Pilau la njegere

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,463
Reaction score
65,772
Hello

Leo bhna tupike pamoja pilau la njegere

Kwanza niliandaa vitu vyangu mapema kabisa
Nikaanza na kuweka mafuta kwenye sufuria baada ya hapo nikaweka kitunguu swahumu

Baada ya hapo nikaweka nyama iliochemshwa nikaweka

Kisha nikaweka kiungo cha pilau

Nikachanganya ipasavyo kisha nikaweka viazi na kitunguu maji
Navyo kikavikaanga kwa muda kisha nikaweka karoti

Baada ya hapo navyo nikachanga kuikaanga karoti nikaweka nyanya nyanya kwenye pilau inaleta radha mzuri pia rangi ya chakula kinakuwa pia nzuri

Nyanya haitakiwi kuiva sana nikaweka mchele mchele usioshe mwanzo osha baada ya kuanza kupika kuna wengine wanaosha mchele kabla ata kuandaa mahitaji inapelekea mchele kukatika

Baada ya hapo nikaweka supu ya nyama unaweza tumia maji ya kawaida ila mimi napenda kutumia supu


Basi baada ya hapo nikafunika kuacha maji kauke ili niweke njegere baada ya kuona maji yamekauka nikaweka njegere

Kisha nikafunika epuka kukologa kologa kuna watu wakipika watakologa kologa mpaka pilau linaonekana umetumia mchele wa chenga na kusingizia mchele mbaya la usikoroge basi baada ya muda nikafunua ili kuzichanganya

Na nilipoona zimeiva vizuri nikaipua baada ya kuzichanganya niliziacha jikoni kwa muda

Mnakaribishwa wotee nikatengeneza na kachumbari yangu hiyo

Karibuni kwetu
 
View nzuri sana😍
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…