PITIA KWANZA HAPA...........ujifunze

PITIA KWANZA HAPA...........ujifunze

Iamabdul

Member
Joined
Sep 26, 2013
Posts
72
Reaction score
27
Mwanzoni mwa mwaka huu mpenzi ambaye nilimpenda kumuamini na kumthamini alinisaliti na kwenda kwa mtu mwingine ambaye ni mtoto wa pedeshee mmoja hapa mjini. Iliniuma sana mpaka ikapelekea kuchanganyikiwa na kusababisha nisimwamini msichana yeyote yule ktk uso wa dunia hii. Baada ya hapo nilijianzishia kajitabia cha kwenda kwa kina dada powa(malaya) kumalizia haja zangu hasa maeneo yale ya mwananyamala, mpaka nikaja kuzoeana na dada mmoja hivi ambaye anaitwa Irene ambaye ni mmoja wa wanaouza mwili maeneo hayo, huyu dada ndo aliyenifanya nipende kwenda karibu siku zote hii yote kwa uzuri aliokuwa nao. Irene alikuwa ni msichana ambaye yuko tofauti na wasichana wengine maeneo yale, hii yote ni kwa uzuri aliokuwa nao kwani alijaaliwa sura yenye mvuto iliyopambwa na tabasamu mwanana ambalo ndani yake kuna mwanya mzuuri uliochangia uzuri wa sura yake. Mbali nakuwa na sura yenye mvuto pia Irene alikuwa na umbo zuri lililojaa hasa maeneo yaleee ya nyuma a.k.a uani, pia uzuri wake ulichangiwa na weupe aliokuwa nao, kwa kumuangalia tu Irene hakustahili kufanya ile kazi kwani ni mdada ambaye angeliweza kuolewa na mtu mwenye fedha zake, vitu hivi viliinifanya nizoeane na huyu mdada mpaka siku nyingine huwa nasahau kutumia kinga. Kwenye mwezi wa tano nilipata safarii ya kikazi jijini Arusha ya karibu miezi miwili, safari hii ilinisababisha nimisi kweli mambo ya Irene, kwani mbali na uzuri wake pia huyu mdada alikuwa anajua mambo yetu yalee ya kunako sita kwa sita na kufanya hata mshahara wako au mauzo yako ya wiki nzima ukamkabidhi yeye kutokana na mambo yake. Baada ya miezi miwili nilirudi Dar na siku hiyohiyo nilifika ofisini kwa Irene kupata ile kitu roho inapenda, nilivyofika maeneo yale sikumkuta Irene nilivyomuulizia nilipata majibu ambayo yalinifanya nidondoke kwa mshtuko kwani Irene alishafariki tangu wiki kadhaa zilizopita kwa ugonjwa wa ukimwi, siku hiyo ndo siku ambayo niliyogundua paa la chumbani kwangu limetobotoboka hii yote ni kwa kukosa usingizi kwa mawazo. Asubuhi yake nilikwenda kituo cha afya kwenda kupima kama nami nimo ktk listi ya IZRAEL. Majibu nilyoyapata ya kanifanya nizimie siku tatu kwani nami nilikuwa nimeathirika na ugonjwa hatari wa Ukimwi. Yaliiyofata ni majuto kwani maamuzi niliyoyachukua baada ya mpenzi wangu kunisaliti yamenifanya kupata gonjwa ambalo sikulitarajia kulipata ktk maisha yangu. NB: simulizi hii ni ya kutunga na haiusiani na mimi hata kidogo bali nimeiandika kwa lengo la kutufumbua macho na kukumbushana juu ya swala zima la Ukimwi na kuwa waaminifu ktk ndoa au mahusiano yetu.
 
^^
Excellent !!! Nafurahi sana kupata mtu mwingine anaepiga vita UKIMWI nadhani Mentor amepata mfuasi ukikumbuka Tanga sirudi tena
^^
 
Last edited by a moderator:
Aaagh! Afu ukimwi bhana! Sehemu zote za kukaa haujapaona ila kwenye mbunye!!!!!
Hii si bure!
Na Ukimwi ni Adhabu sio maradhi!
Kwanini usipatikane katika miti, majabali or baharini??????
 
iamabdul kweli kama alivyosema ndugu hapo juu Tanga hawatarudi tena mi ni m2nzi wa mashairi bt kwa hilo fanya mpango 2tunge riwaya big up sana!
 
Mwanzoni mwa mwaka huu mpenzi ambaye nilimpenda kumuamini na kumthamini alinisaliti na kwenda kwa mtu mwingine ambaye ni mtoto wa pedeshee mmoja hapa mjini. Iliniuma sana mpaka ikapelekea kuchanganyikiwa na kusababisha nisimwamini msichana yeyote yule ktk uso wa dunia hii. Baada ya hapo nilijianzishia kajitabia cha kwenda kwa kina dada powa(malaya) kumalizia haja zangu hasa maeneo yale ya mwananyamala, mpaka nikaja kuzoeana na dada mmoja hivi ambaye anaitwa Irene ambaye ni mmoja wa wanaouza mwili maeneo hayo, huyu dada ndo aliyenifanya nipende kwenda karibu siku zote hii yote kwa uzuri aliokuwa nao. Irene alikuwa ni msichana ambaye yuko tofauti na wasichana wengine maeneo yale, hii yote ni kwa uzuri aliokuwa nao kwani alijaaliwa sura yenye mvuto iliyopambwa na tabasamu mwanana ambalo ndani yake kuna mwanya mzuuri uliochangia uzuri wa sura yake. Mbali nakuwa na sura yenye mvuto pia Irene alikuwa na umbo zuri lililojaa hasa maeneo yaleee ya nyuma a.k.a uani, pia uzuri wake ulichangiwa na weupe aliokuwa nao, kwa kumuangalia tu Irene hakustahili kufanya ile kazi kwani ni mdada ambaye angeliweza kuolewa na mtu mwenye fedha zake, vitu hivi viliinifanya nizoeane na huyu mdada mpaka siku nyingine huwa nasahau kutumia kinga. Kwenye mwezi wa tano nilipata safarii ya kikazi jijini Arusha ya karibu miezi miwili, safari hii ilinisababisha nimisi kweli mambo ya Irene, kwani mbali na uzuri wake pia huyu mdada alikuwa anajua mambo yetu yalee ya kunako sita kwa sita na kufanya hata mshahara wako au mauzo yako ya wiki nzima ukamkabidhi yeye kutokana na mambo yake. Baada ya miezi miwili nilirudi Dar na siku hiyohiyo nilifika ofisini kwa Irene kupata ile kitu roho inapenda, nilivyofika maeneo yale sikumkuta Irene nilivyomuulizia nilipata majibu ambayo yalinifanya nidondoke kwa mshtuko kwani Irene alishafariki tangu wiki kadhaa zilizopita kwa ugonjwa wa ukimwi, siku hiyo ndo siku ambayo niliyogundua paa la chumbani kwangu limetobotoboka hii yote ni kwa kukosa usingizi kwa mawazo. Asubuhi yake nilikwenda kituo cha afya kwenda kupima kama nami nimo ktk listi ya IZRAEL. Majibu nilyoyapata ya kanifanya nizimie siku tatu kwani nami nilikuwa nimeathirika na ugonjwa hatari wa Ukimwi. Yaliiyofata ni majuto kwani maamuzi niliyoyachukua baada ya mpenzi wangu kunisaliti yamenifanya kupata gonjwa ambalo sikulitarajia kulipata ktk maisha yangu. NB: simulizi hii ni ya kutunga na haiusiani na mimi hata kidogo bali nimeiandika kwa lengo la kutufumbua macho na kukumbushana juu ya swala zima la Ukimwi na kuwa waaminifu ktk ndoa au mahusiano yetu.

pokea hii zawadi,nafikiri itakufaa
duh.jpg
 
Kha! Ulivoiandika sasa kama mwathirika kweli...hebu kapime kikwelikweli mkuu!

Kidogo unteke hadi mimi...
 
  • Thanks
Reactions: GKM
uliniteka nikadhani kweli!!! but asante kwa kutukumbusha!!!!!
 
Kha! Ulivoiandika sasa kama mwathirika kweli...hebu kapime kikwelikweli mkuu!

Kidogo unteke hadi mimi...

Mbona inaonekana kabisa ni hadithi ya kutunga hata kabla ya NB...

My first doubt ilianza hapo kwenye miezi miwili with connection na suala la kufariki...that's a very short time.
 
  • Thanks
Reactions: GKM
pokea hii zawadi,nafikiri itakufaa
View attachment 115876
Yaani unampa mwenzio zawadi ya pupu wakati yeye ametoa elimu kwa sisi tunaofakamia kwa kuangalia umbo la mtu??? Tujifunze kuwa ARV ni silent killer. Mtu unamuona mnene ndani ya koti na VX kumbe kesho ni marehemu!!! Utasikia tu alipata pneumonia kawekewa Oxygen na siku mbili akatoweka duniani. Utakuta mama au binti ana wowowo ya kufa mtu ila ukiuliza kwa pembeni utasikia Bwana wake au mume wake alikufa miaka 2000 kwa ngoma!!!! Aise kipimo cha VCT au hospital ndiyo salama yako na yangu tu hakuna kipimo cha macho.
 
Mbona inaonekana kabisa ni hadithi ya kutunga hata kabla ya NB...

My first doubt ilianza hapo kwenye miezi miwili with connection na suala la kufariki...that's a very short time.

Mkuu watu8 kama mtu anatumia ARV ana anakula vizuri nakuhakikishia afya inakuwa safi sana ila siku akikamatwa kidogo na kahoma hasa pneumonia hata wiki wengine hawachukui. Ngoja wenye experience na ndugu au marafiki waliokuwa wanatumia ARV na kuzingatia mlo uone watakupa ushuhuda kamili hapa mkuu. ARV ni noma, mtu kitambi na wowowo hata mtu akikuambia kuna kirusi pale unakataa.
 
kabla ya kuimaliza stor; kwanza nilijua utamuachisha Irene na biashara ile.
Pili nikajiuliza moyoni, hivi hadi leo Irene yupo pale?
Mh! Kumbe kafariki na story yenyewe ni ya kutunga.
Yani sura ya Irene ilinijia na kumuona ni kama Keneth (shombe shombe) wa Mentor aliyekuwa na Tanga
 
Duu nilikuonea huruma kabla ya kujua kumbe ni story ya kutunga...but big up mkuu umeniweza.
 
Mkuu watu8 kama mtu anatumia ARV ana anakula vizuri nakuhakikishia afya inakuwa safi sana ila siku akikamatwa kidogo na kahoma hasa pneumonia hata wiki wengine hawachukui. Ngoja wenye experience na ndugu au marafiki waliokuwa wanatumia ARV na kuzingatia mlo uone watakupa ushuhuda kamili hapa mkuu. ARV ni noma, mtu kitambi na wowowo hata mtu akikuambia kuna kirusi pale unakataa.

mm mke wa anko yangu alikuwa anatumia ARVs kwa muda mrefu na familia ndo tulikuwa tunajua kwa sababu anko naye alikufa kwa ukimwi,mke wa anko alianza kuumwa kichwa kwa muda wa wiki 1,akiwa anapasua kuni akaanguka alipopelekwa hsp akafia mapokezi,Arv ndo zinadanganya sana watu tunaingia mkenge
 
Back
Top Bottom