PINDA: Ukiwa mkaidi usilalamike pale kichapo kitakapokufikia

Umeandamana bila halali na unaleta fujo zinazohatarisha usalama wa watu na malizao, utatangaziwa uondoke maramoja ukikaidi na kuanza kushambulia kinachofuata ni kichapo tu tusidanganyane hapa
Nahii hata ukitokea washington au london au paris watatembeza kichapo tu
 
Ni kweli hata Mwangosi huko Iringa alikataa kutii "amri halali" na waliomba " ushaidi hawakupewa. Heeh eeeh . Hivi amri halali ni kuzuia maandamano kwa kisingizio cha inteligensia kila wakati. Kwa polisi wetu amri halali ni ile kuzuia jambo lisilowapendeza watawala lisifanyike, na sio kuwezesha jambo lifanyike .
Ninadhani pia wale waliopo kwenye makundi ya "wasiotii sheria/amri halali" ndio wa kuwashangaa zaidi...Ni mara ngapi serikali imeshawasihi watu wawe wanatii amri halali?....Inabidi kutumia mbinu mbalimbali katika kuleta amani....sasa kama kuna watu ambao umejaribu kutumia mbinu mbalimbali ili wasilete vurugu lakini unaona bado hawatii,unaweza jaribu na kufanya "extra mile".....inaeleweka mahakamani "miyeyusho na gharama" nyingi....kama vile wananchi wanavyoamuaga kufanya mahakama zao zile mwaita "Wananchi wenye hasira kali"...kwanini nara nyingi huwa mnawatetea wakati mnajua kuna mahakama?...

Mimi niko pamoja na Pinda..."asiyetii amari halali arambwe virungu tu"....ILA tafadhali wale watiifu waachwe wa enjoy.....
 
Ndugu wana jamvi, mambo yanayoendelea sasa katka nchi yetu kati ya mlinda dola na mtaka dola yana mengi ndani yake mpaka kufkia hatua ya kutoa ruhusa mjengon kuwa wanausalama ruksa kuuwa kwa mtutu na virungu. Hofu kubwa iliyopo ni kwamba, dili nyingi zimesainiwa tena kipindi hiki cha mwisho wa muhula wa pili wa mkuu wa kaya, mambo mengi ya kiutajiri yamegundulika nchini ikiwemo gas, uranium na resources nyngne nyingi. Mikataba ming imesainiwa na mchina na wengine walaji weng na hiv karibun raia namba moja wa dunia atatua nchini kumalizia vyake. Dili hzi zilizosainiwa ni hatar wakimuachia Dr Slaa aingie magogoni, ataharibu kila kitu na kuwashtak kama si kuwafunga jela wengi. Hawako tayari Dr Slaa aende kuharibu dili zao 2015. Mirad ya wiz kama jiji la kigambon ambalo ndo sababu hasa ya kuletwa gasi ya mtwara dar wana hofu wataharibikiwa. Kuna mambo meng sana nyuma ya mauaji ya raia wa TZ. Ikulu hailali kuhakikisha inapata muendeleza dili wa mwaka 2015. Hiv unajua kaz halis ya kitengo kipya cha ikulu cha PDU?
 
Nendeni mkaangalie mikutano ya WTO watu wanavyochezea virungu wakijaribu kuleta purukushani kusumbua wakubwa.
 
Lete chanzo cha habari yako vinginevyo. Ni ----- tuu huu

"To know the enemy is half the victory"
 
Kwani Kikwete akisaidi bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dsm anasaini kwa niaba yake peke yake?

Kwani nyie Chadema malengo yenu ni kuharibu haya mafanikio yote ya serikali yetu sikivu? mnataka kutuambia hata barabara za lami mtazibomoa kisa walijenga CCM?

Kama ndio malengo yenu hayo basi magogoni mtaisikia kwenye redio tu labda kwenda kunywa juice ya Box na kuondoka.
 
siku zote huwa tunasema hatuna wabunge,,,na kama wapo hawajui nini wanakifanya katika chombo chetu cha uwakilishi,,mfano ni tukio la jana ambapo wakati waziri mkuu akijibu swali la mbunge alisema wanaokaidi na kuvunja sheria wapigwe wakati akisema hayo wabunge wote walikuwa wakishangilia kauli hiyi bila kujua au kujua kuwa wao ndio watunga sheria na wasimamiaji wa sheria hizo,,,jee tukio hili la wabunge kushabikia kauli hii linatoa tafsiri gani kwa viongozi wetu hawa,,,,??
 
Ni kweli hata Mwangosi huko Iringa alikataa kutii "amri halali" na waliomba " ushaidi hawakupewa. Heeh eeeh . Hivi amri halali ni kuzuia maandamano kwa kisingizio cha inteligensia kila wakati. Kwa polisi wetu amri halali ni ile kuzuia jambo lisilowapendeza watawala lisifanyike, na sio kuwezesha jambo lifanyike .

Mkuu polisi ni binadamu na wanamakosa yao pia kama hayo ya kuua kupora mali za watuhumiwa kusafirisha bangi nk

Lakini hii haiondoi uhalali wa wewe kukaidi utii wa sheria

Naamini chama bora ni kile kinauza sera zake na si kukimbilia maandamano kutafuta attension ya watu
Na nakuhakikishia hakuna nchi duniani ina intertain maandamano ya hovyo hovyo tu, kila kukicha tutaanda maandamano ya hiki mara kile hivi hawa waandamanaji hawanaga kazi za kufanya kweli? Kwanini msiwaambie njia za kujiingizia vipato badala ya kuwatumia kuandamana tuuuuu then what next

Komenti za wengi humu ndani na hii ni hadi kwa viongozi wa cdm wanaonekana wanaota ndoto ya yaliojiiri misri,syria nk
Watu wanaota njia ya mkato kuingia ikulu kwa mgongo wa haki ya kuandamana kisha nchi iingie kwenye machafuko

Hakuna haki bila wajibu wala uhuru bila mipaka vinginevyo itakuwa nifujo tu
 
Maana yake ni kuwa zile kura walizopewa na wananchi hawana shida nazo mwaka 2015 wakati wa uchaguzi.
 
Nauliza hivi kwa sababu Watz wanaamini kwamba serikali yao huendeshwa kwa kufuata misingi ya sheria na katiba likiwemo jeshi la polisi. Na iwapo Pinda ametoa agizo hilo bila kunukuu sheria basi sasa anataka serikali yake iendeshwe kidikteta maana udikteta huendeshwa bila kufuata sheria na katiba.

Sioni tafsiri nyingine, au wenzangu mnasemaje?
 
Ukiruhusu hisia za mwili wako kufanya maaumuzi badala ya utashi, kunakuwa na tofauti ndogo sana kati wanyama wa kawaida na binadamu. Mh. ni mara ya pili sasa anapingana na sheria za nchi alizoapa kuzilinda kwa niaba ya wanyonge(ambao leo anaamuru kupigwa kwao) kwa sababu ya hisia. Akumbuke kuwa wanaopigwa na kufa kama inzi ni watanzania wanyonge na wasio na hatia na sio wale ambao yeye angependa wapigwe...! this is inhuman....!
 
Siungi mkono kuua lakini tunaotoa hoja katika jombo hiki adhimu kinachosomwa na watu wengi Duniani, tutoe vitu ambavyo ni sensible uongozi wa Nchi si kazi rahisi sana kama tunavyojaribu kuliweka na hao mnaomtukana Mzee Pinda mnajichumia dhambi ya bure, unapoongoza watu, wengine wamo vichaa, wengine wakolofi wengine wanataka sifa tu sasa katika hali hiyo bila kuwapo na miiko kila mtu atafanya anachotaka. Mwenyezi Mungu mwenyewe aliliona hilo akatuwekea seria na kila aliyekiuka alipata kipigo sembuse uongozi wa wanadamu? kwanza nashangaa kwa nini serikali inafanya ulegevu katika hili hata ndani ya familia mtoto usipomtia mkongato hashiki adabu, siku moja anaweza akakwambi toka nilale kitandani kwako, ongeza viminyo na anza na hao wanaowachochea vijana wetu innocent wanaoingia barabarani bila kujua ni kwa faida ya nani. Hivi kweli kwa akili ya kawaida ninyi mnaomwita Pinda poor watu kuandamana na kuchoma majumba ya watu wawaache tu au kugomea gasi isitoke, kwa akili yenu ni agenda yenye mashiko? je wa Rukwa tukipata mafuta Lake Tanganyika yabaki Rukwa, huu ni utoto na ninyi ndo ambao mko poor kama si hivyo mna kichaa cha elimu mbaya la sivyo mna mabwana wanaowalipa kutaka kuvuruka amani yetu. Big up Pinda.
 
...ngoja wazee wa kazi warudi bungeni waombe muongozo wa kuwawajibisha, utawaona wanalia pale mbele...
 
Back
Top Bottom