Pinda: Dowans hatuirudishi bungeni

Good move mzee Pinda. Kama kisheria tunatakiwa kulipa tuwalipe otherwise deni litakuwa kubwa tutashindwa kulipa matokeo yake tutabakia kugawa rasilimali zetu kama pipi kwa mafisadi.
 
Bunge letu ni la vikaragosi, niliandika article mwaka 2007 kwamba tunaitaji bunge lenye meno. Katiba inasema Bunge ni mshauri wa serikali. sasa kama serikali haitaki kushaurika, then bunge halina kazi.
 
Waandishi wa habari wa Tanzania wamejawa na ulimbukeni kwanini hawajauliza hatma ya wastaafu wa East Africa Community? Kwanini wasingeuliza mbona Valambia hajalipwa na Serikali licha ya mahakama ya rufaa kuamuzru alipwe? Something fishy here anyway nilikuwa napita tu nikasimama kidogo ngoja niendelee na misafara yangu...
 

Jibu rahisi sana EAC au Valambhia saga CCM wanafaidika nini? Dowans tunajua kuna Rostam Aziz na wenzie ambao tunajua kinachoendelea nyuma yao ni nini!!!
 
Huu ni ukuku mtupu wa serikali ya JK..... kwani kazi iliyofanywa na Mwanasheria Mkuu na ofisi yake ina mashaka??? kwa nini iundwe timu nyingine tena???.........as always son of the peasant doesnt know what to talk!!!!!
 

Inaonekana hawataki kabisa CDM wawe na nafasi kwenye huo mchakato!!Kwani wao hawana wataalam wa sheria wanaoweza kuhusishwa??
 
Good move mzee Pinda. Kama kisheria tunatakiwa kulipa tuwalipe otherwise deni litakuwa kubwa tutashindwa kulipa matokeo yake tutabakia kugawa rasilimali zetu kama pipi kwa mafisadi.

Another CRAP in the house!!!Hizo rasilimali ambazo bado mafisadi hawajagawana ni zipi haswa????
 
Another CRAP in the house!!!Hizo rasilimali ambazo bado mafisadi hawajagawana ni zipi haswa????

Lizzy kwa kukufunua tu,

we have 185 billion we need to pay pia usisahau kuwa there is a 7.5% p.a ,

= $24,168.343.83 plus 7.5% = unapata bei gani? (Kumbuka hiyo ni hadi June 2010).

= $39,935,765.50 plus 7.5% = unapata bei gani (Hadi June 2010).

Sasa jua kwamba tunaelekea June 2011.

Tukiendelea kulumbana tunaingia 2012, 2013 mwishoe tukistuka deni ni kubwa kiasi serikali haitaweza kulipa unadhani serikali yako hata kama ni Dr Slaa atafanya nini?
 


Tatizo ni kwamba ccm wanang'ang'ania tulipe sio kwa faida ya nchi kama ulivyoainisha wewe ila kwa faida yao binafsi!Ingekua ni kitu chenye uhalali kusingekua na asilimia kubwa ya watu wanaopinga huo ulipwaji....maana kama mmiliki tu hatajwi unategemea nini???
 
Tume ya Chenge et al ambao ni wezi pamoja na kiranja wao mkuu. Hivi Dowans waliposhindwa kutoa umeme wakati ule walilipa adhabu ambayo ilikubaliwa? Vile vile maagizo ya Bunge kuhusu Richmond yalifuatwa na serikali?

Serikali haiwezi kulirudisha hili swala bungeni kwa sababu wanafahamu nini kitafuata. Ni wajibu wa wabunge wa upimzani kuona swala hili linajadiliwa bungeni ili tukate mzizi wa fitna. Pinda hana uwezo wa kuzuia swala hili kule bungeni.
 
  1. Walitingisha kiberiti kuwa uamuzi umetolewa na ICC eti Dowans walipwe 185 bilioni, tukaguna.
  2. Wakagutuka wakadai kuwa haikuwa 185 bilioni bali 95 bilioni, tukaanza kujiuliza kulikoni ?
  3. Wakati hatujakaa sawa wakasema ni lazima tulipe kwani hamna tena ujanja, tukataharuki.
  4. Wakaanza na vitisho na matusi kwa kudai Ikulu haihusiki na sakata la Dowans, tukaguna tena.
  5. Wakitisha kikao cha walaji (CCM) na kubariki malipo kwa matapeli, tukasema wakilipa hapatatosha.
  6. Wakaitisha kikao cha wabunge kuweka mkakati wa pamoja, Mungu si athumani, wakakwama.
  7. Wakaunda kamati ya wanasheria wao wabunge eti kutafuta muafaka, tukaguna kwa sauti kubwa.
  8. Mwanasheria moja, Mkono, fisadi aliyekubuhu ataka tujadiliane na wezi watupunguzie - iwe bil. 50 ?

Hapana Pinda, ujanja umekuishia kwani umegeuzwa kuwa tambala bovu na chafu la kupigia deki ! Dowans iende bungeni tuwajue kwa majina na sura watakaowatetea hawa wezi tu tuwashughulikie kama maadui wa taifa.
 
Shame on our country

 
Nakubaliana na wewe, ila tatizo Lizzy kama umetafakari vizuri hii sarakasi mafisadi wamejipanga na kuibana serikali kisheria sasa sijui hata tukipinga sijui kitu gani tutafaidika nacho!
 
Nakubaliana na wewe, ila tatizo Lizzy kama umetafakari vizuri hii sarakasi mafisadi wamejipanga na kuibana serikali kisheria sasa sijui hata tukipinga sijui kitu gani tutafaidika nacho!

Yani wewe Mdondoaji ni mdhaifu sana....kwahiyo kama wamejipanga na sisi hatuwezi kujipanga????
Acha kua mwepesi wa kukubali kushindwa kiasi hicho!!
Refer post ya Mag3 ....kama tungekubali tangu mwanazo kulipa Bil 185 tungekua tumejisaidia au tumewasaidia?Think about it!!!
 

Sawa Lizzy,
Hata hivyo kama mtu niliyepitia sheria kidogo napendelea kulifahamu na kulisupport jambo ambalo kisheria we can build a case to defend it. Sasa kama jambo naliona kabisa tunaelekea kushindwa tukawa tunalazimisha tu kwakuwa wengi wanaliunga mkono I stand away from the crowd!!!
 
Wakoloni wote wa Kiarabu na kizungu walitutawala kwa kutumia Katiba na sheria.
Wlitunyanyasa kwa kutumia katiba na sheria.
Walituibia na kutupokonya kila kitu kwa kutumia katiba nasheria.
Walitufanya watwana na kutuweka pamoja na kundi la hayawani kwa kutumia katiba na sheria.
Walituziba macho na masikio na kutufunga midomo midomo yetu kwa kutumia katiba na sheria.
Walitufanya tuamini unyonge,umasikini, mardhi na hali yetu duni ni majaliwa yetu kwa kutumia katiba na sheria.
Walitufanya tuamini kwamba kila wasemalo ni kweli kwa kutumia katiba na sheria.
Walitutetemesha kwa katiba na sheria.

Kwa kutamani matunda waliyofaidi wakoloni kwa kutunyonya bila Huruma Viongozi wa CCM wanatumia katiba kuwanyonya kwanza wanachama wanyonge na ndondocha wa CCM wanao unga mkono uwepo wa CCM huku CCM ikiendelea kuwatia katika umasikini.
Pili wanawanyonya Watanzania wote kwa kuwalazimisha kuamini kwamba hawana namna nyingine kuweka mambo yao sawa bali kutii bila maswali hoja za CCM, na zaidi kuamini kwamba kitokacho midomoni mwao ni wakfu.

Leo hii CCM nao wanatuingiza tena katika makucha ya kugandamizwa kiuchumi kisiasa na kiutamaduni kwa kutumia katiba na sheria ya nchi.
Wanaruhusu wageni kurudi tena nchini na kutuibia tena kwa kutumia hial zile zile za Kikarlpeters ( Waziri anapewa shanga za kiunoni na kuvaa yeye na mke wake kisha nasign mkataba wa kuliingizia taifa mabilioni) kwa kutumia katiba,sheria, PORISI na RISASI.

Tuliwafukuza wakoloni weupe kwa kupiga mayowe tukabwetekaa, tukatoa mwanya kwa wakoloni weusi ambao wananyonya hadi kukata ziwa na chuchu zake.
Tunapambana na wakoloni Weuse wa Mashati ya kijani wanaolindwa na Kikosi cha Uslama wa Taifa na RiMwema na maPolisi wote na Viongozi wa ngazi za juu wa JWTZ wasiojali Captain kala nini.
Wako tayari kuweka watu jela na hata kuua ili kukata kiu yao ya Kinyonyaji.

Ukoloni ni ukoloni tu ufanywe na mtu mweupe au mweusi.
CCM ni Genge la Wakoloni weusi.


Sisi waTanzania ni kwa uwing na ujumla wetu ni WAFAAKIRI.

Ukweli ni huu kama tulivyo vaa khanga na kofia za kijani na kufakamia masinia ya wali na kuwapigia kura ili wapate rungu la kutubonda, ni hivyohivyo itabidi tusimame kidete kuwaondoa hata kama gharama yake ni uhai wetu.
 
Ha ha Tanzania is a special case. Raisi anaweza aka jitokeza na kusema tofauti na waziri mkuu. Kisha tutaambiwa haya yalikua maoni binafsi ya Mizengo Pinda na si tamko rasmi kutoka kwa waziri mkuu. Mh au wana tingisha kiberiti tena???
 
Pinda is not the pinda anymore ameishapinda tayari, hakuna cha mtoto wa mkulima anymore wameishamvisha joho la ufisadi, mafisadi wameishateka akili yake hawezi fikiria wala kusema chochote against them he has already lost credibility.

Halafu hii serikali inanishangaza sana kila mtu anaongea la kwake halafu rais yuko kimya ndio maana siku moja jamaa mmoja aliuuliza hivi rais wa nchi hii ni nani?
 
And as far as i know haya siyo maamuzi ya serikali kama pinda anavyosema bali ni maamuzi ya cc ya ccm halafu anakuja kusema serikali wakati ishu hata bungeni haijafika what a crap huyu jamaa akili zake wameishazichezea
 
Ha ha Tanzania is a special case. Raisi anaweza aka jitokeza na kusema tofauti na waziri mkuu. Kisha tutaambiwa haya yalikua maoni binafsi ya Mizengo Pinda na si tamko rasmi kutoka kwa waziri mkuu. Mh au wana tingisha kiberiti tena???

He he he thats what i was talking about Pinda atakuja na la kwake, Mwanasheria mkuu naye atasema la kwake yaani ni mvurugani at the end of the day all i can see here is a kind of game being played kuwapumbaza watu, chukulia mfano ishu ya katiba kila mtu alikuwa anaongea la kwake kuanzia Tambwe Hizza, Makamba, Mwanasheria Mkuu, Celina Kombani halafu at the end of the day Rais naye anakuja na statement tofauti kabisa kama sio kucheza na akili za watu maana yake ni nini???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…