "hela mfukoni" hahaha
Sasa hizo ducoment zinamsaidia nini mama muuza mihogo au muuza ndizi ambae biashara imekuwa ngumu. Tumia akili we bwege.
 
Jamaaa ameongea point mno zote with evidence huenda kuna mengi wanayajua sema tumpe muda chadema wafakapo jibu tena fyoko atupe memgine zaid na kama wasipojibu watakuwa waongo kweli, na kama wakijibu wajiandae kupasuliwa zaid tena dakika za lala salama.
 
jamaaa ameongea point mno zote with evidence huenda kuna mengi wanayajua sema tumpe muda chadema wafakapo jibu tena fyoko atupe memgine zaid na kama wasipojibu watakuwa waongo kweli, na kama wakijibu wajiandae kupasuliwa zaid tena dakika za lala salama
Hili la mzunguko wa pesa kusinyaa na kusababisha ugumu wa maisha alitakiwa alizungumzie.
 
Hili la mzunguko wa pesa kusinyaa na kusababisha ugumu wa maisha alitakiwa alizungumzie.
pesa imesinyaa lakini siyo kwa kiasi tunachoaminishwa,fedha ipo na watu wanatumia fedha,na hata hela iliyotumika yote ipo kwenye miradi mikubwa ambayo mingi ishaaanza kurudisha fedha na mingine soon itaanza kutoa fedha katika kipindi kifupi kama Air tanzania,stiglor gorge n.k
 
jamaaa ameongea point mno zote with evidence huenda kuna mengi wanayajua sema tumpe muda chadema wafakapo jibu tena fyoko atupe memgine zaid na kama wasipojibu watakuwa waongo kweli, na kama wakijibu wajiandae kupasuliwa zaid tena dakika za lala salama
Mbona tunamwita Magufuli akatuelezee katika mdahalo atakaki?
 
Back
Top Bottom