Poleni sana UKAWA, hao ndiyo Wazungu!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Ukawa walifikiri Wazungu wangekinukisha dhidi ya nchi yetu, walikuwa na mategemeo makuubwa sana kumbe masikini ya Mungu Wazungu walikuwa wanawaridhisha tu, hamna cha vikwazo dhidi ya nchi yetu wala nini!

Raisi Sheni ameshaapishwa na tayari ameshaunda Serikali yake, Wazungu kimyaa, kwa kawaida Wazungu jinsi walivyo kama kweli wangeamua kulivalia njuga hili swala sasa hivi pangekuwa tayari hapatoshi, kungekuwa kila siku matamko ktk kwa Balozi zao, vyombo vya Habari vyote nje na ndani vingekuwa vinajadili nini kifanyike kwanza hata wangewaonya raia yao kuhusu hali ya usalama nchini mwetu n.k lkn wamekaa kimyaa!

Lakini waapi, kwanza ndiyo kila siku tunawaona Mabalozi zao wakikutana na Viongozi wa Serikali yetu kujadili mambo ya Kiuchumi, hili ni pigo lingine kwa ukawa, wamebakia kuwa wakiwa, Poleni sana!
 
Ilikuwa ndio hoja inayo watoa Kimasomaso
Hawana hoja mbadala
Hawa kiukweli sioni hata umuhimu wa kutoa Ruzuku kwa watu wasio jiongeza
 
hongereni kwa ushindi wa chama kimoja, hiyo tunaiita demokrasia iliyopevuka..
 
Hv ww una wadhifa up pale lumumba? Una kaz yoyote halali ya kukuingizia kipato? Maana muda wote unakesha humu ndani na hyo mipasho
 
...Raisi Sheni ameshaapishwa na tayari ameshaunda Serikali yake, Wazungu kimyaa, kwa kawaida Wazungu jinsi walivyo kama kweli wangeamua kulivalia njuga hili swala sasa hivi pangekuwa tayari hapatoshi, kungekuwa kila siku matamko ktk kwa Balozi zao, vyombo vya Habari vyote nje na ndani vingekuwa vinajadili nini kifanyike kwanza hata wangewaonya raia yao kuhusu hali ya usalama nchini mwetu n.k lkn wamekaa kimyaa!...
Kumbe kimya kimya mnaogopa wazungu? Mbona wkati mwingine mnasema hatutegemei misaada?
 
Mazungu wajanja, wamepima kina cha maji. Wameshtuka wakaona wasianzishe front nyingine ya magaidi pale Zanzibar. Akili mu kichwa.
 
UKAWA hawasomeki wanaenda wapi
4058b08952115911b716180d3546e8ac.jpg
 
Ukawa walifikiri Wazungu wangekinukisha dhidi ya nchi yetu, walikuwa na mategemeo makuubwa sana kumbe masikini ya Mungu Wazungu walikuwa wanawaridhisha tu, hamna cha vikwazo dhidi ya nchi yetu wala nini!

Raisi Sheni ameshaapishwa na tayari ameshaunda Serikali yake, Wazungu kimyaa, kwa kawaida Wazungu jinsi walivyo kama kweli wangeamua kulivalia njuga hili swala sasa hivi pangekuwa tayari hapatoshi, kungekuwa kila siku matamko ktk kwa Balozi zao, vyombo vya Habari vyote nje na ndani vingekuwa vinajadili nini kifanyike kwanza hata wangewaonya raia yao kuhusu hali ya usalama nchini mwetu n.k lkn wamekaa kimyaa!

Lakini waapi, kwanza ndiyo kila siku tunawaona Mabalozi zao wakikutana na Viongozi wa Serikali yetu kujadili mambo ya Kiuchumi, hili ni pigo lingine kwa ukawa, wamebakia kuwa wakiwa, Poleni sana!
wanaombea litokee utafikiri wao wajapani hawatoguswa ukawa bana
 
so mnataka wapige kelele kwani wao ni waswahili wa pemba?! hayo ya kelele yanawezekana kwa walafi wa madaraka ndio wanaochezesha mashavu tu kutetea uozo. Hao wazungu wanafanya yao kwa manufaa yao .
 
Ilikuwa ndio hoja inayo watoa Kimasomaso
Hawana hoja mbadala
Hawa kiukweli sioni hata umuhimu wa kutoa Ruzuku kwa watu wasio jiongeza
ACT hamuhitaji ruzuku kwakuwa mzee wa migebuka alikua anachota pesa za kuendesha chama kutoka NSSF kupitia Dr. Dau ambaye soon anaburuzwa mahakamani.
 
Sisi wanaukawa tumeamua kurudi majimboni sababu hali ni mbaya, tena mbaya sana. Ukizingatia wananchi hawatuelewi wamekomaa na hapa kazi tuu, ila tumegundua kosa letu nikumleta lowasa, dah!! maskini sisi
 
Hii asilimia 90 ya wajinga wa nchi hii tunaiondoaje katika nchi maana ni wengi! Kwa sababu kama baba mjinga ina maana mkewe mjinga na watoto watakuwa wajinga,wajukuu,........na kuendelea. Maskini tz
 
ACT hamuhitaji ruzuku kwakuwa mzee wa migebuka alikua anachota pesa za kuendesha chama kutoka NSSF kupitia Dr. Dau ambaye soon anaburuzwa mahakamani.
people demand freedom of speech as a compensation for the freedom of thought which they seldom use.
 
Sisi wanaukawa tumeamua kurudi majimboni sababu hali ni mbaya, tena mbaya sana. Ukizingatia wananchi hawatuelewi wamekomaa na hapa kazi tuu, ila tumegundua kosa letu nikumleta lowasa, dah!! maskini sisi
semea nafsi yako, "maskini wewe" sie unamjumlisha nani kwenye maoni yako?
 
Back
Top Bottom