Hamjambo waungwana wa JF?.
Nipo hapa BoT Jijini Mwanza nikifuatilia kikao cha Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda na viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo kuhusu nani mwenye mantiki ya KUCHINJA wanyama.
Ameingia ukumbini majira ya saa 6:10 mchana, akiwa na msururu mrefu wa magari ya Serikali kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa kiroho. Yap, baada ya kuingia ukumbini, Pinda aliruhusu waandishi wa habari kuzama ndani ya ukumbi then akatoa maelezo mafupi ya pole kuhusu mapigano ya kidini yaliyotokea Buseresere Geita na mtafaruku uliopo Nyehunge Sengerema.
Cha ajabu, baada ya hapo Pinda alijipinda kutoa maagizo waandishi wa habari waondoke ukumbini ili atete vizuri na Masheikh na Maaskofu. Wakiwa nje ya ukumbi waandishi, ofisa mmoja wa Usalama wa Taifa aliwafuata akitaka waende nje kabisa ya geti....lakini wakamdindia kwa kukataa kwenda nje na akawaacha.