PM: Serikali kutoa vibali 16,000 vya ajira kwa walimu mwaka 2019/2020

View attachment 1263174

Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutoa vibali vya ajira kwenye sekta za afya, elimu na kilimo na hivi sasa inatarajia kutoa vibali 16, 000 vya ajira za walimu na kisha itatoa vya watumishi wa afya.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo tarehe 14/11/2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi, ambaye alihoji, nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wanapatikana watumishi wa kutosha kuwahudumia Watanzania.

Amesema mkakati wa kujenga miundombinu ya kutolea huduma mbalimbali nchini unakwenda sambamba na kuajiri wataalamu watakao wahudumia wananchi katika maeneo husika.

”Serikali imeanza kutoa vibali vya ajira katika sekta hizi mbili za afya na elimu, hata kwenye kilimo. Mwaka jana tuliajiri watumishi 6,000 na sasa tuna kibari ambacho kitatoka hivi karibuni cha watumishi 16,000 kwa upande wa sekondari na msingi.”
Mwaka wa fedha 2019/2020 umaishia,hakuna ajira mpya.
 
watatumia corona kama kisingizio cha kuchelewesha ajira. Dawa ni kumnyima kura anayewanyima ajira
 
Back
Top Bottom