Pitia nwa hii kama unaweza kunishauri

mkokotoaji

Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
54
Reaction score
10
Kifupi naomba nikushirikishe jambo hili nilikuwa kwenye mahusiano na binti mmoja kipindi hicho nipo chuo mwaka wa kwanza mpaka mwaka huu almost four years. NilijitahidI kumtimizia kila nilichoweza kimahitaji kama mpenzi Wangu. Nikamtambulisha kwetu na kwao kwa ahadi ya kuoana nae mwishoni mwaka huu.

But nilImkuta na vitu vya ajabu mno kwenye simu yake nikawa mpole but yalinishinda ikabidi tufikishane mpaka kwa mzazi wa binti mamaye mama akakiri mwanae hajatulia akaniomba msamaha kwa niaba ya binti yake mapema mwaka huu.

Kiukweli nilmkuta hana support ya wazazi nikamlea kwa kila kitu nikiamini atakuwa mke sahihi, but baada ya ugomvi ule niliamua kukaa pembeni kukaa kimya.

Tukaachana na binti but toka nimeachana nae amekuwa akizungumzia maneno machafu mengi kwa rafiki yake but kiukweli sikuwahi kuwajibu chochote hao rafki zake nliamua kukaa kimya but kila siku yanazungumzwa mapya na ni almost miezi sita imepita since tulivooachana.

So wanajamvi wenzangu nifanye lipi nimfate laivu nimpe makavu au niendlee na maisha mengne?
 
achana nae mkuu atakaa kimya mwenyew tu hata bila kuambiwa coz ataona kadharauliwa mpaka mwisho..
 
Kwani wewe unasoma nae shule moja ama umejenga karibu na kwao? Hayo maneno kwa marafiki zake unayapataje? Manake hao ni rafikize, kaa nao mbali kama unavyokaa mbali na yeye. Na anaetaka kukuhadithia muambie hauko interested. Manake ndio unajochochelea maneno hapo!
 
Wala asikuumize kichwa huyo, barking dogs seldom bite.

We endelea na timings zako, mwache roho ya usaliti imtafune.
 
Embu achana nae kabisa,wadada kama hao mimi nawaita wapuuzi,unajua nn bro wengi hawajui thamani ya ndoa au mke anatakiwa awaje,,,,we jifanye huoni husikii atakapo kaa kitaa akiona kila mwanaume anamfuata kimaslah anasepa ndio atakukumbuka believe me,wadada wengi ndio wapo hivyo yan hawataki kabisa kutulia hata wakioneshwa upendo wa kwel na kinacho wapa kiburi ni kutongozwa na wanaume wengi,,,,inaniuma coz muda si mrefu yalinikuta kama hayo so i knw how it pain,MPOTEZEE TU,MWISHONI ATAKUELEWA,akikua.
 

Barabara.
 

Ni kawaida katika saikolojia kuwa mgomvi wako asipokusikia ukimjibu anachokuzushia huwa anaumia mara mia zaidi. Kaa kimya kabisa kama kwamba humsikii. Nakuhakikishia kuwa aliko hapati raha na hata anaendelea kupoteza. Ipo siku atakuja kama mbwa koko kukupigia magoti, nani muda huo atakuwa akilia na kusaga meno lkn atakuwa amechelewa saaaana tu. Kaa kimya kabisa!
 
Achana nae, usipoteze muda nae, pia kumbuka anakuongea kwa mabaya coz anajutia sasa, so hasira anazipeleka kwa kukusema vibaya.
 

Achana nae,..yalisha nikuta kwa binti mmoja home walimfahamu ila kwao akawa hataki wanifahamu kumbe anaajenda za siri, ..nikamuacha kimya kimya,..leo anajuta.
 
Thnx wadau kwa ushauri wenu na busara sahihi hakika ntaafuta ushauri huu mzuri wenye tija.Tuendlee kumuomba Mungu juu ya Taifa hili
 
Wadau hapo juu WAMESHAMALIZA MKUU. Umefanya vyema kukaa kwako kimya. Ukimya ni dawa nzuri kushinda zote kulingana na mazingira yako.

Pole sana, chukulia kama ulitoa sadaka tu kumsaidia huyo, Utavuna kivingine kwa wakati wako.
 

aseme yoooote ila akizungumzia kama kwenye 6*6 huna lolote mkate makofi kabisa!!!
 
Achana nae, Fanya kama husikii kitu siku zote mfa maji haishi kutapatapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…