Picha ya Dkt. Mauki na binti yake imekuwa na mjadala mkubwa FB

ERoni

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
43,670
90,153
Je, ni sawa au sio sawa?

Ni mkanganyiko wa tamaduni au tupo kwenye "right track"?

Toa maoni yako.

Samahani kama Dr. Mauki yupo huku na hatofurahia kuona picha yake huku.

FB_IMG_1536868650201.jpeg



Nyani Ngabu,

========
Michango:


I thought so.

Hii Video imenifadhaisha sana na najiuliza ni mauki huyu huyu au account yake imekuwa hacked.
Bonding si lazima ifanyike bafuni na kwa picha . Mimi binafsi kama mwanamke nikivaa viatu vya huyo mtoto , nisingependa kabisa baba yangu apost picha za mimi nikiwa na taulo . Imagine binti amekuwa mkubwa yupo na familia yake hii picha anaweza asiipende. Na ningekuwa mke wa mauki wala nisingeshiriki kuposti hii picha. Tukumbuke kitu unachoposti mtandaoni usikionee aibu hata kama mchungaji wako , au mzazi wako au rafiki yako akisoma unachoposti. Hebu leo mauki ajiulize, kwa post ile ana jisikiaje siku mwanae akiiona after 20 years, je atajisikiaje mchungaji wake akiitumia? Jamani kuna mipaka , hata Obama kwa kuwapenda sana mabinti zake hajawahi kuposti such things . I beg to differ.

Ukaribu wa baba na mtoto ni mzuri sana hasa kwa mtoto wa kike ila kila umri ina aina yake ya ukaribu. Kumbuka siku hizi mabinti wanabalehe kuanzia miaka 10 (naona hata huyu yupo above 10 kama sikosei) na umri huu unafaa baba akastep back kidogo. Kama ni suala la dharura sawa baba kimbilia bafuni msaidie , ila suala la nywele tu hapana sio dharura mpeke salon au muite mama yake amrekebishe vizuri.

Chriss ametumia nguvu nyingi kujitetea ila anadhani tunapokosoa tuna mawazo mgando , hapana akumbuke bado tupo kwenye mihimili ya vitabu vya dini , hasa Biblia anayoiamini yeye, mwanamke au binti anahitaji kusitiriwa na inawaamuru kina mama kuwalea na kuwaongoza mabinti katika staha na sala.
Pengine tunadhani ni uzungu sana , la hasha tumeishi nao na tunaona wazungu wenye staha nyingi tu wana njia tele za kubond na watoto wao kwa kuwasikiliza, kwa kuwa nao kwenye sports , kwenye sala, matembezi nk ila narudia kuna mipaka.

Alichokifanya Dr Mauki ni sahihi kabisa kwanza mimi pia nina mtoto wa kike, mtoto wa kike mapenzi ya mwanaume wa kwanza anapaswa kuyapata kwa baba yake, ila tatizo la Dr Mauki ni swala la personal kuliweka Public kwenye mitandao ya kijamii.

Watanzania wengi tunakabiliwa na tatizo kubwa la kutokujuwa do n donts kwenye hii mitandao ya kijamii.

Kwa mfano mimi app ya Instagram nilidownload ili nipate fursa ya kuangalia drama za Wabongo mimi binafsi sipost chochote na wala sicomment chochote huko.

Facebook ndio naitumia zaidi lakini unaweza kuhisi mimi huwa sipigi picha maana huwa napost picha kwa nadra sana tena kwa matukio maalum lakini device yangu imejaa mapicha kibao. Mimi siwezi kupost mtandaoni picha zangu tukiwa club au kwenye vikao vya kushangweka kwenye bia na nyama choma maana nawajuwa vizuri Wabongo wenzangu watatokea Mafarisayo na wengine kujifunzia uhubiri kwangu kwamba nimepotea, namchukiza Mungu wakati yeye ni mchafu kuliko wewe

Watanzania wakijifunza do n donts kwenye mitandao basi watajiepusha na mafarisayo.
P

Nilichogundua kwenye mjadala huu wachangiaji wengi wanaokosoa ni wale wenye uchu na papuchi kupita kiasi, either kwa kutokua na mademu wa kutosha au madomo zege. huyo binti ni bado mdogo sana. huo mwili ni sababu ya maisha mazuri tu, kingine haina shida kwa sababu ameanza kumlea hivyo tangu amezaliwa, ni mwanae yuko nae muda mwingi. Mimi mwenyewe nina binti yangu yupo kidato cha tatu, tuko nae karibu sana kwa jinsi ninavyomlea kiasi kwamba anajisikia huru kaniambia chochote kinachomkwaza au mawazo yake katika maisha. ukaribu kwa binti humjengea kujiamini sana. Kumbukeni jinsia ya kike hujiamini sana kuwa karibu na jinsia ya kiume. kwa hiyo kuwa karibu sana na mtoto wako wa kike kuanzia anapozaliwa, na kadri anavyokua asili ile ya kua mwanaume ndio kichwa cha nyumba anaendelea kukua nayo. huyo binti kuja kudanganywa na wanaume mapema inakua ngumu sana. kwa sababu kila analomwelekeza baba ndilo linakua sahihi kichwani mwake. Binti tangu amezaliwa unambeba unamsaidia mkeo kumuogesha unambadili nepi akijisaidia mpaka anafikisha umri wa kuhudumiwa na mama yake utaanzaje kumtamani kwa mfano ? sibishi wako watu wa kuwatamani binti zao ila ni wenye matatizo ya kiakili na ambao nimewaelezea hapo juu. na mwisho wachangiaji wengi Wamesema hapo ni chooni, wana hakika gani na hilo ? hawajui siku hizi hata sehemu ya kulia chakula chakula Kuna sinki la kunawia mikono na kioo ? Je hawajui siku hizi watu wanajenga mpaka kaunta za vinywaji kwenye sebule za nyumba ?
NB: tuepuke kurusha picha hovyo mitandaoni.
 
Back
Top Bottom