Weekend iliyopita Simba ilikuwa Dodoma kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Polisi ya Dodoma kama sehemu ya kujiweka sawa na maandalizi ya michezo yao mbalimbali ikiwemo Kombe la FA watakalocheza weekend hii Arusha dhidi ya Madini FC.
Simba wakiwa Dodoma moja kati ya vitu vilivyovutia ni picha ya shabiki mtoto wa Simba ambaye aliamua kuonesha mapenzi yake kwa staa wa Simba Ibrahim Ajibu kwa kuandika jina na namba ya jezi ya mchezaji huyo katika t-shirt yake kwa pen, kitendo ambacho kilifanya wengi wampongeze.
Baada ya hapo Simba kupitia ukurasa wao wa instagram waliomba kuwa mtu anayemfahamu mtoto na wazazi wake wawajulishe, leo March 14 baada ya Simba kumpata imeripotiwa kuwa mtoto huyo anatumiwa jezi original ya Ibrahim Ajibu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.