Pilipili ni uchungu pekee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pilipili ni uchungu pekee

Discussion in 'JF Doctor' started by Jayfour_King, Jan 4, 2010.

 1. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wana JF,
  Nimekuwa nikila pilipili kwa mazoea muda mrefu umepita bila kufahamu mbali na hiyo ladha kali iliyonayo, ina kazi nyingine mwilini kitaalamu? Naomba wadau wenye upeo na hili wanijuze nipate kuelewa.
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Pilipili ni vegetable. Mbali na kuwa na vitamins na madini kama vegetables nyingine, pilipili inaongeza apetite ya kula pamoja na kusaidia katika digestion. Huko nyuma kabla ya ugunduzi wa refrigiration pilipili ilikuwa mojawapo ya viungo vya kutunza vyakula (preservatives). Wataalamu zaidi wataongezea manufaa mengine.
   
 3. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Pilipili huwa inastimulate hamu ya kula, ni appetizer
   
 4. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Nilisoma sehemu kwamba pilipili pia husaidia kuchachawisha (stimulate) mishipa ya damu. Je ni ipi namna ya ulaji sahihi ambayo inakuwezesha kupata manufaa hayo, kwa kuitafuna na kuimeza au pia ukiimeza nzimanzima afu ikaenda kusagwa kwenye mfumo wa umeng'enyaji chakula wa ndani ya tumbo?
   
 5. Shark's Style

  Shark's Style JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 207
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Pia inakufanya uwe Hot sexual So inawza kuwa Dawa kwa watu wenye matatizo ya kukosa hamu ya kufanya mapenzi.
   
 6. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Dah kuna siku nilialikwa chakula na rafiki angu mhindi hehe hehe nilijuuuta kula kwa watu shughuli yake chooni acheni tuuu
   
 7. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hehehehe! Mwana Ukome hiyo inaitwa hahahah! hao jamaa kwa pilipili noma!pole MR!
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,611
  Likes Received: 82,194
  Trophy Points: 280
  Inadaiwa pia ni kiungo kizuri sana katika kuzuia magonjwa mbali mbali ya binadamu ikiwemo cancer na pia huongeza libido.

  YouTube - Ayindjo
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,611
  Likes Received: 82,194
  Trophy Points: 280
  Hahahahahaha si ungeahirisha tu kwenda kwenye shughuli za kule mahali hadi tumbo litulie LOL! MR, inaelekea tumbo lako limechakachuliwa LOL! Vinginevyo hutakiwi kusikia chochote kama tumbo lako liko bomba.
   
 10. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Yani acha tu nimekomaaa Wahindi kwa pilipili nawanyooshea mikono!!!
   
 11. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Yani i wish ningeweza ahirisha yaliyonikuta we nipe pole tuuu tumbo langu halijazoea mikiki mikiki!!! ila cha moto nilikiona mwanaa khaaa!!
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,611
  Likes Received: 82,194
  Trophy Points: 280
  Pole sana, siku nyingine akikualika mwambie akupikie chako pembeni bila mapilipili LOL!
   
 13. c

  chetuntu R I P

  #13
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pilipili ina vitamin C, A na inatakiwa iliwe ikiwa mbichi au pasturized.
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Pili pili zina faida nyingi kwa afya baadhi ni

  1. Capsaicin ni kemikali inayo patikana kwenye pili pili, hii ndo husababisha muwasho.Capsaicin imethibitishwa inaweza kuuwa kuuwa vimelea vya kansa ya kibofu (prostate cancer cells)
  2. Pili pili husaidia kupunguza uzito, ukiweka nyingi kwenye msosi basi hata ulaji wa chakula hupungua maana itakubidi uwe unawahi maji mengi.Hivi karibuni kuna jarida limeandika pili pili huweza kupunguza hamu ya kula (appetite suppressant)
  3. Husaidia kuyeyushwa kwa chakula kwenye mfumo wa chakula (GIT)
  4. Capsaicin husaidia kuponya vidonda vya tumbo, tofauti na watu wengi wanahisi pili pili hukuza vidonda vya tumbo
  5. Pili pili hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo kama (Blood pressure), capsaicin inafahamika kwa kupunguza cholesterol
  6. Pili pili husaidia kusafisha matumbo ya kwenye mfumo wa chakula (Colon Cleanser)
  7. Kuna vitamini nyingi kwa pili pili, Vit P, K, C na A, huleta joto mwilini na kuongeza hamu ya kufanya mapenzi.
  Pili pili iliyo nzuri ni ile kali sana, Ukienda Malawi wana pili pili sauce inaitwa Nali Hot Peri-Piri ni kali sana wameandika kabisa itumike kwa watu walio na miaka 18

  [​IMG]

  Kwa sasa naweza agiza sauce kali kabisa amazon inaitwa Ultimate insanity hii inasemekana ni hottest sauce on universe

  [​IMG]

  Haya wapendwa tumieni pili pili kwa wingi kwa afya bora

  Sharing is Sexy

  Rev Masa K


   
 15. c

  chetuntu R I P

  #15
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Thanx Rev kwa ufafanuzi.
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Gonga thanks hapo juu basi!
   
 17. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  pilipili husaidia kuifanya damu kuwa nyepesi yaani majimaji na hii ndiyo ambayo hutoa ahueni kwa wagonjwa wa moyo wenye tatizo la kuwa au kuziba kwa mishipa inayoingiza damu na kutoa damu katika moyo hiyo ndiyo inayosabababisha moyo kuwa mkubwa kama mshipa wa kutolea damu umeziba inamaana damu inayoingia ni nyingi kuliko inayotoka hivyo husababisha moyo kuwa mkubwa na kama mshipa wa kuingizia damu ndio umeziba au kuwa mdogo inatengeneza pressure kubwa na hiyo ndiyo inayoleta maumivu ya moyo na kuwa na kitu wanaita bp hapo pili pili ikisaidia damu kuwa nyepesi au majimaji inamaana itawezesha damu kupita kwenye mirija iliyoziba ua kubana kwa urahisi na hivyo kumpunguzia mgonjwa maumivi kwasababu itapunguza ile pressure inayotengenezwa na ile sehemu iliyobana.

  kumbuka matatizo ya moyo kuwa mkubwa au kubana kwa mirija ya kutoa na kuingiza damu kwenye moyo linawezakuwa ni tatizo mtu alilolozaliwa nalo au linaweza kumpata mtu kutokana na mtindo wa maisha kama ulaji wa vyakula vyenye mafuta hivyo mafuta kuziba kwenye mishipa hiyo.

  watu wengi wanaeeleza zaidi kuwa matatatizo mengi ya moyo ni ya kuzaliwa lakini wanasahau pia kuwa mtindo wa maisha ya wazazi yanaweza kupelekea kupata matatizo ya moyo kwa mtoto mdogo kuna wazazi wanakunywa pombe kwa mfano na wana tabia ya kuwanywesha watoto wadogo pombe kabla hawajakomaa kumbuka kwamba mwili wa mtoto mdogo ni mdhaifu na kama unampa pombe basi huenda kuathiri mfumo wa moyo hivyo kupata watoto wadogo wako na tatizo la moyo na wengi wanafikiri kwamba walizaliwa nayo wazazi wenye watoto kama hao wengi utawasikia wakisema watoto wao wana matatizo yaa moyo na kwamba walizaliwa hivyo.

  hii ni kwa ujibu wa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ambaye alifanya utafiti baada ya kuwa daktari katika hospitali moja kubwa na kushuhudia tatizo ambalo aliliona liko zaidi kwa watu wa kabila fulani, na kwenye utafiti wake aligundua kuwa watu wa kabila hilo ni wanywaji wa ile kitu inatwa ....... na hupenda sana kuwanywesha watoto wao na baadae watoto wao hupata tatizo la moiyo either ukubwana au katika umri mdogo.
  katika utafiti wake Dk huyo bigwa wa magonjwa ya moyo amefafanua zaidi kuwa watu wa kabila hilo huwa wanafanya pombe kama chakula na hata mara nyingi utakuta imekuwa ikitumiwa na wazazi kama kuwanyamazisha watoto na kuwafanya wapate usingi ili wazazi hao waweze kuendelea na shughuli zao. hapo ndipo tatizo linapoanzazi.
  hivyo kama mzazi ndugu na jamaa jaribu kutokuwapa watoto wadogo pombe kwani ni mbaya sana kiafya na haswa katika tatizo hili ya moyo ambapo tumeshuhudia ongezeko la watoto wadogo kupatwa na magonjwa ya moyo
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Kumbe ina faida namna hii.
   
Loading...