Poleni wasomi wa SUA, CCM ni kero!

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,006
2,166
Ktk uchaguzi wa 1995 SUA kilikuwa kitovu cha Mrema wa NCCR. Habari zilisikika kwamba SUA Ilimkataa MKapa kwa zaidi ya 90%.

Baada ya hapo Serikali imekuwa na mizengwe na vyuo sasa vinawekewa makada kuviongoza. Tumeyasikia UD, UDOM na pia yamejitokeza SUA. Mwaka jana vyuo vikazuiliwa kufungua kwa sababu ya kugawa kura tu!


Sasa nasikia SUA wana uongozi mpya, mtiifu kwa Serikali na CCM. Sawa! Lakini mbona nasikia ubora wa uongozi ni zero?


Viongozi wa chuo hicho sasa wanazuia wanataaluma kwenda masomoni kwa misingi ya kisiasa. Wale wanaoonekana ni wanachama/watiifu wa CCM wanaruhusiwa, na wale wanaoikataa CCM hawapewi ruhusa. Mkuu mmoja nasikia kaulizwa hana sababu zaidi ya hasira kwa maswali.


Hicho Chuo kinaelekea wapi? Hivyo vyuo vya serikali vinaelekea wapi?
 
Back
Top Bottom