Pneumonia kiswahili chake

Pneumonia ni neno la kilatini likimaanisha mapafu. Wataalamu wa Engineering hutumia neno Peumatic wakimaanisha hewa.(Peumatic pressure)
Kiswahili sahihi ni Homa ya mapafu kwasababu peumonia hujitokeza kwa dalili ya homa. Kutokana na mapafu kuathirika kwa ugonjwa huu, mtu hujisikia kichomi, kwahiyo Kichomi pia ni neno sahihi. Kuna maneno ya mtaani yenye maana hiyo hiyo ''Limonia n.k'' kutokana na matamshi na ufahamu wa mtu. Peumonia hutamkwa (Nyumonia) ukikazia Nyu.
Asthma sio Peumonia. Asthma ni Pumu kwa kiswahili, na hii hutokana na kubana kwa mapafu. Tofauti na Penumonia ambayo huwa ni inatokana na infection ya wadudu, Asthma ni kubana kwa mapafu kunakotoka na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kurithi. Asthma haina homa mpaka pale tu mapafu yatakpokuwa yameathirika na infection. La muhimu kujua hapa ni kuwa mgonjwa wa Asthma akipata Pneumonia mambo huwa magumu kidogo kwasababu anakuwa na 2 in 1.
Peumonia hutibiwa na dawa kama Antibiotics wakati Asthma huwa na dawa za kufungua mapafu.
 
kwa ufahamu wangu ni ugonjwa wa kupooza mwili au kifupi UNYAFUZI

hapana mkuu pneumonia ni kichomi hayo ni mengne kabisa. Kupooza ni POLIO, unyafuzi ni MARASMUS mtoto hukonda sana anakuwa na uzito mdogo kwa urefu wake, anakuwa na high apepite, kitumbo kikubwa cha chini chini, ****** yanatepeta, ngozi kuvutika nk.
 
Hapo uko nje saaana. Pneumonia ni kichomi/nimonia. Ugonjwa wa kupooza ule utokanao na vijidudu (si ule unaotokana na kiharusi au stroke) nafikiri ni polio. Unyafuzi nafikiri ni kiswahili cha kwashiorkor-matatizo ya utapiamlo unaotokana na kupungukiwa kwa protini mwilini.
unyafuzi ni MARASMUS Upungufu wa nishati mwilini, mwili unashindwa kufanya metabolic activities including digestion stysteme ambayo ndio source ya virutubish vyote na protein ikiwemo.
Kupooza ni POLIO .
 
kwa ufahamu wangu ni ugonjwa wa kupooza mwili au kifupi UNYAFUZI

hapana mkuu pneumonia ni kichomi hayo ni mengne kabisa. Kupooza ni POLIO, unyafuzi ni MARASMUS mtoto hukonda sana anakuwa na uzito mdogo kwa urefu wake, anakuwa na high apepite, kitumbo kikubwa cha chini chini, ****** yanatepeta, ngozi kuvutika nk.
 
kwa ufahamu wangu ni ugonjwa wa kupooza mwili au kifupi UNYAFUZI

UNYAFUZI mwanangu ni Marasmus. Mimi nakubaliana na yule jamaa aliyesema Homa ya Mapafu ingawa hili tunalitumia sana kwenye kuelezea "Pneumonia" ya mifugo (Ng'ombe, mbuzi n.k). Kwa binadamu hawapendi sana kutumia hayo maneno, isipokuwa wanatohoa kama lilivyo"Niumonia"
 
Acheni kubahatisha majibu, mnamchanganya mwanajamii mwenzetu. Kwa ufupi ukitohoa ni Nimonia, kiswahili safi ni vichomi au homa ya mapafu, unaweza kutumia neno lolote kati ya hayo utaeleweka tu ndugu yangu.
 
Pneumonia[naimonia/nimonia] kiswahili ni-HOMA YA VICHOMI. Na HOMA YA MAPAFU NI "TB".
 
Katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu iliyotolewa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (Toleo la pili uk. 158), imeeleza maana ya neno "Kichomi" kuwa ni "nimonia" au "mkamba". Ndio kusema unaweza kutumia neno "nimonia" ambalo limetoholewa au "kichomi" au "mkamba".

:decision:UKO SAHIHI KABISA
 
Back
Top Bottom