PLEASE READ: Nampenda lakini ana itikadi za KILOKOLE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PLEASE READ: Nampenda lakini ana itikadi za KILOKOLE

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tugutuke, Aug 3, 2012.

 1. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Za siku nyingi wana Jf.
  Ebwanae, mimi nimepanga kama mjuavyo kupanga kuna mambo mengi. Sasa katika nyumba yetu hii kuna dada mmoja inasemekana ni mlokole[maana sijawahi kumwona anatembelewa na walokole ] na anakaa chumba cha 3 kutoka room yangu. Kiukweli ni mzuri sana,na ninampenda ila sijui au nashindwa namna ya kumwingia na kumpa somo langu hilo. Kwa sababu hz.
  1. Nilimkuta ameshapanga siku nyingi,make mimi huu mwezi wa 5 tu tangu niamie hapo.
  2. Nimewahi kuingia na mashost wawili tofaut ndani kwangu,na yeye bahati mbaya aliwaona.
  3. Anapenda sana muda wote kupiga nyimbo za injili tupu,na hata yeye huwez kumsikia anaimba bongofleva.
  4. Ni mpole,kiasi kwamba nashindwa nianzie wapi kumtongoza.
  5. Nina namba yake ya simu ila yeye hajui kama ninayo[nilipewa na mshkaji mwingine ambaye naye nilimkuta humo geto kama house tenant mwenzangu]
  6. Naambiwa hawajawahi kumwona ametoka na mtu wala kusikia anamegwa na mtu.
  7. Ananiita sana sana kaka,nami nkajikuta namwita dada. Halafu Jana tu,nimemkopesha buku 5 lakini mpaka sasa hajanirudishia[sijui nianzie hapo kwa kujifanya namdai].
  Je,nifanyeje au nimwingieje mpaka ajue nampenda na aweze kabisa kuridhia? Maana kapanga anaishi peke yake,na mimi naish peke yangu. Tena ninataka nikimpata nitulie kwani itanifanya nipunguze u-playboy,kwani sitaruhusu mtoto wa kike anitembelee geto!. Naomba ushauri bandugu.
   
 2. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Kupata au kukosa ni matokeo, jaribu bahati yako kama unavyofanyaga kwa hao totoz wengine! Si umesema wewe ni playboy? unaishiwaje mbinu tena??kila la kheri kwa binti mlokole!
   
 3. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,679
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Huna Haya Wewe, utaupunguzaje u play boy? Ukishamwaribia utaanza oh hajui kitu yupo Kama gogo etc, mwache mtoto Wa watu utapata malaana bure.

   
 4. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Aaaaa jamani!
  Hakuna kisichoachwa!
  Nadhani nikimpata tu ntatulia na kuacha kutanga tanga,maana utakuwa ni upako mpya.
   
 5. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Baada ya kuingia Uislamu sasa unaanza kufakamia mabinti wa Kilokole...ushindwe na ulegee!
  Labda uwe ni Jeryson mwingine
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Hahahahahahaha
  Chakufanya leo mwambie mpendwa ntakuja kukutembelea kwako najua hawezi kukataa kutembelewa na ukienda kwake wewe ni kupiga story za dini na jua yeye ata tawala jukwaa na wewe utakuwa unachangia kidogo na ikiwezekana una mwambia aweke wimbo fulani, unaupenda sana alaf unachagua wimbo anao upenda kuupiga sana.

  Na hapo itakuwa ni mwanzo wa wewe kumzoea na huanze kumuita mpendwa sio dada tena, na ikiwezekana unaanza kusali kanisa analo sali na hiyo itakuwa njia ya kumnasa na inabidi uonekane kubadilika kidogo na wewe unatakiwa kuanza kupiga nyimbo za dini ili aone mna endana na usialakishe kumtongoza, vuta subira utaona muda muafaka na naamini hato kataa.
   
 7. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Cha msingi kama unamaana anavigezo na unamhitaji siyo kumchezea then usepe basi nenda naye taratibu, usijaribu kumtongoza. Jaribu kwanza kumfahamu yeye ni nani, life story (profile) yake ikoje mfano anafanya kazi, amesoma wapi wazazi wake wako wapi nk.
  Ukishamfahamu hivyo, basi jaribu kuwa na subira, mkaribishe kwa dinner mkaribishe (ningeshauri mtoke out) wakati huo huo zile tamaa zako usizionyeshe. Piga tu stori za kawaida usitake kujionyesha unajiweza au unajua sana kuongea, wewe piga tu stori za kutaka kumjua anapendelea nini. Unaweza kufanya hivyo mara mbili kabla ya kumuulizia inshu zake zinazohusiana na mahusiano.
  Nakushauri usizimwage vile vitotoz vyako ili uchukue muda zaidi wa kumfahamu huyo binti kabla ya kufanya maamuzi sahihi kwani itakubidi ikuchukue muda na ujizuie zuie (may be 2 months hivi mtakuwa wote mmekolea mkijashakuja kukubaliana kuachana itakuwa inshu)
   
 8. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Hivi kwanini hamuwachukui hao mnaoplay nao, na kutafuta wakiojitunza? Waliojitunza nao wanahitaji vijana waliojitunza si vicheche kama wewe!
   
 9. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hilo li avatar lako limenikera hata sijasoma ulichoandika.
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wewe walokole ndo warahisi kuwapata hao we ongea mpe somo uone ka hajahamia kwako
   
 11. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kasinge waitu!
   
 12. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nafikiri si jambo la busara kuwaangusha watu waliosimama kwenye imani zao kwa makusudi, hiyo ni dhambi mbaya! Mshauri kama kweli ana nia ya kuwa naye kama mke wake wa baadaye na kuachana na tabia za ukicheche then naweza kumshauri aendelee kumfuatilia lakini vinginevyo, mhhh siungi mkono hoja!
   
 13. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  saafi sana!
  Yeye ni muha,mwenyeji wa kigoma!
  Kazi yake ni mwalimu wa shule za watoto[nursery school teacher].
  Ana kati ya miaka 19-22. Wazazi wake wote wanaishi huko huko Kigoma. Labda ni mara chache anatembelewa na kaka yake,ambaye pia ni mlokole. Tena kaka yake akijaga basi ndio mapambio ndani huzid,wakija kulala wanaimba sana na kuomba sana! Ila kaka'ke anaporudi kwao,kidogo ile hali ya mapambio kwa mdada hupungua,na kuonekana mchangamfu tofauti na anavyokuwa na kaka'ke.
  Lakn ndugu,atakubali kutoka out? Make ndo hvo,full ulokole!
   
 14. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mfuate na umueleze tatizo lako, huenda naye anakupenda ila anashindwa akuingie vp, ila angalia usianzie hapo kwenye kibuku tano utachekesha, hebu nisaidie namba zake ndugu yangu nahitaji mtu wa kuingia naye katika maombi
   
 15. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  duh! Kweli wewe ni mtotowamjini.
  Kuna mtu aliwahi kuniambia vile,kuwa mlokole ni rahis kumpata kuliko mtu wa kawaida! Lakn kwa mtazamo wangu naona kama ni ngumu,hawa watu wanahitaji mbinu kali sana!
   
 16. D

  DOOKY JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Acha kutumiwa na shetani ili uharibu mipango ya watu wewe.... ushindwe kabisa....
   
 17. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  sio ntanyang'anywa tonge mdomoni?! Wewe nipe ya kwako halafu nimwambie kuna mtu anahitaji kufanya maombi na wewe,akikubali najua atakuvutia waya tu.
   
 18. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  hakuna aliyezaliwa tu na kuibukia ulokole hasa hapa kibongo bongo!
  Wengi wanaingia kuokoka baada ya ushetani mwingi.
  So ucshangae nikimpata basi nami shetan atakomea hapo hapo!
   
 19. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  A book is not judged by its cover..! stukaaaaa
   
 20. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Kama umefatilia maelezo yake vizuri kaweka wazi nia yake! Na kasema akimpata ataacha u play boy!Nakumpata ndio itakuwa njia pekee ya jamaa kubadili tabia Nilicho fanya nikutoa ushauri.
   
Loading...