Pinda azitaka asasi za kiraia ziwe chachu za ajira

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumanne, Novemba 20, 2012 06:56 Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amezitaka Asasi za Kiraia (Azaki) kuwa chachu ya upatikanaji wa ajira kwa vijana kwa ajili ya kutimiza lengo la kuisaidia Serikali na jamii kwa ujumla. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam juzi, alipozindua Jumuiya ya Waarabu Tanzania.

Alisema kuweza kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake ni lazima asasi za kiraia zifanye kazi zao kwa kuisaidia jamii.

Alisema hivi sasa Serikali inakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwamo ukosefu wa ajira kwa vijana, utoaji wa huduma kwa wazee, yatima na walemavu, ambao ni makundi anayohitaji mahitaji maalumu.

Alisema kwa mujibu wa takwimu mbalimbali, zinaonyesha makundi hayo yanayohitaji msaada ambapo hivi sasa vijana ni milioni 23.4, sawa na asilimia 10.5 na kati yao milioni 1.4 wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira.

Alisema kundi jingine ambalo aliitaka jumuia hiyo kuliangalia kwa karibu ni la wazee ambalo kwa sasa wamefikia idadi ya milioni 2.4, sawa na asilimia 5.3 ya Watanzania wote.

Alilitaja kundi jingine kuwa ni la yatima, huku akisema kuna takriban yatima milioni mbili wanaoishi katika mazingira magumu.

Alilitaja kundi jingine kuwa ni la walemavu ambao kwa mujibu wa sera ya Taifa ya mwaka 2004, kuna takriban walemavu milioni 3.5, sawa na asilimia 7.8 wanaohitaji kusaidiwa.

“Hii ni kwa sera ya Taifa mwaka 2004, lakini kwa sasa wanaweza wakawa wameongezeka zaidi, kundi hili lina changamoto kubwa ya kumudu maisha yao, hivyo taasisi hii iwasaidie zaidi na kuangalia uwezo wa kutoa fedha katika makundi haya.

“Katika kipindi cha miaka miwili kulikuwa na shetani mkubwa hapa nchini, ambapo wafanyabiashara na washirikina waliwaua watu wenye ulemavu wa ngozi.

“Mwaka 2011 kulikuwa na jumla ya taasisi 5,994 ambazo zimejikita zaidi katika maendeleo ya wananchi katika kutoa elimu, lakini wana wajibu mkubwa katika kuangalia suala zima la utunzaji wa mazingira,” alisema Pinda.

Awali, Katibu Mkuu wa Muda wa Jumuiya hiyo, Mohamed Sufrin, alisema taasisi hiyo ni ya hiari, yenye lengo la kuunganisha jamii, huduma za afya na taasisi nyingine za kijamii.

Alisema taasisi hiyo itakuwa na utoaji wa misaada na kushirikiana kwa ajili ya kuweka malengo ya maisha bora kwa wananchi.

“Taasisi hii haina malengo ya kutafuta maslahi binafsi na kwamba wameona Serikali pekee haiwezi kufanikiwa kutatua matatizo ya wananchi katika kushirikiana, huku akiwataka baadhi ya waumini mbalimbali kuzisaidia jamii ambazo hazijafanikiwa,” alisema Sufrin.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Back
Top Bottom