Point inayoipatia ushindi CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Point inayoipatia ushindi CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Dec 24, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Napenda kuwakilisha hoja ambayo huenda ikatupelekea kwenye point au kwenye mchakato ambao ,huipatia ushindi CCM.

  Tuangalie Chaguzi zote za mfumo wa vyama vingi ,tupime matatizo yake namna gani,hila zipi CCM walizitumia na kubuka kwa kutangazwa kuwa ni washindi.

  Naona tuipime Zanzibar kwa ujumla ni njia zipi CCM walitangazwa washindi ,tukimaliza tuone ,Je ? njia hizo zinaweza au zimeweza kutumika upande wa Tanzania bara ? Ninavyoona ni kuwa hila na njama zote zitumikazo Zanzibar zime au zitatumika na huku kwetu Tanganyika.

  Kama tujuavyo uchaguzi wa safari hii matokeo yamebadilishwa ,mbinu hii ilitumika kumpa ushindi Salmini Amour na pia Karume wa Zanzibar ,sasa kama tunajipanga kwa uchaguzi wa 2015 ,okay tutazame kilichotokea Zanzibar hii 2010 ,Shein hakushinda ila ametangazwa na tume ,ajabu Mwinyi na Mkapa walitua Zanzibar usiku hadi hoteli ya Bwawani na huko kilichotokea wanakijua waliokuwa ndani.Inasemwa matokeo yalimpa ushindi Seif kwa asilimia kubwa ,Mapinduzi yalifanyika tuseme mapinduzi baridi.Hakuna vita wala mtu kukwaruzwa na tulitangaziwa na wengine kusherehekea.

  2015 haipo mbali ikiwa tutakuwepo na tuhai na wenye afya uchaguzi upo kama Katiba inavyosema,sasa lengo ni kuona njia hizi zinazotumika na kutumiliwa na CCM zinadhibitiwa kuanzia wizi wa kura ,mabadilisho ya matokeo na utekaji nyara wa tume ya uchaguzi,maana Zanzibar wanasema tume ilitekwa nyara na majeshi ambao wananchi waliyalalamikia kuwepo kwake kabla ya uchaguzi yaliwekwa standby kutuliza ghasia zozote zile ikiwa wengine hawatakubali matokeo,hapa alisikika mkuu wa majeshi akionya kumbe lengo lilikuwa limeelekezwa Zanzibar ambako majeshi walitayarishwa kabla ya miezi sita na kuhamia huko eti kwa lengo la kufanya mazoezi.

  Sasa huku kwenye jungu kubwa ambako CCM wanamiliki hazina ya Taifa hili ,haionekani ya kwamba wataweza nako kufanya utekaji wa tume na kutumia ileile mbinu iliyotumika Zanzibar ,hawa akina Mwinyi na Mkapa (Muislamu na Mkiristo) wanamiliki kitu gani katika mwenendo mzima wa Taifa hili hata ikawa wana nguvu ya kuyapinda matokeo ,nguvu hizo wanaweza kabisa kuzitumia huku Tanganyika au Tanzania bara.

  Nawakilisha hoja ni namna gani mbinu hizi zinaweza kudhibitiwa 2015 ,kwani kila tukienda mbele ndio mambo huwa makali zaidi na watu hujitayarisha kwa mbinu chafu zaidi. Zanzibar naweza kusema wameshatulia kwani lengo lililotegemewa la CUF kuyakataa matokeo ili CCM wabaki peke yao halikutokea.
   
Loading...