Kuna kijana mmoja ambaye alifanyiwa kitendo kama hiki na mama yake miaka takriban 18 iliyopita,kwa bahati akaokotwa na wasamaria wema na kupelekwa katika kituo cha kulelea watoto yatima,aliishi pale muda mfupi akaja kupata wazazi wakufikia ambao walikuwa na na matatizo ya uzazi.Baba alikuwa raia wa ujerumani na mama raia wa Tanzania,bahati mbaya zaidi yule baba alifariki kijana akiwa bado mdogo,kilichofuatia ilikuwa wanasheria kumtafuta huyo mtoto,maana ukiacha majumba aliyoachiwa mtoto kulikuwa na makampuni yanayomiliki meli yote yakiwa kwa jina la mtoto huyo ambayo yako Ujerumani.Kwa hiyo hawa dada zetu wanaofanya vitendo kama hivi wakumbuke kuwa kuna mungu ambaye anawaangalia waja wake na kuwalipisha watendao maovu