Pingamizi la CUF dhidi ya CHADEMA latupiliwa mbali Chalinze

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Pingamizi lililokuwa limewekwa na mgombea ubunge kupitia CUF na washirika wake dhidi ya Chadema limetupiliwa mbali na msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Chalinze jioni hii.

Msimamizi wa uchaguzi baada ya kupokea majibu ya Chadema na kuyapitia amesema hoja zote za CUF hazina msingi wowote.

Amesema CUF wameshindwa kuthibitisha chochote na hivyo kuonekana wanapoteza muda tu.

Hivyo msimamizi amemtangaza Rasmi Mathayo Torongey kama mgombea halali wa CHADEMA.

Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa ambaye leo alishangiliwa kwa maneno... Rais...Rais..Rais na maelfu ya waendesha Bodaboda Dar anatarajiwa kuzindua Rasmi kampeni za Chadema Jumapili hii.
 
AAH! Kumbe jamaa hakuwa na uraia wa uwingereza?

Tunajua mtashindwa vibaya huko Chalinze , lakini tunataka mshindwe kihalali, sio kufanya makosa kwa makusudi kwenye kujaza fomu ili msishiriki uchaguzi. Janja yenu tuliishaishtukia
 
Naomba uniruhusu nitunge kitabu chenye tittle "mwalukosi na mkosi wa rambirambi"
 
AAH! Kumbe jamaa hakuwa na uraia wa uwingereza?

Tunajua mtashindwa vibaya huko Chalinze , lakini tunataka mshindwe kihalali, sio kufanya makosa kwa makusudi kwenye kujaza fomu ili msishiriki uchaguzi. Janja yenu tuliishaishtukia

Mkuu kila tukiona jina lako tunachokikumbuka ni Rambirambi za Marehemu Mwangosi
 
Na kwa namna pingamizi lilivyoandikwa unaona kabisa walivyo shallow! Limewavua hadi nguo za ndani!

Msimamizi wa uchaguzi amependekeza itungwe sheria ya kuwadai fidia wanaofungua mapingamizi ya kijinga
 
Back
Top Bottom