Shalom wapendwa katika Bwana.
Mapishi ya keki ya chocolate yapo mengi leo nawawekea pishi hili.
Mahitaji
Unga wa ngao 250g
Kokoa vijiko vya mezani(tbsp) 3
Baking powder vijiko vya chai(tsp) 2
Siagi 250g
Sukari 250g
Mayai 4
Maziwa 10tbsp
Mapishi au Hatua za uandaaji
Pasua mayai na uyapige pige kwenye bakuli
Weka unga, kokoa, sukari na baking powder kwenye bakuli la kuchanganyia (mixing bowl) na changanya pamoja.
Ongeza sukari, siagi, mayai na maziwa na changanya hadi viwe vimechanganyika kabisa.(viwe kama uji mzito). Ni rahisi zaidi ukitumia mixing bowl ya umeme.
Miminia mchanganyiko kwenye tray la kuokea la ukubwa wa kati.
Washa oven joto la 160 degree za centigrade na oka kwa dakika 50.
Chomeka kijiti chembamba kwenye keki na kama kikitoka kikavu basi keki imeiva
Epua na weka icing kadiri unavyopendelea.
Inaweza kuliwa na chai, kahawa, juice, soda au hata maji.
Enjoy!
Kwa watakaofanikiwa kuipika tafadhali naomba feedback.
Mungu akubariki sana.