Pinda anavyofuta nyayo za CHADEMA Kagera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda anavyofuta nyayo za CHADEMA Kagera

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwana wa mtu, Mar 5, 2011.

 1. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  05 Machi, 2011
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  WAZIRI MKUU AONYA KUHUSU UCHAFUZI WA AMANI
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewaonya wakazi wa Manispaa ya Bukoba na Watanzania wote kwa ujumla kuacha kuchezea hali ya amani ambayo imekuwepo kwa muda mrefu hapa nchini.

  Ametoa onyo hilo jana jioni (Ijumaa, Machi 4, 2011), wakati akijibu risala ya Wazee wa Manispaa hiyo ambao waliwaomba Watanzania wote waitunze amani na wasikubali kudanganywa na kauli za uchochezi zenye lengo la kuwatia hofu na kuwakatisha tamaa.

  Akizungumza na maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Bukoba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mayunga (Uhuru Platform), Waziri Mkuu alisema: “Wana-Kagera mnajua maana ya vita kwa sababu mmepata rasharasha mwaka 1972 wakati Idd Amin aliposema anataka aje kunywa chai Mwanza lakini ninyi pia ni mashahidi wa vita halisi ya mwaka 1978,” alisema.

  “Hivi majuzi tumepata matatizo kule Gongo la Mboto, wakati watu wanakimbia kuokoa maisha yao, wako wengine waaliokuwa wakikimbilia kwenye nyumba za wenzao ili kuiba mali zilizoachwa. Ni ajabu iliyoje kumsikia mtu akitamka: Bora vurugu bwana!” alishangaa.

  Alisema kama kamwe wananchi wasikubali uchochezi huo kwani maandamano na vurugu siyo suluhisho na amani ikishapotea kuirudisha ni gharama kubwa mno.

  “Kila kukicha, kuna watu wanazua madai ya kila aina, mara kura zimeibiwa, mara Katiba mpya; walichoamua ni kutembea nchi nzima … pengine hawana kazi za kufanya ndiyo maana wanatembea kuitisha maandamano huku na kule,” alisema.

  Alisema: “Kama suala ni kuing’oa CCM madarakani ni laima wajiulize maswali ya msingi ni vipi wataweza kuindoa CCM katika matawi, mashina, kwenye kata na tena mjijengee uhalali kwa wananchi hadi wawakubali.”

  “Msipofanya hivyo, mtatembea weee lakini CCM haingoki ngo!,” alionya na kuongeza kwamba: “Uongozi unategemea wananchi wanavyotutazama… wanatupima, je watu hawa wataweza kutusaidia? Je watajali shida zetu?” alitahadharisha.


  Mapema, katika risala yao iliyosomwa na Mzee Haruna Almasi, wazee hao waliomba kupatiwa matibabu bila mlolongo mrefu ili wasihangaike. “Tunaomba Serikali ituwekee utaratibu mwepesi wa kuwasaidia wazee kupata tiba…”, alisema Mzee Almasi.

  Wazee hao ambao walisema wanaiunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa Februari 28, 2011 wakati akilihutubia Taifa, pia waliomba kuwe na uwakilishi wa wazee katika ngazi mbalimbali za vikao vya kufanya maamuzi kuanzia kwenye Serikali za Mitaa hadi Bungeni.

  Kesho (Jumapili, Machi 6, 2011), Waziri Mkuu atakuwa wilayani Chato ambako anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo na kufungua SACCOS ya Mshikamano kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye shule ya msingi ya Chato.

  (mwisho)

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAMOSI, MACHI 05, 2011.

  Hii taarifa tumeinasa imetumwa kwenye vyombo vya habari mchana huu....tujadiliane Wakuu!
   
 2. Supervisor

  Supervisor JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 553
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Marekebisho kidogo hapo kwenye 'maelfu' ya watu inatakiwa iwe mamia tafadhali kabla haijasomwa
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ukisikia kutapatapa ndo huku. Alikuwa wapi kwenda kufanya ziara Bukoba hadi aone moto wa CHADEMA ndo aende? Haya atueleze akitoka Kagera anaenda wapi??? Lakini sio kosa lake ametumwa na mkwere, maana sasa ni kujibu mapigo ya chadema kila kona, huku wasira, kule chiligati, pale Sofia simba, nyuma Pinda, na wasaidizi wao Cheyo, Mrema kwa pembeni, Kafulila akiuma na kupuliza, then sasa hivi CCM B (CUF) watajibu nao. Wote hawa ni wapinzani wa CHADEMA. Aisee kweli PEOPLE HAVE POWER LOH!!!!!
   
 4. l

  lwangwa Member

  #4
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pinda hana jipya tumemuzoea ni kama mtu anayepiga jalamba ,uwezo wake mdogo ,kila kukicha amekuwa akiapa kufanya mazuri lakini ndiye anayeongoza mafisadi kuwa tetea hatumsikilizi sisi tuko tayari kufa anaongea na hao wazee vikongwe uwezo wao wakufikiri umekwisha kwanini asiongee na vijana wampe vipande vyake ache hizo hana lolote .
  Pinda achukue tahadhari kauli zake zitamgharimu asije akashusha heshima yakle mbele ya jamii amesahau ya juzi kuongea uongo mbele ya bunge pinda hanakitu cha kujifunza kuhusu kauli zake chi hii siyo ya ccm wa la chadema chedama inafanya yale wanayo yataka wenye nchi wananchi kama ccm inaomba msaada wa dola basi pinda na ccm yake wasome histori ya ufarasa jeshi lilipo amua kuuweka chini silaha na kuungana na waandamaji kudai mkate ,pinda anasahau kuwa watumishi wa dola pia wana ndugu zao wanaoteseka na maisha ,anasahau histori ya vita kuu ya duni a adolf hitler alitakia kuuwawa na mmoja wa askari wake sasa pinda sijipeleke kimbelembele chadema imekubalika kwa wananchi hata uite majini yata kwaya pole pinda pole sana tena pole .
   
 5. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  watu wanalala njaa we wasema amani hipo Tanzania. Maisha taiti wasema amani hipo.Bidhaa zinapanda msharaha chini . Mzee zama za kutisha watu zimekwisha .
   
 6. Lugovoy

  Lugovoy JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kazi anayo,panapofuka moshi dawa yake ni kuzima moto chini,anapoteza muda sharti ajibu hoja za msingi na sio kuwatia hofu wananchi.
   
 7. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Pinda alianza ziara yake Kagera kwa kupewa mipasho; mradi pekee aliofungua katika Munincipali ya Bukoba hiyo jana ni barabara ya mita zipatazo 25 hivi (nasisitiza neno mita wala siyo kilomita), iliyojengwa kwa changalawe zilizomiminiwa lami nyepesi maarufu kwa jina la otta seal. Kwa wadadisi wa mambo, kitendo cha waziri mkuu kushiriki katika ufunguzi wa mradi mdoga wa aina hiyo, ni ishara tosha inayo thibitisha ni kwa kiwango gani serikali imeutelekeza mji huo, na mkoa kwa ujumla.
   
 8. b

  banyimwa Senior Member

  #8
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Je, njaa hizo zitaondolewa kwa maandamano? Mimi nauliza tu wajameni!
   
 9. e

  emalau JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  The same old song amani!! amani ipi anayosema au kwa sababu hatupigani ndo anasema tuna amani? Watu hatuna umeme, kazi zetu hazifanyiki maofisini na kwa maana hiyo familia zetu zimekosa vipato na kwa undani zaidi serikali anayoiongoza kupitia TRA inakosa mapato kwa kuwa hakuna uzalishaji, je hiyo ni amani anayoongelea?

  CCM should stop singing the same old song they should reinvent themselves by putting new strategies in place otherwise smear tactics didn't work before election and they not gonna work after election.
   
 10. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hana lolote huyu kijakazi wa mafisadi papa
   
 11. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ha! ha! ha! kwaani umesahau kuwa mtu siyo lazima abebe makopo na takataka ili aitwe punguani. Hizo ni dalili za mfa maji mkuu. Katika picha hii ni kionjesho, bado picha halisi yaja mkuu. Pepleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,S
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  muulize pinda kama ataondoa njaa kwa maneno mkuu!
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Haya mambo (kulala na njaa na maisha taiti) hawa wachonga mbuyu nao wanayapata? Nafikiri ingekuwa jambo la busara kwa wao kupita hizo sehemu wakifanya mema yalioshindwa na Serikali. Ni juzi tu tuliwasikia hapa kuwa wanakatazwa kusema kiasi kisichoendana na hali halisi ya mapato ya Tanzania wanacholipwa kule bungeni na hiyo serikali (ya CCM) wanayopita kuipinga.

  Hawa (wanasiasa kwa ujumla wao) ni wakaanga mbuyu tu, kwani wale waliokufa Arusha ni hao wakombozi?
   
 14. s

  smz JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wabunge makini wa CDM walisema kwamba wana pewa sh mil90 kila mbunge kwa ajili ya gari. Na wakasema hadharani kuwa pesa ile ni nyingi mno.

  Siku zote mafanikio yanaanza na moja. CDM wameonyesha njia, wenye nia ya kweli wawaunge mkono na kuwapa mbinu shirikishi. Lakini siyo TLP wala UDP. Hawa wameshafirisika kisiasa.

  Yako wapi Mapesa aliyotaka kutujaza mzee Cheyo?? Au ulikuwa usanii. Kageuka kuwa mpambe wa ccm hadi anatukana wabunge wenzake, amba sisi tunawaamini kuwa ni makini kuliko yeye.

  Angekuwa yeye katukanwa haraka angeomba Muongozo wa spika, lakini Lissu alimpuuza kwa kujua mzee kesha jiishia.
   
 15. Laface77

  Laface77 JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2011
  Joined: Jul 9, 2008
  Messages: 1,301
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Ole wake Pinda kwa kukubali kuendelea kutumika na hawa mafisadi,wenzake wana uraia wa zaidi ya nchi moja pamoja na fedha nyingi tu katika nchi za nje hivyo ni rahisi kukimbia, je yeye mtoto wa mkulima atakimbilia Rukwa?Nguvu ya uma itamfuata tu.
   
 16. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kaaaaaaaaaaazi kweli kweli hawa jamaa wamechanganyikiwa kila kukicha ni maneno dhidi ya UKWELI, ukweli hauwezi kufunikwa kwa maneno ya jukwaani au hizi taarifa za ofisi ya PM. Siku zote wanapaswa kuukabili ukweli, Hakuna Umeme waje na umeme, Mishara midogo wao posho mlima waje na kupunguza yao na kuongeza wale wa ngazi za chini, Mfumuko wa bei jibu ni kuudhibiti siyo kupiga blah blah tu serikali nzima imekuwa kama ni akina Tambwe na Mjinga mwenzie Makamba. Sisiem badilikeni nchi imewashinda irudisheni kwa wananchi wenye nchi.
   
 17. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  picha za watu waliomsikiliza pinda ni muhimu
   
Loading...