Pinda akiri mazungumzo na CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda akiri mazungumzo na CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 11, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h]

  Na Godfrey Ismaely

  Dodoma

  WAZIRI Mkuu Bw. Mizengo Pinda amekiri kuwapo mazungumzo baina ya ofisi yake na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu mgogoro wa umeya Arusha kutokana na madai kuwa uchaguzi wa kujaza kiti hicho ulikiuka sheria.


  Kukiri kwa Bw. Pinda kunatokana na tamko la Kamati Kuu ya Chadema lililopokea na kutambua mazungumzoa yaliyofanywa na Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe na Bw. Pinda na hatua waliyofikia ya kuunda kamati chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa kushughulikia suala hilo.

  Akizungumza na Majira mjini Dodoma jana, Bw. Pinda alisema, “Ni kweli hivi karibuni nilikutana na mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe akiwa ameandamana na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa hapa Dodoma, kikubwa ambacho niliweza kuwashauri ama kutoa maoni yangu baada ya wao kunieleza kwamba dhamira ilikuwa ni kuleta maridhiano ya amani katika jiji hilo, niliwaunganisha na msajili wa vyama vya siasa Bw. John Tendwa ili kuharakisha mchakato huo.

  “Kwa kuwa Bw. Tendwa ndiye anayehusika na vyama vya siasa na ofisi yake ipo chini ya ofisi yangu hivyo ninaamini kwamba baada ya muda watatueleza walipofikia kwa matumaini kwamba mambo yatakwenda vizuri,” aliongeza.

  Kauli hilo ya Bw. Pinda ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inakuja wakati chama hicho 'kimeshanawa' mikono kikisema hakina mgogoro na CHADEMA mkoani Arusha huku kikisisitiza kuwa uchaguzi wa meya mkoani humo ulishamalizika na ulifuata sheria na kanuni zote.

  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye alilieleza gazeti hili juzi akisema kama kungekuwa na mgogoro huo ofisi ya msajili inayoshughulikia vyama vya siasa ingewaandishi barua kuwafahamisha suala hilo, jambo ambalo halijafanyika.

  Wabunge kughushi sahihi yake

  Akizungumzia juu ya wabunge kughushi sahihi yake kwa kuandikiana vikaratasi vya kuwadanganya wenzao kwamba anawahitaji, Bw. Pinda alisema kuwa hilo siyo jambo jema kuendelezwa na watu ambao wamepewa dhamana na wananchi, badala yake wanapaswa kubadilika mara moja.

  “Bunge hili lina mambo ya utani sana, wakati mwingine wanaweza kukuchora kikatuni na kukuwekea kwenye kibahasha wanakutumia, ukifungua ndani unashangaa sana, lakini mara baada ya lile tamko la Mwenyekiti wa Bunge hawakuendelea tena, jambo la msingi ni kwamba hawapaswi kufanya mambo ya mzaha ndani ya bunge, na wala hawapaswi kuendeleza tabia hiyo kwani wakati mwingine wanawapotezea wenzao fursa ya kufuatilia kwa umakini mijadala inayoendelea bungeni,” alisema Bw. Pinda.

  Akosoa maswali ya papo kwa papo

  “Hiki ni kipindi kizuri sana ambacho kikanuni kimelenga kumpa mwananchi nafasi kujua mambo yanayoendelea serikalini, na ni kweli mfumo huu tumeiga kwa kiasi kutoka Uingereza kwa dhamira nzuri tu ya kuwajulisha kikamilifu wananchi masuala mbalimbali tatizo linatokea pale ambapo muulizwa maswali ambaye ni waziri mkuu, ahandaliwi kwa kufahamishwa ni swali gani atakumbana nalo kwa siku, bali mbunge yeyote tu anaweza kuuliza swali,” alisema Bw. Pinda.

  “Lakini ninaamini mwanzo huu ni mzuri na siku moja wakubwa wakifikia mahali wataamua kukifanyia maboresho kipindi hicho, ili maswali yaweze kumfikia waziri mkuu ndani ya masaa 24 kabla ya kuyajibu, kwa lengo la kuleta ufanisi zaidi, kwa kuwa yanahitaji ufanisi mkubwa na utaalamu wa kutosha katika kuyatolea majibu kikamilifu,”
  aliongeza.
   
Loading...