"Tumeagiza matumizi yasiyo ya lazima yasimamishwe, tubane matumizi kwelikweli ili shughuli za serikali ziendelee kama kawaida, kweli mfumuko wa bei unapanda sana ingawa tumejitahidi kutafuta kila mbinu, lakini haitusaidii," alisema Pinda na kuongeza:
"Tumejitahidi kuondoa ushuru wa sukari inayotoka nje, lakini bado haitoshi, mafuta nayo yanapanda bei kila siku hivyo tunaomba wafanyabiashara waisaidie serikali wawe waaminifu wasipandishe bei bila sababu."
Serikali inakabiliwa na hali mbaya kutokana na uhaba mkubwa wa fedha za kuendesha shughuli zake. Kutokana na hali hiyo, serikali imeziagiza wizara na taasisi zake kufunga mkanda na kuhakikisha wanabana matumizi ili angalau fedha zilizopo ziweze kumaliza mwaka huu wa fedha wa 2011/2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo bungeni jana wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge. Pinda alitoa kauli hiyo wakati akimjibu Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed, aliyetaka kujua serikali inafanaya nini kupunguza makali ya maisha kwa watanzania hasa kutokana na kupanda kwa kiwango cha mfumuko wa bei.
Mohamed alihoji kama serikali imefilisika kwa kuwa Wizara na idara zake zote zimekuwa zikilalamikia ukata. Mbunge huyo alisema hali ya maisha ya Watanzania inazidi kuwa mbaya kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu, lakini serikali haionyeshi jitihada za makusudi kukabiliana na hali hiyo. Katika majibu yake, Pinda alikiri kuwa hali ya maisha imepanda, lakini si kwa Watanzania tu kwani hata nchi zinazoizunguka nchi hali ni hivyo hivyo.
Tumeagiza matumizi yasiyo ya lazima yasimamishwe, tubane matumizi kwelikweli ili shughuli za serikali ziendelee kama kawaida, kweli mfumuko wa bei unapanda sana ingawa tumejitahidi kutafuta kila mbinu, lakini haitusaidii, alisema Pinda na kuongeza: Tumejitahidi kuondoa ushuru wa sukari inayotoka nje, lakini bado haitoshi, mafuta nayo yanapanda bei kila siku hivyo tunaomba wafanyabiashara waisaidie serikali wawe waaminifu wasipandishe bei bila sababu.
Hata hivyo, Pinda alisema kuwa serikali haijafilisika. Pamoja na hayo serikali haijafilisika kwani ingekuwa hivyo wewe usingekuwa hapa bungeni? alihoji.
CHANZO: NIPASHE
Mijadala ya awali:
Hivi mnatumia mifumo hipi kichama kuwapa nafasi za juu watu kama hawa. So far nimekutana na watu wanaoniambia Mh.Pinda yupo Ikulu muda mrefu (to me it doesn't mean he is a qualified decision maker nor a useful spokes person), majibu yake ya pumba pumba kuanzia sakata la mgomo wa madaktari, issue ya Jairo, posho za wabunge and many more says it all.
Na alivyo pimbi yeye huwa hanafikiria in terms of the higher echelon kwenye majibu ya bajeti or social issues. Ukweli wenyewe tuna safari ndefu sana ya kutafuta accountability and democracy, especially kuwafanya hawa jamaa wajue wajibu wao vilivyo or else may be its just me and my views of how responsibility should be, are outdated or do not fit the Tanzanian society. Lakini kama siasa inatumika Pinda ni pumba tupu na majibu yake.
"Tumeagiza matumizi yasiyo ya lazima yasimamishwe
pinda ni janga la kidunia. Nachelea kusema ni aibu kumsimamisha katika jukwaa moja na mwenzie raila odinga kwani mwenzie yuko deep sana na ana mtazamo wa kimaendeleo.
Tutamkumbuka sana dr slaa, angekuwa presdaa asingetuwekea watu legelege kama hawa katika nafasi muhimu. We fikiria eti pinda, ngeleja na werema ni sehemu ya baraza la mawaziri... Nchi hii ina laana au aliyetuloga alikufa.
Serikali inakabiliwa na hali mbaya kutokana na uhaba mkubwa wa fedha za kuendesha shughuli zake. Kutokana na hali hiyo, serikali imeziagiza wizara na taasisi zake kufunga mkanda na kuhakikisha wanabana matumizi ili angalau fedha zilizopo ziweze kumaliza mwaka huu wa fedha wa 2011/2012.
...
CHANZO: NIPASHE
Mijadala ya awali:
Hilo jibu la waziri ni jibu la kipumbavu kabisa!
Angechanganua makisio ya mapato na mapato halisi kwa miezi kumi iliyopita.
Halafu atuambie matumizi ya mapato, na ukasi unaotukumba ni wa kiasi gani na wizara zote zipunguze matumizi kwa asilimia ngapi.
Huyo mbunge wa CUF aliridhika na hilo jibu kweli?... yaani hamna swali la nyongeza?
That was too shallow!
Sidhani!