Pitia elimu fupi: Subaru forester 4th generation (eyesight)

Pitia elimu fupi: Subaru forester 4th generation (eyesight)

FB_IMG_17293354413678324.jpg
 
Hii oil original ya subaru forester xt ikoje?
Mimi natumia Castrol oil edge ful SYNTHETIC 5W-30..mara ya Kwanza nilikuwa nimetumia Atlantic 5W-30 fully synthetic lkn bado haiwezi kuifikia Castrol Kwa ubora hata Ile smoothness ya engine imekuwa tofauti.. kumbuka boxer engine XT zinafua joto jingi Sana kwasababu ya turbo ndiyo maana wenyewe manufacturer wamependekeza Castrol oil

Tafuta hii na bei yake ni 180,000 Kwa dumu lita 5
IMG_20250118_100915.jpg
 
HII NDIYO FORESTER NEW MODEL (4th GENERATION)🔥🔥

FORESTER ni gari ambayo imepata umaarufu wake kutokana na Ufanisi wa Utendaji wake ambao ni thabiti hata katika barabara zenye changamoto.

Katika Toleo la NNE (SJ) Kuna maboresho ambayo yamefanyika.

Hapa tunazungumzia matoleo ambayo uzalishwaji wake ni kuanzia 2012 - 2018

Utofauti wa toleo hili na matoleo ya nyuma upo kwenye Muonekano na ukubwa kiasi ambapo 4th Generation imeongezeka kiasi.

UIMARA
Moja kati ya maboresho ni uimara wake hata inapotokea ajali ambapo hapa yamejizolea alama nzuri sana (97%) kwenye Jaribio la Kugonganisha (Crash Test).

Pia ni gari ambayo inadumu na ni moja kati ya vitu ambavyo vimewavutia wengi kumiliki SUBARU FORESTER katika Matoleo Yote.

MATUMIZI YA MAFUTA
Injini na matumizi ya mafuta ni kama ifuatavyo:
🔰PETROL
🔰MANUAL na AUTOMATIC
🔰2,000 CC inakwenda 14 Km/L
🔰Turbo na ambazo sio za Turbo

Yenye TURBO hujulikana kama SJG ambayo haina TURBO hujulikana kama SJ5.

Unaweza kuchagua kati ya FORESTER yenye TURBO kwa ajili ya nguvu zaidi au ambayo haina TURBO kwa matumizi mazuri ya mafuta.

VIFAA NA MAFUNDI
Vifaa vyake vinapatikana kwa jitihada kiasi hasa kwa mikoani na kwa kwa bei ya juu kiasi. Fanya utafiti katika mazingira yako kama unaweza kupata vifaa vyake. La sivyo utalazimika kuagiza Dar es Salaam Mwarobaini wa Vifaa vya magari 🤭😊

Mafundi wa FORESTER pia wapo jiridhishe na uwezo wa Fundi wako kabla ya kumkabidhi kutengeneza gari yako kwani mafundi wengi wamezoea mifumo ya Gari za Toyota ambayo ni Tofauti na SUBARU FORESTER

MAUA YAKE
Wamiliki wa FORESTER za Wamiliki wa FORESTER hii wanavunia Muonekano wa kuvutia sana na nafasi ya kutosha kwa ndani iliyoongenzwa kulinganisha na matoleo ya nyuma.

Inakuja na Teknolojia ya Eyesight ambayo inaboresha ufanisi wa uendeshaji kwa:
🔰Kufunga Breki za dharura
(Pre-collision Braking system)
🔰Ishara ya kuonyesha unahama
kwenye upande wako wa
kuendeshea
(Lane departure warning
system)
🔰Mfumo wa uendeshaji
kuendana na gari iliyo mbele
(Adaptive Cruise Control
system)

X-MODE: Hii ni Nyongeza ambayo ipo kwenye FORESTER ambayo kazi yake ni kuongeza ufanisi zaidi katika kukabiliana mazingira ya barabara zenye Changamoto sana na kufanya safari zako kuwa za kusisimua.

TUZO: Canadian Utility Vehicle of the Year, New Zealand Car of the Year Award. FORESTER haikupa tuzo hizi kwa bahati mbaya ni kutokana na ufanisi wa utendaji, Usalama na muundo wa kisasa kabisa 👏👏👏

UTULIVU
Utulivu wake ni mzuri sana kwenye barabara za lami na za vumbi kutokana na uwiano mzuri wa umbo lake pamoja na muundo wa chasis.

CHANGAMOTO
Gari hii tofauti na nyingine haivumilii oil tofauti na iliyoshauriwa na mtengenezaji. Hakikisha unaipa oil yake usije kuua injini

BAJETI
Unaweza kuimiliki SUBARU FORESTER NEW MODEL 4th generation kwa bajeti ya kuanzia TSH 30M mpaka TSH 35M

HITIMISHO
Sifa zake ni nyingi nimalizie kwa kusema zipewe tu maua yake. Kama mfuko wako unaruhusu njoo tukuagizie🌺🌺🌸🤗

Elimu hii fupi imetolewa na YETU MOTORS ambao ni washauri na waagizaji magari wenye ofisi

Mbeya: Mwanjelwa Soko Jipya
Mwanza: PSSSF PLAZA
Dar: Golden Jubilee Towers

View attachment 3125529View attachment 3125530
Nipo Dar na Mzee wangu ana changamoto ya Gari lake Forester. Je Mnapatikanaje? Contact
 
Back
Top Bottom