Pinda ahutubia umati KARATU

Pinda ahutubia umati KARATU

John Akonaay

Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
65
Reaction score
10
Pinda yuko na mkutano wa hadhara hapa Karatu mchana huu ktk viwanja vya mazingira bora hapa Karatu.
 
Pinda yuko na mkutano wa hadhara hapa karatu mchana huu ktk viwanja vya mazingira bora hapa karatu

Weka Picha,asije akawa anaongea na watu watano unaita mkutano wa hadhara badala ya kikao....!
 
mwambie aondoke haraka niko hapa makao ngorongoro ole nimkute hapo lazima apigwe eh maana tumechoka....
 
sasa Nyalandu anaisifia karatu kuwa ni mji mdogo wenye hoteli nyingi za kitalii. Anasema mji wa karatu unakuwa kwa kasi. Anahimiza vijana wajifunze kichina, upishi na tour guide. Anasema karatu inajitahidi kupambana na ujangili.
 
sasa anapanda jukwaani kassimu Majaliwa. Anasema karatu imeongoza kwa idadi ya watu waliokuja kumpokea pinda. Anasema kitaaluma karatu imepitiliza lengo la serikali. Anasema mpaka kufikia mwenzi wa 11 tatizo la elimu litakuwa historia. Anatamka banjuki badals ya banjika.....anasema vitabu vingi vitasambazwa shule zote sasa hivi vipo kwa mkurugenzi. Anasema serikali imetenga bilioni 17 za madawati. Milion 486 zimetengwa kwa ajili ya shule mbili. Milioni 50 za ukarabati wa karatu high school zimeshatolewa. Anasema Ayalabe itabaki kuwa shule ya msingi haitafanywa chuo. Anahimiza wazazi kufuatilia mwenendo wa watoto wao wanaporudi kutoka shule...amemaliza
 
sasa Nyalandu anaisifia karatu kuwa ni mji mdogo wenye hoteli nyingi za kitalii. Anasema mji wa karatu unakuwa kwa kasi. Anahimiza vijana wajifunze kichina, upishi na tour guide. Anasema karatu inajitahidi kupambana na ujangili.

Anaongea na nani?.....!
 
Ndio RAHA ya kuchagua WAPINZANI, kila mara viongozi wa juu watawatembelea, kijimradi kidogo kinakuja kuzinduliwa na kiongozi mkubwa wa serikali. Badala ya wananchi kujikomba kwa viongozi, viongozi wanawanyenyekea wananchi. Viongozi wa sehemu hiyo wa CCM wakiwa wajanja miradi mingi inaelekezwa kwao, kwani wataomba iwe hivyo ili jimbo au kata ikombolewe. Maendeleo ya sehemu husika yanahitaji ujanja wa viongozi wa kisiasa.
 
ole sendeka anapanda jukwaani....anaanza kwa utani kidogo. Anawapongeza karatu kwa maendeleo ya kila sekta apa anaquote vitabu vitakatifu. Pia anawapongeza watu wa karatu kwa uelewa kwa vile hawajawahi aandamana. Anasema kazi ya mbunge ni kuwa kipaza sauti cha wananchi....anaingiza utani kwa CDM. Sasa anaongelea katiba mpya anasema hataki ushabiki hata wa CCM kwenye katiba mpya..
anadai sheria ya mabadiliko ya katiba imefanyiwa marekebisho kidogo hivyo anashangaa kwa nini wapinzani waliipinga.
 
Mama Tunu yupo jukwaani...anatoa salamu kwa furaha. Anasema karatu imevunja rekodi kwa mwitikio wa watu.
 
So called mtoto wa mkulima anapanda jukwaan...mkuu wa wilaya anampa zawadi i.e kondoo, ndama, kinyago cha faru, mgorori....zawadi nyingi sana magunia ya vitunguu, mbaazi,....anasema karatu hoyeeee mikono kuu, kikwete juu. Anasema haijapata kutokea. anamkaribisha Natse jukwaani Natse anaanza na peopleees power...umati unaitikia kwa furaha....mkutano unafurahisha. Pinda z playng fair.
 
hapa naona porojo tu hakuna cha maana , ni dhahiri hawana chakufanya fikiri vema kabla haujaweka kitu
 
Back
Top Bottom