Poleni ThisDay kwa msiba huu

Invisible

Robot
Joined
Feb 26, 2006
Posts
16,285
Reaction score
8,465

MAREHEMU REDEMPTUS ANGELO
(Picha kwa hisani ya blog ya Michuzi)


Wafanyakazi wa Kampuni ya Media Soulutions LTD (chini ya IPP Media) wachapishaji na waendeshaji wa magazeti ya ThisDay na KuliKoni wamekumbwa na msiba mzito wa ghafla wa mfanyakazi mwenzao, Redemptus Angelo ambaye amefariki Jumapili Agosti 01, 2010 Saa 4.00 usiku katika Hospitali ya Mwananyamala.

Marehemu alikuwa ni Mkuu wa kitengo cha Usanifu wa kurasa (Graphics Designer) na alikuwa anategemewa sana na Media Solutions hasa kuelekea katika hatua muhimu na nyeti ambayo kampuni hiyo inajiandaa kuifanya karibuni.

Taarifa za awali (kabla ya uchunguzi rasmi) zinadai kwamba marehemu kafa kwa sumu.

Sisi kama JamiiForums, tunapenda kutoa salaam zetu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na Uongozi mzima wa IPP Media & Media Solutions kwa msiba huu mzito.

Apumzike kwa amani
​
 
RIP Redeptus,

Raha ya milele umpe hee Bwana na mwanga wa milelel umwangazie, apumzike kwa amani amina
 
Je, polisi wanasemaje? Je, kuna sababu zipi?
 

Ni mgombea katika eneo lolote? alitangaza nia?. May his soul rest in peace amen.
 
Lo Poleni wafiwa na Media Solution. Kubenea na wale waandishi mahiri wa habari za kifisadi na mikanganyo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii mpo? Nawaombea Mungu awanusuru kwa kila hila ili muendelee kutuhabarisha.
 
Sisi kama JamiiForums, tunapenda kutoa salaam zetu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na Uongozi mzima wa IPP Media & Media Solutions kwa msiba huu mzito.
Sisi kama JamiiForums, tunatoa salaam zetu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na Uongozi mzima wa IPP Media & Media Solutions kwa msiba huu mzito.
 
poleni lakini msiwe na huzuni sana kwani kazi ya mungu haina makosa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…