Pinda acha kutudhihaki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda acha kutudhihaki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bornvilla, Mar 10, 2011.

 1. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 921
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mh.Pinda huku ni kutudhihaki Watanzania.Eti unashangaa watu kujenga nyumba za nyasi Ngara! Umetembea nchi nzima na kuona? Hujaona nyumba za tembe zilivyo zagaa Shinyanga,Tabora,Singida na Dodoma? Maisha yetu magumu sana wakati ninyi mnajinufaisha! Pesa tu ya mlo wa kilasiku kwetu ni mbinde,simenti na bati tutaviweza? Tujengeeni nyumba kisha mtupe bure,kwani pesa kiasi gani zinapotea? Nasi twataka kuifaidi nchi yetu wala sio wachache.Wengine mnaishi peponi bwana wakati sisi tupo kwenye mateso.Usishangae kwani Mh.wewe hujui?
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,233
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Aliyeshiba hamjui mwenye njaa!...kaka umesahau hilo?
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,826
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Huyu mnafiki sana, kwao Sumbawanga wako nyuma saaana nyumba za nyasi ndo zimejaa huko leo eti anajifanya anashangaa PINDAAAAAAAA nilikuamini sana mwanzoni lkn sasa hivi nakuona kama joka la kibisa huna loloteeeeeee
   
 4. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Anashangaa nini huyo Pinda? anajifanya anawaonea huruma wananchi wakati yeye yu-pamoja na Mafisadi!

  Anataka maendeleo wakati anatumika kumzuia Magufuli kufanya kazi yake? Je, sheria inasema nini juu ya hifadhi ya barabara? ni umbali gani toka hifadhi ya barabara unatakiwa uwe kabla ya kukuta majengo? Kama hawezi kuheshimu hifadhi ya barabara ataweza kuheshimu makazi ya raia huko Ngara? Huyo ni mnafiki na hafai kabisa. Sote twatambua anatumika kumchafua Magufuli!

  Kama anauchungu na raia wa nchi hii kuishi nyumba za nyasi/udongo, kwanini serikali yake isifute kodi kwenye bidhaa za ujenzi ili bati na simenti viuzwe Tsh. 5,000?=@?
   
 5. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Anatung'ong'a huyu. Kwani ndo mara yake ya kwanza kwenda vijijini? au anaigiza? Kama waziri mkuu, anatakiwa awe na takwimu kuwa ni wananchi wangapi wanaishi kwenye nyumba bora na wasioishi katika nyumba bora wanakwamishwa na nini na suluhisho lake ni lipi na serikali inakwama wapi kuwasaidia. Taasisi za tafiti zipo nyingi sana, asilete usanii katika mambo ya msingi.
   
 6. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo ndiyo Pinda,sura yake halisi tunaiona,ni mnafiki.Anashangaa ngara,wakati kwao mpaka mjini zipo,
   
 7. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Wale waliombatiza Pinda kama "mtoto wa mkulima" mimi sikukubali. Yeye ni "kibaraka wa mafisadi". Ndio maana anajifanya kushangaa umaskini uliokithiri kijijini. kazi kubwa ya Waziri Mkuu ni kufuatilia utekelezaji na sio kushangaa! CDM walishasema wangeingia madarakani, wangepunguza bei ya simenti na bati ili wananchi wajenge nyumba bora kama walivyofanya Rwanda. Lakini JK na Pinda wake waliponda sera hiyo. Sasa anashangaa nini? Hawa watu wanaudhi kwelikweli. Tunahitaji mabadiliko hata kabla ya 2015.
   
 8. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kweli jamaa nae yupo kwa maslahi ya wakubwa wake hana jipya la kuwaambia wadanganyika ni mnafiki mkubwa.

  kwa namna nyingine amewatukana hata waliompa kura kwao alikotoka sijui wote kawajengea nyumba.
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,105
  Likes Received: 523
  Trophy Points: 280
  nimetoka kwao pinda kule kijijini yaani kumechoka sana.....namshangaa kwa kauli kama hizo za kipuuzi kabisa
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,712
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Huyu mzee mafisadi wameisha corrupt akili yake
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,712
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Aliyeshiba hamuoni mwenye njaa, huyu mzee hayo maneno yake ni kama vile punguwani anaongea namshangaa sana
   
 12. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 425
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Msimlaumu may be he was expecting a difference kulinganisha na kwao Sumbawanga na jinsi anavyowajua watu wa Bukoba kuwa ni wachapakazi.
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 38,465
  Likes Received: 3,350
  Trophy Points: 280
  Yaani hata mimi namshangaa huyu ndugu yetu sijui kapatwa na nini!!
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 38,465
  Likes Received: 3,350
  Trophy Points: 280
  Hata Sumbawanga ni wachapakazi....
   
 15. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,055
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwa lipi kama mazao yao hayana soko la kuaminika?!?
   
 16. M

  MASOKO Senior Member

  #16
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Pinda tusije tukakupiga mawe tafadhali
   
 17. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,841
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  aaaah ntarudi bdae kumbe anazungumziwa stage shoo wa sharobaro
   
 18. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 8,515
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Siku hizi hakuna cha uchapa kazi ni ufusadi mbele kwa mbele. Huoni hata wachaga wameshindwa kujenga migombani kama zamani??

  Huyu jamaa kweli anadhihaki watu, inamaana hata zile tembe za Dodoma hajaziona au alifikiri kagera siyo TZ.
   
 19. N

  Nanu JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  PM yuko sawa. Anakubaliana sasa na hoja ya Dr. Slaa kuwa watu hawana makazi bora na wanahitaji makazi bora. Hivyo maisha yao yaboreshwe na vifaa vya ujenzi vishushwe bei. Yeye ni mmojawapo katika kambi ile ya kusema kuwa haiwezekani kushusha bei ya saruji na bati lakini kwa sasa wanapiga debe sukari ishushwe. Kwanini pia wasipige kelele saruji na bati zishuke bei?
  Kwa watu makini maana yake PM Pinda anaunga mkono sera ya Chadema pamoja na Dr. Slaa.
  Hii ni pointi mojawapo ya Chadema kutumia wakati wa mikutano ya hadhara yajayo na kudhirisha kuwa serikali inayowaongoza wanashangaa kuwa wanaishi kwenye tembe na nyumba za nyasi kwamba hawajui kuwa watu wao ni maskini kiasi gani!!!! Ndiyo Wanashangaa sasa!!!! Yaani kweli CCM wakati mwingine ni viini macho.
   
 20. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,574
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Karimoti Ka Wachache...Nyoka Wa Kibisa:decision:
   
Loading...