Poleni wasanii mnaoshabikia kulipwa redioni

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,829
15,791
Hivi huu mfumo wa kuwalipa wasanii ukianza kila wimbo unapopigwa msanii analipwa ni wasanii wangapi watasurvive?

Mi naona tutawapoteza wasanii wengi sana, sioni mtu kama 'Ruge Mutahaba' akubali kukulipa kirahisi rahisi msanii ambaye anaona huna ushawishi hata kama wimbo wako mzuri, huu mfumo naona utawanufaisha wachache tu hao kina Diamond na kina Kiba, ila hawa wengine wahesabu maumivu.

Tutarajie kuona redio kuanza kucheza zaidi nyimbo za kinaija na za mbele ili kukwepa kutoa mshiko kwa wasanii wa ndani, kwani redio zote zikikubaliana kutwanga nyimbo za kinigeria hazitasikilizwa?

Maoni yangu wasanii waachane na hili, watajuta, otherwise kama wana uwezo wa kucreate ushawishi kama kina Diamond.
 
nadhani hizo radio na TV zitakuwa zinatakiwa kuhakikisha zinapiga miziki ya ndani kwa asilimia kadhaa na ile ya nje kwa asilimia kadhaa!
 
Inawezekana hii? Kama ndivyo hapo nafuu
 
nadhani hizo radio na TV zitakuwa zinatakiwa kuhakikisha zinapiga miziki ya ndani kwa asilimia kadhaa na ile ya nje kwa asilimia kadhaa!

Hilo kulisimamia ni ngumu... Kenya wanao huo utaratibu, ila matokeo yake almost 80 ya nyimbo zinapigwa ni za nje, alizungumzia hili Niki wa pili siku walipokuwa wanaukataa huu mfumo...
 
halafu mwakajana nikasikia wamegoma eti kwanini media zinapiga sana nyimbo za nje hehe!
 
Ndio hivo, Nyimbo za diamond ndio zilikuwa zinapigwa kuliko msanii yeyote wa Kenya, kwa mbaaali sauti sol wakawa wanafuatia...
 
Hivi huu mfumo wa kuwalipa wasanii ukianza kila wimbo unapopigwa msanii analipwa ni wasanii wangapi watasurvive? Mi naona tutawapoteza wasanii wengi sana, sioni mtu kama 'Ruge Mutahaba' akubali kukulipa kirahisi rahisi msanii ambaye anaona huna ushawishi hata kama wimbo wako mzuri, huu mfumo naona utawanufaisha wachache tu hao kina Diamond na kina Kiba, ila hawa wengine wahesabu maumivu, tutarajie kuona redio kuanza kucheza zaidi nyimbo za kinaija na za mbele ili kukwepa kutoa mshiko kwa wasanii wa ndani, kwani redio zote zikikubaliana kutwanga nyimbo za kinigeria hazitasikilizwa? Maoni yangu wasanii waachane na hili, watajuta, otherwise kama wana uwezo wa kucreate ushawishi kama kina Diamond
Hii inachekesha, kila kitu tunaiga nje, inapokuja swala la kulipa, ghafla linaonekana haliwezekani
 
Hilo kulisimamia ni ngumu... Kenya wanao huo utaratibu, ila matokeo yake almost 80 ya nyimbo zinapigwa ni za nje, alizungumzia hili Niki wa pili siku walipokuwa wanaukataa huu mfumo...

Wasanii wa nje nao wanatakiwa kulipwa. COSOTA wakikomaa na hivyo vyombo wenyewe wataona ni heri kulipia muziki wa tanzania kuliko kulipia hiyo miziki ya nje. Suali ni je COSOTA imeingia mikataba na makampuni ya nje yanayofanana nayo ili hayo makampuni yakusanye pesa ya muziki wa bongo unaopigwa huko. Kwa mfano MCSK ya Kenya.
 
Hivi huu mfumo wa kuwalipa wasanii ukianza kila wimbo unapopigwa msanii analipwa ni wasanii wangapi watasurvive?

Mi naona tutawapoteza wasanii wengi sana, sioni mtu kama 'Ruge Mutahaba' akubali kukulipa kirahisi rahisi msanii ambaye anaona huna ushawishi hata kama wimbo wako mzuri, huu mfumo naona utawanufaisha wachache tu hao kina Diamond na kina Kiba, ila hawa wengine wahesabu maumivu.

Tutarajie kuona redio kuanza kucheza zaidi nyimbo za kinaija na za mbele ili kukwepa kutoa mshiko kwa wasanii wa ndani, kwani redio zote zikikubaliana kutwanga nyimbo za kinigeria hazitasikilizwa?

Maoni yangu wasanii waachane na hili, watajuta, otherwise kama wana uwezo wa kucreate ushawishi kama kina Diamond.
Kwani hizo nyimbo za nje hazilipiwi ? Nyimbo za nje zinalipiwa kwa hiyo Radio stations kupiga nyimbo ya nje ya Tz haiwasaidii kupunguza gharama, wengi wanatolea mfano wa Kenya, Kenya Diamond aliongoza na ndiye aliyelipwa pesa ndefu na si kwamba kuongoza kwa Diamond kumuwapunguzia wao gharama.
 
Huu mfumo ni mbaya na unaua muziki wetu, tusiangalizie kwa Mataifa yaliyoendelea. Kama Cosota wanataka kwanini wasibane kwanza kwa sehemu zinazotoa na kuruhusu mtu kudownload kwa malipo nadhani kidogo kidogo itaanza kuleta matunda.
 
Back
Top Bottom