Piracy: Mchango, athari, faida na hasara zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Piracy: Mchango, athari, faida na hasara zake

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mtazamaji, Jan 8, 2011.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi napinga piracy hasa ya kazi za watanzania lakini pia napinga watu wanajifanya wako kifua mbele kupinga piracy inayoweza kuwa mkombozi wa taifa letu.

  Mfano. Shule na vyuo hazina vitabu kwa hiyo kusmahrui mwnafuzi kusoma au kupakua kitabu cha GPRS and Wireless Applicatins Personal Wirelss Communication , Bluetooth arctecture. Kutoka Afroit.com au Jamiiforums.com hata kama hawana copy right ya kufanya hivyo kwangu ni sahihi. Tembelea Communication--Wireless Technologies--GPRS and 3G Wireless Applications uone baadhiya vitabu walivyonavyo

  Wanafunzi wa chuo kulalamika hana vitabu wakati kwenye mtando kuna vitabu vya bure kwa kisingizio cha copy right ni uzushi.

  Mtotowa mkulima kushindwa kufanya course ya CCNA au MSCE sababu hana uwezo wa kulipa mafunzo wakati kuna Video za mafunzo tena za kiwango bora ni uzembe. Mfano kuna vide nzuri tu kama Train Signal Cisco CCNA Training Videos (download torrent) - TPB
  Au MICROSOFT VISUAL STUDIO 2010 TRAINING DVD [thethingy] (download torrent) - TPB

  As long as piracy haihusihi kazi za watanzania kwangu naona Ni fursa ya Kutumia Internet na IT kwa manufaa yetu bila woga. Nashauri na serikali iache kufuata fuata mkumbo tu.

  Je una maoni gani juu ya mchango,atahri, faida na hasara za piracy kwa maendeleo ya Tanzania.

  Nawasilisha kwa mjadala
   
 2. redSilverDog

  redSilverDog JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 486
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Honestly, wengi katika sisi wakati tunasoma tumenufaika na pirated software au elctronic books n.k. Software ni ghali, na kama kumuambia mzazi akununulia ni headache nyengine unaampa mzee. Hasa kwa watoto kama mimi niliekulia kwenye familia ya kimasikini.

  Hata hivyo, mimi naona kazi za watanzania ndo zinadeserve kuwa pirated! Watanzania wachache au hamna kabisa wanaofikiria watoto wa kimaskini. Hio ni kinyume na nje, ambao wanachapisha vitabu kwa ajili ya maskini, 'cheap edition', ambavyo ni kwa ajili ya India na nchi za chini ya Jangwa la Sahara.

  Kwa kifupi, piracy sio kitu kizuri, lakini ili kuzuia, lazima tueke bei ambazo ni 'reasonable'.
   
 3. rancosys

  rancosys Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe: Ati sababu vitabu ndio kisa mwanafunzi asifanye mtihan au kupata mafunzo fulan,,, Internet technlogy imetuwezesha watumiaji kupata Degree online, na Taaluma mbali mbali, Pia Mbali ya vyeti Tumeweza kupata mafunzo na taaluma muhim kupitia IT tech,, ambazo zimeongeza ufanisi na Kufaulu ,mitihan mashulen.
  NI UZEMBE WA WATANZANIA WENGi,, BADALA YA MTANZANIA ACHUKUE TIME YA KWENDA CAFE AKASOME AU ACHUKUE LAPTOP NA KUUNGANISHA MTANDAO NYUMBANI KWAKE KWA MANUFAA YA KITAALUMA KTK SHUGULI ZAKE... ANAONA ANAPOTEZATIME BORA AKAANAGLIE UPUUZI,, HAD ANASAHAU TEACHER KAMBA assignemnt gani ....
  VITABU VYOTE VIZURI VINAPATIKANA KWA INTERNET
   
 4. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtazamaji, Naona hapa unazidi kupotosha watu. Piracy is piracy, in any guise it will still be piracy.
  Ilaumu shule na uongozi wake kwa kutokuwepo na hivyo vitabu na resources zinginezo kwenye elimu.
  Kwa nini tu uheshimu copyright laws for products za Mtanzania? Nani kwakwambia kuwa aliyeandika hicho kitabu cha CCNA ni tajiri sana na kutopata returns yake biashara yake haitaharibika?
  Mtoto wa mkulima, anatafuta nini kwenye CCNA? Anataka apate elimu ambayo itamlipa pesa nyingi, mfano, 2Million Shillings per month. Kitabu hiki costs around $50. equivalent to 70,000TSH. Ukiniambia kuwa huyu aliyekitumia hiki kitabu akishapata kazi atamkumbuka mwandishi wa hicho kitabu pengine nitakuelewa, lakini kusema sisi masikini imepitwa na wakati. Nchi hii ina pesa bwana, ila tu hatujajua jinsi ya kujiendeleza.

  Tukisha jisaidia na vitabu vya wizi, je mahospitalini tutafanyaje?, tutaweza kuiba madawa, na resources zingine ilhali sisi maskini?

  The internet is strewn with free, I mean completely free resources za elimu, kwa hiyo madai ya kutokuwepo na alternative means mtanzania hatasoma ni kuwa unajidanganya na kuendeleza tabia ya wizi. Ndugu yangu, believe me, ukianza kudokoa'dokoa mali za watu at this level, you will not stop at stealing from a resourceful writer/developer. Utaanza kuwaibia ndugu zako, nchi yako, na hata kujiibia mwenyewe.

  Take pride in being honest in your dealings...
   
 5. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  JAMANI PIRACY ITABAKIA KUWA PIRACY. NA HATUWEI KUJITETEA ETI TUNAIABA KWA SABABU YA NJAA ZETU. NA KAMA SISI NDIIO JAMII INATUTEGEMEA KWA MAANA YA UTALAAM TULIO NAO BASI NI BUSARA ZAIDI TUKAWA WA KWANZA KUHESHIMU KAZI ZA WENGINE.

  KUTO KUHESHIMU KAZI ZA WENGINE NDIO CHANZO CHA KUBOROMOKA KWA VIWANGO VYA TAFITI. HAKUNA MTU ANAYE FANYA KITU KWA MASLAHI YA MWINGINE.

  NCHI ZA AFRICA NA ZA KIARABU NDIO ZINAZOONGOZA KWA PIRACY (SOMA HAPA) . HILI LIM4ECHANGIWA NA DHANA KAMA HIZI KWAMBAKWANINI NILIPE KIASI KIKUBWA KWA AJILI YA KITU AMBACHO NAWEZA KUKIPATA KIRAHISI??

  ASANTENI.
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  OK wajumbe Hu ni mjadala tu wajumbe.

  Piracy ni kosa lakini nii hipiracy imewafnya hata microsoft kuwa na free version kama SQL server express na Visuala Studio Express .Ni hii Piracy imewafanya microsoft kusupport proect fulani za open source code .Tembelea site ya codeplex.com kwa maelezo zaidi

  Nachosisitiza ni watanzania tusipigane vita tusiyojua ni kwa faida ya nani. Hata China na Russsia wana sheria za piracy lakini kwa manufaa ya nchi yao kuna mambo fulani fulani wanayafumbia macho. China na Russia ndio nchi zinazoongoza kuzalisha pirated version za Microsoft.

  Bado nasisitiza wanafunzi na watanzania kwa ujumla tuna oportunity ya kufaidika zaidi kwa pirated software and application

  Teh teh teh tuendelee kujadiliana faida na hasara.
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu naomba nikujibu inawezekana nawapotosha watu lakini dhumuni langu nikuleta mjadala. Je wewe Laptop yako ukiondoa gharama za za laptop umetimia shilingi ngapi kuinstalll software unazotumia. ?

  Naweza kuheshimu copyright law kwa product ya mtanzania sababu ya uzaledno. Umeona taarifa za wiki leaks kuhusu ATCL na Beoing. Yule balozi wa USA anawezekana kasemakweli lakini kaandika aneno yale kutetea masali ya nchi yake. Kwa sababu Beoing ni kampuni ya USA. TUsingejua habarihizi kama boeing singekuwa moja ya kampuni zinazouza ndege.

  We can pretend to play by the rule and be fair but for whose benefit . Je wao wana play by the rule na wako fair kwenye mambo amabyo sisi tuko kwenye advantage kama ya kilimo?.

  Tunaweza kujifunza mengi kutoka china. Kampuni isiyo kuwa na branch china haiwezi kupta msaada mkubwa kutoka serikalini wa piracy au counteefeit ya bidhaa zake.

  Bado nasisitiza kuna watu wamejtolea DVD za video walizopewa kwenye training kama za CCNA, MSCE, etc wameziweka online. Ingawa copy right law inawazuia bado naona anayehitaji asishindwe kudowloadvideo hizi.

  Hahhahaa umenichekesha eti nikianza kudokoadokoa...... Na mimi nina wasi wasi ukianza kutii tii tu kila sheriaeti kwa sababu ipo bila kujiuliza msingi wake na faida zake matokeo yake hufiki popote.

  Kwa nini iwe halali wewe kunuanua CD ya microsoft office laini iwe kosa ukitaka kushare software hiyo rafiki yako aitumie. Kwa nini hwakufanya copy right kamahii ya licence kwenye bidhaa kama Nguo tuondokane na mitumba.

  Sitashangaa site kama piratebay.org wakitaka wahamishie makao makuu yao Tanzania watakataliwa lakini huko kwa wanaojua sheria zenye manufaa kwa nchi zao sweeden ,Russia , etc vtu hivi vinajadilika. kuna movemnet za kussspot, piracy ,open source na sharing

  Huu ni mjadala tujadili faida na hasara.
   
 8. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umetao mfano mzuri wa opensource software ambazo zinafanya kazi kama hizo za kulipia. Vitabu na learning materials zake zipo za kumwagwa na katika kujifunza, ni vyema mwanafunzi atumie hizi na makampuni pia wanaweza ku'implement mission critical application solution kwa hizi hizi za opensource. Sasa tukiingia kwenye materials mtu/watu au makampuni wametengeneza ili kuendeleza biashara zao, kwa nini tusitoe heshima kwao kwa ujuzi wao na kuwawezesha kuendelea na developments ambazo zitatunufaisha baadae? Ukiwafirisi sasa hivi nani kweli ameumia? Kama kampuni unayofanya kazi wame implement AIX systems au CISCO based networking, na the company husika (CISCO na AIX) zikafirisika, hence support kuwa withdrawn, inamaanisha kuwa your employer naye itabidi atafute alternative. Inamaana sasa wewe utakimbilia kwenye net kutafuta vitabu vingine vya kuiba? Najua example yangu ni simplistic if looked at one-on-one basis lakini inaeleza implications of cashflow to these businesses.

  Tungesema hivi, watu wengi sasa wameshatoka kwa kutumia vitabu/software hizi na sasa wamebobea katika fani zao. Sasa hawa ndio wa kuikomboa nchi yetu kielimu kwa kuandaa vitabu kwa wanafunzi wetu, mali hii itakuwa officially free for the TZ student. Pia waandike software ambazo zitatumika kwenye makampuni etc etc. Before I go further naona ushaona kuwa hili haliwezi kufanyika. There are costs, massive costs involved in putting these out to market hence tuheshimu hiyo na kulipia hizi mali.

  Tusiseme kwa sababu China, Pakistan, Armenia sasa wameongoza kwa wizi na sis tuwe wezi. Sifa nzuri ni kama kusema Russia wameamua kuwa from 2013 Opensource software ndio zitakazotumika in government organisations ndio mambo ya kuiga sio kuwa na Russia wajanja mno kweny ku'pirate software na online scams.
   
 9. redSilverDog

  redSilverDog JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 486
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Swali moja, kwanini government isisubsidize? I will commit piracy if i have to, no question on that!
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nakimekulewa mkuu lakini tusiogope kuhoji matatizo yaliyopo

  • Mfano kwa ninii we kosa wewe kutuoa copy ya DVD ya mafunzo ya CCNA uliyolipia kihalali kwa rafiki zako wengine?
  • Kwanini tusiombe licence terms agreements zinazoendana na mazingira yetu
  • Kwa nini litumike neno piracy na sio sharing
  Tujiulize tundelee kujadili
   
 11. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo copy ya DVD kama imeambatanishwa kwenye kitabu na imekuwa copyrighted basi si mali ya ku-share. Kama utampa kitabu pia basi hapo sidhani unakiuka hiyo right kwani there's what they call "Fare Use Policy" ambayo inakuruhusu provided you giving away the complete set of material to second person. Remember the term given here used to mean no monetary exchange has taken place. Hata kwenye software, unayo fursa ya kuitumia on this fare use basis. Ukimpa mtu PC yako with all the softwaere installed hence licensed to the PC that's fine. Lakini making a second install of the software to another machine you personally not going to use is infringing on the law.

  Piracy and sharing ni vitu tofauti. You only share where you have implied rights to do so and you infringe on the rights hence becomes a piracy especially where financial hit is directly incurred by the owner of the right.

  On issue of terms that can benefit us. We only have to ask and I guess a pricing policy by the main operators can bring it down to a manageable level. Microsoft I hear have such but I can't say for sure what that means in terms of Tanzania.
  But remember, you can't just ask an organisation to spend their time to work out a policy if your region is reportedly happy to allow piracy to take place. Ndio serikali should support the fight on piracy without expemption, and only if that is happenning can we ever have such ideas workable.

  SilverDog:- Subsidize (don't make me laugh!!!) Our ministers first look is pesa za LandCruiser na posho when they have their talking shops.... Hilo la kuwa na mkakati wa kutenga kiasi cha pesa for volume purchase of copyrighted materials hatuna, na ukiwapa hii idea, cha kwanza ni kuangalia %'ge watakazoongeza kwenye hiyo proforma resulting in the costs being unreasonably expensive.
   
 12. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kama sijasahau,kuna usemi kwenye mambo ya management ambao unasema kuwa binadamu huwa anapitia hatua kadhaa kaatika maisha yake,pia katika kila kipindi huwa anaweka mnyumbulisho wa nini cha muhimu na nini ni anasa.Kwa mfano miaka ya zamani ilikuwa ngumu kuona matalii wa kichina,ila siku zinavyokwenda mbele wanazidi kuongezeka.

  Sasa,nini nilitaka kumaanisha,nchi zote katika maendeleo yake,lazima wapitie hatua fulani ambazo either matatizo na wizi hutawala,au baadhi ya watu kuumia ili wengine wafaidi.yaani kwao ni kuhakikisha wanafikia malengo kikamilifu.Si umekuwa ukisikia jinsi US inavyopigia kelele haki za binadamu kwa Uchina? Jamaa wanasema kwa sasa wao wanaangalia nafasi,mambo mengine mbele ya safari.

  Sasa,baada ya kuchonga,kuleta utata na kutoka nje ya mada,labda nirudi kwenye mstari,mawazo yangu bado yapo palepale kuwa inabidi tuwaibie wenye hela ili kuwasaidia mafukara wa kitanzania, kwani kuna wizi wenye baraka.

  Natoa wito kwa wataalam wa code wakopi na kubadili baadhi ya code ili nasi tuanze kupata vitu fulani pindi wanajipanga kuandika za kwao.

  Tembelea AfroIT Materials kwa vitabu kibwena online au AfroIT Download kwa self Service.

  Samahani kwa tutakao wakwanza kwani hii ni sehemu ya maisha.
   
 13. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kukwazana kupo lakini mijadala kama hii lazima iruhusiwe.

  Kazi yenu wakuu nimeipenda . Je mmeweza kutafuta contact za ma lecturer kama wa UDSM na vyuo vingine kupitia web z ao na kuwaandikia kuwaomba wawaambie wanafunzi wao watembelee web yenu wakihitaji baadhi ya machapisho ya subject fulani fulani au kuwauliza kama mnaweza kuwapatia online books kama mlizoweka tayari .

  Msichoke endeleeni na moyo huo huo . Tupo pamoja
   
 14. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kilongwe
  I agree with you that ndio, katika maisha priorities change over time. Lakini ni muhimu kuwa na concrete position in terms of morals la sivyo, your current "TIME" tuseme ni nzuri kimaisha, might mean someone elses ni mbaya since we all don't operate on same time cycle. Sasa kama mmoja yupo ok na sasa kwa sababu amefanikiwa priority zake in terms of morals atasema, sifanyi kitu fulani, mfano, nimeacha wizi, while the other persons "TIME" inaruhusu wizi kuwa its ok. Sasa, kwa nini akija kukuibia, unakasirika, unampeleka mahakamani, why then don't you accept that its all part of the "TIME" appreciation.
  Ona jinsi wenye nazo wanajihami kuzuia wizi wa mali zao, sasa wenyewe (most) wameiba, lakini hawataki wengine wawaibie.....

  The only way I can condone any aspect of piracy is where the producer of the product has worked overtime to deny you access to the resource. That would be understandable but where a viable access to these is available at a reasonable cost then I don't see why I can say its ok.
  So far AfroIT (being the only one I can challenge here) has celebrated a birthday if not two. Why don't you do a simple research on your patrons to see how they have actually benefitted from this resource and if at all they can now start producing own materials to appear on the site to complement and maybe eventually remove those that should not be held, linked to and continually being sort to be added to the burgeoning list. Hapo nitaelewa kuwa, mlitaka kujenga knowledge and then share it legally :- au.

  Investor wa kweli aki'iangalia region for investment huwa anataka kujua... Je kweli kuna ethos fulani ambazo zinathaminiwa katika jamii. Akisikia kuwa, to suceed, itabidi 10%'s awe amejumrisha kwenye hesabu zake, akisikia watu wavivu kikazi, watu wezi na hawana the simplest moral compass to guide them basi, huyo atatafuta kwingine. Wanaoshuka sasa kwa wingi are of the like minds with the locals, WIZI mtupu, na ndio watawatengea hao wachache hizo 10% na kuzoa 1000% wakati the rest of the population wanaambulia patupu. Sasa nani kashinda!!!!!
  In your earlier argument then, hii nayo tuikubali kuwa kuna wengine kati yetu sasa ndio muda wao kuchuma kwa wingi.....

  Thats an example of the reality of cementing underhand and negative morals to society......
   
 15. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #15
  Jan 10, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mkubwa awali napenda kukupa pongezi juu ya michango yako,inaonesha umekomaa na malengo yako ni kwenye kujenga.Kama wote tungekuwa hivi basi tungefika mbali.Jia you!

  Tukirudi kwenye ushauri wako,ni kweli tumekuwa tukifuatilia kwa karibu mno kuangalia ni jinsi gani watu wanavyofaidika na vitu vyetu kadri ya uwezo wetu,ingawa bado kuna challenge nyingi zinatukabiri. Kama umeona,siku hizi tumesimamisha kuweka video za watu wengine na tumeshaanza kurekodi zetu wenyewe,tukijumuisha Podcast na mengineyo. Hivyo tunahitaji kamuda na ushirikiano zaidi toka kwa wadau wengi ili kuhakikisha siku ya mwisho kila kitu kinakuwa chetu wenyewe.

  Kama umekuwa ukifuatilia vizuri AfroIT,utagundua kuwa tumekuwa tunapitia mabadiliko kadhaa tangu kuanza kwetu.Hii inamaanisha hatutabaki kuwa tegemezi kwa maisha yote,ila ipo siku itafika AfroIT itakuwa 100% free from Piracy(amini mimi).


  Kuhusu Ushauri wa Mtazamaji,Kaka tumejaribu na tunaendelea kujaribu ila kuna utata kidogo,inawezekana kwakuwa hatupo nyumbani hivyo mambo mengi hutegemea simu na e mail. Ila hatujakata tamaa
   
 16. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera Kilongwe and the team at AfroIT. Nawapongeza tena kwa kuanza kurekodi materials wenyewe na kuziweka kwenye site yenu kwa manufaa ya Mtanzania. Materials zote ambazo from word go, zimetolewa for free from anywhere in the world should appear here na hapo kwa kweli mtakuwa mmefanikisha kitu muhimu kwa jamii. Kumbukeni, watu wakiwapa shukrani, wakiwaombea mbarikiwe zaidi, baraka zitakuja kwani, mmefanya kitu legal for the benefit of the community.

  Nadhani challenge hivi sasa ni kuwa'encourage the ICT experts wetu to contribute their knowledge to this site. Kwanza labda kuwaonyesha ni jinsi gani mtu anaweza kutengeneza materials i.e. to record them and have them available at your site, resources gani anahitaji on their computer (commercial vs opensource) na kama kuna collaborations that can be organised with other people to get materials out.
   
 17. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Uk sahihi binfsi nilikuwa najiluza na najaribu kujifunza ni nmana gani naweza kutumia digital camera ya kawaida kutengeza clip bora za kiswahili
   
 18. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtazamaji,

  commercial: techsmith.com (camtasia studio)
  opensource: camstudio

  Others are as follows
  captivate (not sure who owns this company)

  There should be a few for the Mac operating systems but not sure.
   
 19. HT

  HT JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  our father does not provide home meal so let us go and steal and it is cool. Basically kuna pesa za vitabu tunalipia kodi. So serikali inatakiwa kununua e books. Kwa shule huwa kuna punguzo maalum. Ujuha wa viongozi serikalini sio execuse ya kuiba kazi za watu!
   
 20. HT

  HT JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Linux GTK Record na nyingine nimeisahau ila ukisearch google 'screen recorder' au 'screencast recorder' utapata!
   
Loading...