picha ya mwisho wakichuma dawa

Sijaua madhara ya kuchimba dawa ni yepi?
Ni kuchafua mazingira? huo uchafu ni environment friendly
Kushambuliwa na wanyama wakali? si lazima kuchimba ktk mazingira hatarishi
Kulinda maadili kwa rika? Haja ikikushika haina adabu maadili unaweka kando
Kuna vyoo vimeandaliwa? ni vya kulipia? nani atavisafisha?kuongeza mzigo kwa msafiri
yameletwa mabasi yenye vyoo ndani? sijayaona
Ukichimba dawa utakamatwa? wanawekwa askari maporini?

Ubongo wangu una maswali na majibu haya, napata shida kuelewa. labda kwa vile Kayumba.

Wanasema TABIA HULETA MAZOEA, kuchimba dawa ni tabia ambayo ilishajengeka muda mrefu kwa wasafiri mwisho wa siku watu wakazoea na kufanya ni kanuni, kuchimba dawa kuna madhara haina ubishi hasa kiwango kikubwa cha kinyesi kinaposhushwa eneo moja kwani kama kuna chanzo cha maji karibu ni balaa lakini pia kuna kulinda maadili kwa rika kama ulivyouliza pia inafuta ile dhana ya MSAFIRI KAFIRI chochote unafanya bila aibu uwapo safarini. Kama wewe ni msafiri mzuri si kwamba hakuna vyoo, vyoo vipo kila sehemu gari linaposhusha abiria kula ila ili kuwahi madereva wakaleta huu utaratibu wa kuwachimbisha abiria dawa kwa kuwa unapokuwa porini suala la matundu ya choo halizingatiwi hivyo ndani ya dakika 5 biashara imeisha watu wanaendelea na safari (hivyo hakuna foleni porini). Vyoo vipo kama unakwenda Iringa hadi Mbeya ukifika pale Ruaha Mbuyuni (Aljazera hotel au Kitonga vyoo vipo vya kutosha tatizo ni dakika 10 tu zinatolewa kula na kuchima dawa), kama unakwenda Arusha pale Transit Hotel - Korogwe, Dar express ana hotel zake pia pale Liverpool Hotel - Mombo vyoo vipo, njia ya Dodoma to Mwanza pale Moro, hata Gairo kuna Hotel nzuri inavyoo japokuwa labda Singida wanatakiwa waboreshe huduma si nzuri. Maswali yako ni changamoto nzuri ya nini kifanyike na wala si Kayumba wewe ila all in all inabidi tukomeshe hii tabia kwani inajenga tabia mbaya kwa watoto kwamba anapoona kichaka tupo huru kujisaidia na mwiaho wa siku inakuwa ni tabia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom