Madai
Kumekuwapo na taarifa iliyochapishwa
Facebook kuwa Iran ilishambulia ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwa kutumia ndege zisizo na rubani (drones), na kuonesha picha ya moto mkubwa kwenye majengo kadhaa.
Uhalisia
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia nyenzo za kidigitali utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umebaini picha hiyo inahusiana na moto uliozuka Traun, Austria, siku ya Mwaka Mpya, Januari 1, 2026.
Moto huo
ulitokea katika jengo la makazi lililoko Guido Holzknecht-Straße, Traun. Watu takriban 70 waliokolewa, wanne walipata majeraha madogo.
Picha zinafanana na muonekano wa mitaa kwenye Google Maps na ripoti za vyombo vya habari vya Austria, ikiwa ni pamoja na Kronen Zeitung na Österreichischer Rundfunk.
Hakuna Ushahidi wa Shambulio la Iran, hakuna ripoti rasmi au vyanzo vya vyombo vya habari vinavyokubalika vinavyohusisha picha hiyo na shambulio lolote dhidi ya Netanyahu au ofisi za Israel.