Pinda azidi kumwaga Chozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda azidi kumwaga Chozi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwiba, Mar 3, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  2009-03-01 13:13:38
  Na Mwandishi Maalum, Ireland


  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema kuwa mgogoro wa kifedha duniani usiwe kisingizio cha nchi wafadhili kuacha kutimiza ahadi zao za kuzisaidia nchi zinazoendelea.

  Katika mhadhara wake kwenye Chuo Kikuu cha Dublin juzi jioni, Waziri Mkuu, alisema kushindwa kutimiza ahadi hizo kutaongeza nyufa za maendeleo kati ya nchi tajiri na masikini.

  Alitoa mfano kuwa kuna methali ya Kiswahili nchini Tanzania inayosema: Usipoziba ufa, utajenga ukuta.
  ``Naomba, mpaka sasa hivi, kuwa msukosuko wa fedha wa kimataifa usiifanye Ireland na nchi nyingine washirika wetu wa maendeleo kuacha kutimiza ahadi zao za misaada ya maendeleo kwa nchi zetu,`` alisema
  Endelea... Mgogoro wa kifedha duniani usiwe kisingizio wafadhili kutusaidia-Pinda

  ------------------------------------

  Hapa Pinda anawambia nini wafadhili ? ..Usipoziba ufa...! Je kuwaachia akina Lowasa na Karamagi na wengine ni kutwambia kuwa watakao kuja itabidi wajenge ukuta ? Maana mpaka leo ni miaka inakatika akina Pinda na wenziwe wanawaburuza waTanzania katika kuuziba ufa huu uliojitokeza maana hata kuuita ufa ni aibu tuliokuwa nao ni mpasuko kabisa ambao upasuko wake unaona mpaka upande wa pili bila ya kuhitaji kuchungulia ,Pinda wajibika hapa nyumbani kwanza ndio hata hao wanaokusaidia au wanaotusaidia wataona jitihada zenu ,msione mnawaburuza WaTanzania mkafikiri na hao wafadhili hawafuatilii ,itakuwa mnajidanganya ,maana wao ndio wanaofuatilia kwa ukaribu na kuyachunguza mambo na kuyajua kwa undani ,usiombe wakifika kutoa ushahidi ,utawala wetu huenda ukaumbuka.
   
 2. Giro

  Giro JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 360
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwani lazima??? wakigoma utawafanya nini??
  Kila siku umatonya tu.Mnashindwa kapambana na mafisadi mnalazimisha kingi.Yani wao kila siku watusaidie matatizo yetu?? Yaani umatonya tuu umetufanya mpaka tumekuwa masikini wakufikiri.Mtu mwenye busara ni yule anayejifunza kuvua samaki mwenyewe na sio kila siku kusubiri nchi kavu.
   
 3. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2009
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Pinda naye ameprove failure,haiwezekani wala haingii akilini kwa mtu mzima kama yeye kufikir kuwa tutaendelea kwa misaada ya nje na wafadhili,kufikiri hivyo ni uvivu wa kufikiri.Maendeleo ya kweli yataletwa na Watanzania wenyewe na si mataifa ya nje.Umefika wakati sasa wa sisi kufikiri kama taifa na kuachana na mawazo mufilisi kama ya PINDA.Ukombozi wetu upo mikononi mwetu,,,,,inawezekana timiza wajibu wako............
   
Loading...