Pinda: Wana Mtwara,ni gesi kidogo tu ndiyo inakwenda Dar,makapi yote yatabaki hapa

we jamaa unapotosha pinda hajasema kuwa asilimia moja ya saruji itaenda dar bali asilimia moja ya gesi ndiyo itakayoenda dar na asilimia 99 itabaki mtwara,sasa wewe unayepotosha hatukuelewi lakini ndiyo matatizo ya vijana wa bavicha.

Mkuu hata mimi nilikuwa sijaona upuuzi huo ulioandikwa , kumbe anasema saruji? Dar es Salaam wana shida gani na saruji?
 
Mtwara hawajui matumizi ya Gesi. Itakuwa ni uharibifu wa rasilimali kwa kuwaachia 99%.
 
Waziri mkuu MKPP ameyasema hayo wkt akizindua ujenzi wa kujenga kiwanda cha Saruji mkoani mtwara ktk kijiji cha madimba. amesema kuwa wana mtwara wasiwe na wasiwasi kwani ni kiasi kidogo tu cha saruji ambacho akizidi 1% ndio kitakachokwenda Dar baada ya kusafishwa na makapi (mabaki) yote yatabaki hapohapo Mtwara kwa matumizi ya wana mtwara.
My Take:
Dar niya gesi safi,wana Mtwara niwa Makapi. Tutafika tu,hakuna shida.


Hope ata gesi safi itapatikana kuanzia mtwara, lindi hadi Dar au? Lakini maligafi yatabaki MT and Lindi siyo?
 
baada ya kuelimika juu ya swala la gas kupitia mawazo ya members wa jf,nimeona hakuna tatizo bomba la gas kujengwa kuja dar es salaam kwa sababu za kiuchumi, na hata kama bomba hilo la gas lingejengwa kuelekea nchi jirani naona ingekua sahihi ikiwa tu soko lake linaridhisha. kinachotakiwa ni kupata fedha nyingi iayotokana na rasilimali hii ili kuwekeza kwenye elimu,afya miundombinu nk.

NB: mimi si mkazi wa mtwara!
 
kweli uongozi si elimu, rangi wala umri uongozi ni weledi apo pinda kawatukana live wanamtwara na watz kwa ujumla


CC. THE BIG SHOW
Mkuu sometimes maneno kama haya huwa hayafai.
Makapi yanayotokana na processing ya natural gas ni maliasili ya maana sana, jaribu kugoogle uone.
Makapi ndiyo lugha yenyewe, kwa hiyo usipende kuanzisha vurugu ambazo kwa kweli wala hazitakiwi kuanzishwa. Watu wataopoteza mali na maisha ni watu innocent na wala hawajui hiyo gesi mchakato wake ukoje.

Nawaunga mkono ushinikizaji wenu wana mtwara kutaka uwazi wa mikataba kama mlivyowakilishwa vizuri tu na kambi ya upinzani. Lakini sitaunga mkono vurugu ambazo hakuna atakayeshinda, ni ujinga na ni kutumiwa na watu ambao hata wao hawajui wanachokizungumza.

Kuna vyama vina sera ya gesi asilia, vyama vya siasa .... hiyo lazima ikujulishe kuwa kuna kitu hapo!!!
Acheni hizo bana!!!
 
Tusilumbane sana jmn hii nchi yote yetu kwny ukweli semeni kwny uongo semeni lkn kuonana kwamba huyu ndio mzuri huyu hafai haisaidii, tubadilike tublame kwa kiasi na tukumbuke pia kusifia pale mtu anapofanya kizuri sio lawama tu
 
hivi kweli watu ni kwamba hawafaham au wanaekit ili kupotosha ukweli. ges inayoenda dar ni ile ambayo imeshasafishwa, hii inamaana kwamba mitambo ya kusafisha gesi itakuwa mtwara, hivyo bai mtwara watakuwa wanauza ges kwa tanesko, vilevile percent ambayo itakuwa inaenda dar ni ndogo sana kulinganisha ges itakayokuwa inazalishwa yaani 1% of the production, alafu kitu kingine makapi inaanisha ges ikishachujwa kuna masalia ambayo pia yanatumika kwa kutengeneza mbolea etc. sasa nyie mnashikilia makapi mnajifanya hamueliwi ili kupotosha ukwel,
 
Tatizo la magamba hawaamin km wananchi wakichoka wanaweza kufanya lolote? Wamebaki kusingizia Chadema. Halafu magamba yanasahau mapema km kuku, sasahiv wamechakachua matokeo ya kidato cha nne wanaandaa wamachinga wengine, hawa wakija kuandamana wakidai Haki zao za msingi utashangaa ooh Chadema Hao watakuwa wamesahau uchaka chuaji huu wa matokeo. Kazi ni kubwa kwa watoto masikini
 
Ule mpango wa CHADEMA kutaka kutumia vurugu za MTWARA kama mataji wa kujitafutia umaarufu MTWARA utakuwa umezikwa rasmi.
Jamani mda mwingine tuwe tunajadili masuala ya msingi haya masuala ya vyama yatatugawa. Kinacho takiwa tujadili gesi yetu tutanufaika nayo vipi. Sisi ni wamoja bila kujali itikadi ya vyama.
 
Dawa watoe mkataba uwe wazi, halmashauri za mtwara na lindi zipewe hisa forty percent wawekwe wataalamu wetu hata wa kukodi wasimamie mradi tugawane faida na hasara, pia halmashauri zipewe vipaumbele vya bajeti.
 
Hakuna upotoshaji wowote nliofanya,Amesema gesi ni nyingi sana,Dar itakwenda si zaidi ya 1% ya gesi yote,na makapi ya gesi itakayokwenda Dar yatabaki hapohapo Mtwara.

1% to Dar
99% makapi (Crude gas) For Mtwara.
Kama ni hivyo walikuwa wanagomea 1% ya gesi. Basi mimi nashauri 99% Crude gas (makapi) iende DSM na maeneo mengine ya nchi wao tuwaachie 1% Purified gas.
 
Baadhi ya wanaJF wanapenda umbea sana

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom