Hilo la kauli kuitolea bungeni..Huko ni kudilisika kimawazo. Huyu Pinda si ndiye mliyekuwa mnamwita mpole mdhaifu. Halafu kumbukeni kuwa kauli ile katoa ndani ya ukumbi wa Bunge ambao una kinga kisheria. Vinginevyo waache wauze tu sura na wao wajipatie kipato
mbona mi ni chadema lakin ni mnyaturu,vp zito,wenje,sugu,msigwa,slaa, n.k usichangie post kiukabila.
Mkuu hapo kwenye neno la mwisho pigia mstari,ushahidi ni mkoa anaotoka.....afungwe tu maana tumechoka sasa kha!!Pathetic Pinda,
Kauli zake na matendo yake hayana tofauti na mchawi
na safari pia ni mchaga,
na baregu
na marando,
na watanzania wooooote ni wachaga.
Hujaelewa tafsiri yake ya "wachaga".
Wewe ndiyo mwanasheria mahiri?
Dua la kuku kamwe halimpati mwewe,kesi haiwezi kuwageuka.Mwisho wa siku lazima haki itapatikana!
Usikwepe kujibu swali ambalo unajua jibu lake.Ujiulize mwenyewe kwamba mtumiwa anapigwa au anafikishwa kwenye vyombo vya sheria? Yeye Pinda aliposema "wapigwe, tumechoka sasa". wamechoka yeye na nani, na kwa sababu gani? Fuatilia mada humu jamvini, kwamba JWTZ yawateka watu wanne waliokuwa wanashangilia mjadala wa juzi - ITV ambapo JWTZ walitumumiwa kwa kuwafanyia watu vitendo vya kinyama. Kwa hiyo anayeshangilia apigwe tu?
Ukumbuke kauli za Pinda zenye maelekeo ya serikali kujichukulia sheria siyo kitu cha mara ya kwanza. Hata wakati wa mauaji ya albino alisema wauaji wa albino wauawe badala ya kusema washtakiwe. Kama hukumu ndiyo itakayosema wanyongwe hadi kufa ni sawa lakini siyo kiongozi (ambaye siyo hakimu) hana mamlaka ya kusema wauwe.
Usikwepe kujibu swali ambalo unajua jibu lake.
Anayetazamiwa KUPIGWA ni yule mleta fujo, muandamanaji ovyo, asiyetii amri halali, na hata mdharau mamlaka.
Kama wewe umo katika kundi hilo subiri kisago , maana kwa uhakika kitakujia.
Usijiingize ndani ya kundi la kondoo ilhali wajifahamu kuwa wewe ni chui mrarua amani nchini.
Pengine uelewe vile vile kuwa HAKUNA sheria itakayokupa kinga wakati unararuriwa ukifanya vitendo vilivyo kinyume na ustaarabu wa amani ya nchi.