Pinda na umiliki wa Sumry Express

Status
Not open for further replies.

sasa wewe umebase kwenye nini wakati huna chochote?
 
Haya sasa, bahati mbaya huwa haingii humu
 
huyu bwana ametumwa kuzusha na kuchafua hapa, hamna cha point wala nini wewe mzushi tuu, kama sio mzushi thibitisha kauli hio. Kwasababu mwananchi wa kawaida ambaye anaweza kupata taarifa kama hizi ni mwananchi wa kawaida wa aina gani huyo? ni wazi kwamba anatudanganya hapa lakini anamjua aliemtuma kufanya hivi. Tumeshawazoea hawa.
 
Wewe lazima ni mganga unayenunua viungo vya ALBINO, una hasira na Pinda kwa sababu kakumwagia mboga. Unaleta vitu ABSTRACT, hatujui hata tuanzie wapi
 
Huyu mwanzilishi wa hii thread atakuwa mfuasi wa Maige.
 
Lete ushahidi wa madai yako...
 

Tupe supporting document ya claims zako!! Tunakwenda kwa data maana hii ni story ambayo tungependa tuhakikishe ukweli wake!!!! But between kwa mshahara wake na marupurupu kwani haruhusiwi kuwa share holding? Mbona Azimio la Arusha lilishakufa na sasa viongozi wetu wanaishi kwa Azimio la Zanzibar lililozalisha mafisadi na mabepari tulio nao ndani ya SSM? Mbona huyu mzee ni cha mtoto? Tena ni maskini sana kwa uwekezaji huo maana wenzake wana vitalu vya wanyama na twiga na tembo hai wanaandaa mbuga ndogo majuu huko. Sema lingine hili dogo sana.

Kingine uwanja wa ndege hajengi yeye ni serikali na mkoa ule mzima maendeleo yako chini sana na ardhi nzuri na uwekezaji umeanza na unahitaji miundombinu. Ehee lete lingine!!!

Kuhusu Yambesi hata kama asingekuwa ni kabila lake but ni mchapa kazi maarufu anajulikana tangu akiwa Mkurugenzi wa Policy Utumishi. Ana certificates za the best accomplishments for the public service tena toka nje ya nchi. So hata kama akiwa ndugu yake but ana uwezo na ni mchapa kazi. Mbona usimseme yule ndugu yake jamaa wa kitengo cha computer kule kweupe bila elimu ya kutosha? Mbona usimseme Halfan Mkurugenzi wa sasa wa Tantrade ambaye ni nduguye mkulu but ni mchapakazi na kule Tantrade amefanya kazi kubwa smart kabisa. He is mchapakazi. Leta habari ingine!!!!!!!
Una lako jambo!!!!!!
 
Toka aukwae u Pm barabara fasta, mkoa mpya wa katavi, isue ya kilimo kwanza fasta Rukwa, mabenki yanafunguliwa mpaka kina Kibonde na lift za ndege za siricali kwa ajili ya PR, teuzi mbalimbali za huko kwao. Nakubaliana kwamba Rukwa ilisahaulika lkn kigoma je? singida nk. au ndo anafuata nyayo ya za Msuya? Pinda binafsi amenithibitishia kuwa ni mtu mbinafsi sana. Si ajabu ubinafsi kurandana na mada tajwa. Mnaohoji hamna data bora ukae kimya. Inawezekanaje waziri wa Tamisemi na senior state officer akawa na mil 20 benki kama Pinda alivyotaka tuamini? kwani hatujui zaidi ya nusu ya mwezi anakuwa nje ya kituo na analipwa posho na bado huko anakoenda analipiwa kila kitu? msitufanye mafala. period!
 

acha habari zisizo utafiti, sumry express ina umri gani? na pinda amekuwa waziri mkuu tangu lini?. wewe mwenyewe huna ushihidi unaongea kwa hisia kuliko logic. kafanya uchunguzi halafu utoe viashiria halisi hapa.

umeanza sumry, unakwenda uwanja wa ndege mpanda, unakwenda kwa yembes. vyote hakuna hata moja lenye japo ushahidi, si ungekaa kimya kuliko kuongea vitu hata ushahidi huna
 
wabongo kwa wivu na chuki..unless una evidence hizo ni accusations tu
 
yale mabasi yenye picha y penguine yanaitwaje? huwa yanapiga ruti za dar-mbeya na dar-tunduma.
 
kumbe huyu mzee naye jizi?? sasa kwa ccm nani kabakia safi??
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…