Pinda: Wauza viungo vya albino siku zenu zahesabika

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
Pinda%2820%29.jpg

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda



[FONT=ArialMT, sans-serif]Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ukataji viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi waache kufanya hivyo mara moja kwa sababu siku zao zinahesabika.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Napenda kuwaonya watu wote wanaojihusisha na vitendo viovu vya ukataji wa viungo na wauaji wa walemavu wa ngozi popote walipo kuwa siku zao zinahesabika. Ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi nawahakikishia Serikali itashinda vita hii na mtaishi kwa uhuru ndani ya nchi yenu,” alisema. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana wakati akiwahutubia wakazi wa mji wa Iringa kwenye maadhimisho ya Siku ya Walemavu wa Ngozi Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Garden, mjini hapa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha inatokomeza ukatili na unyama wa aina yoyote wanaofanyiwa wananchi wenye ulemavu wa ngozi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alitumia fursa hiyo pia kuwaonya waganga wa kienyeji waache kuchochea ukatili huo kwa kuwadanganya watu.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Nawaomba viongozi wa dini na taasisi zisizo za kiserikali waendelee kuwaelimisha Watanzania juu ya vitendo hivi viovu, vinavyofanywa na wauaji hawa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema pamoja na kuwa nchi inaadhimisha siku hiyo ya walemavu wa ngozi, bado serikali inakabiliwa na changamoto ya kukabili matukio ya mauaji ya walemavu hao nchini ambapo alibainisha kuwa tangu Oktoba, mwaka jana hadi sasa, mlemavu mmoja wa ngozi ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema hali imetulia ikilinganishwa na miata mitatu iliyopita. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akichanganua takwimu za kura ya maoni iliyofanyika nchini nzima Machi mwaka jana, Waziri Mkuu alisema jumla ya watu 97,736 walipigiwa kura kuwa wanahusika na makosa mbalimbali yakiwemo ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kwamba upelelezi wa kina unaendelea kuhusu watuhumiwa hao.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alifanua: “Hadi sasa, watu 3,217 wamefikishwa polisi, watu 295 wamefikishwa mahakamani ambapo kati yao, watu 106 wamehukumiwa kwa makosa mbalimbali, yakiwemo ya vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.” [/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Kati ya kesi zilizofikishwa mahakamani, 11 ni za mauaji ya walemavu wa ngozi. Kesi tatu zimetolewa hukumu na watuhumiwa wanane wamehukumiwa kifo. Upelelezi wa matukio mengine 27 ya mauaji unaendelea,” aliongeza.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kuhusu maombi yao ya kupewa upendeleo wa kupata mikopo kwenye mabenki, Waziri Mkuu alisema sio rahisi kuyaagiza mabenki yaweke masharti nafuu kwa ajili ya walemavu wa ngozi pekee yao kwa kuwa huduma hiyo hutolewa kwa uwiano na biashara ya sasa ni huria. [/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Nawashauri mjiunge kwenye Saccos ili muweze kupata mikopo kwa ajili ya uzalishaji mali muweze kujikwamua kiuchumi. Mkiweza vile vile muendeleze mshikamano miongoni mwenu na mtumie fursa hiyo kujenga SACCOS yenye nguvu… mtaweza kupata fursa za kupata mitaji kama vile mabilioni ya JK kwa manufaa yenu na ya jamii yote ya watu wenye ulemavu kwa ujumla,” alisema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliwataka Watanzania watambue kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wana mchango mkubwa katika jamii hasa wakiwezeshwa na binadamu wenzao wasio na ulemavu huo. “Wito wangu kwa jamii ya Watanzania ni kuwa iwape nafasi kwani wanaweza,” alisema.[/FONT]



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom