[PICHA + VIDEO] CHADEMA ndani ya Butiama

[PICHA + VIDEO] CHADEMA ndani ya Butiama

kitungi

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
239
Reaction score
597
Mbowe-kuzungumza-butiama.jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akitoa salamu za chama hicho kwa Familia ya Mwalimu Nyerere, wakati vongozi mbali mbali na wabunge wa chama hicho, walipomtembela Mama Maria Nyerere (katikati) nyumbani kwake Butiama jana. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilibrod Slaa

Mbowe-shada-butiama.jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, wakati viongozi mbalimbali wa chama hicho walipomtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Butiama hii leo.

Halimashadalamaua.jpg

Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), akiweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, wakati viongozi na baadhi ya wabunge wa chama hicho, walipomtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Butiama leo. (Picha na Joseph Senga)

SlaakusalimiananaMama.jpg

Slaa-Mbowe-Maria.jpg


Slaa-nyerere.jpg

Mama Maria Nyerere akiteta jambo na katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, wakati viongozi wa Chama hicho na baadhi ya wabunge, walipomtembelea nyumbani kwake Butiama hii leo.

 
Last edited by a moderator:
Tumeona mkuu.

Shukrani na kila la heri Chadema katika shughuli zao za kusaka uongozi wa nchi ila sioni wala sijasikia taarifa zao za kuongeza idadi ya wanachama wapya. Mikutano bila kupata wanachama wapya na kufungua matawi ngazi za vijiji kutakuwa na tija kubwa?

Nimeona na kusifu juhudi za kamanda Mbowe kufungua matawi Arusha lakini sijaona juhudi zaidi za kuyaendeleza huko wanakofanya mikutano ingawa inaweza kuwa inafanyika bila kupewa nafasi katika vyombo vya habari. Nashauri nalo liwe linasemwa ili tuone ongezeko na ukuaji wa CDM.
 
Wakuu naomba kujua, nini "maana" ya kuweka maua kaburini?
 
Thanks Chadema na Viongozi wetu kwa kuendeleza "Heshima" pale inapohitajika. Hii ni fundisho kwa ccm na wachanganyikiwaji kuona kwamba Chadema kama chama tunapokea hata wanachama wa ccm wakitaka kuvuka mto na kuja kwetu.

Sasa swali ni hili, kama Taifa lilimjengea Mwalimu Nyerere mahali pa kuishi baada ya kustaafu, Je Mwinyi, Mkapa, Kikwete wamejifisadi kiasi gani? Tutawakumbuka kwa kitu gani?
 
mbowe kasika nini hapo? au kifimbo cha mwalimu kakipaka rangi?
 
:usa2:

Katika siku mlizofanya jambo la maana ni leo kutuletea hizo picha. Jana tulikosa maandamano ya Musoma ambayo ilikuwa bomba sana kama mngetuwekea picha lakini leo mmejirekebisha CDM.

Hapo ndo tunapowapenda maana mnawasikiliza watu wanahitaji nini, Bravoooooo! Hebu tuwekeeni na Ratiba basi ya siku hizi kumi za kanda ya ziwa ili sie tulio mbali na huko tufuatilie kwa ukaribu leo mko wapi na kesho mko wapi. Hongera makamanda wetu ALUTA CONTINUA

:rain::rain:
 
Naomba Mungu kwa kweli huku aliko baba wa Taifa aliombee taifa lake liondokane na RUSHWA ILIYOKITHIRI....
 
vizuri sana kaka, kwel upo makin nimeamin sasa, kazi njema, kesho wap? Tupen root!
 
Ndugu yangu wewe unabahati ujawahi kufiwa,
nadahani utajajua tu,xxxxxxxxxxxxxxxxx i reserve my coment.xxxxxxxxxxxxxx
 
Safi sana Mkuu Nguvu ya Uma inazidi kusambaa na Marehemu mwl. Nyerere kaisikia.

tusubiri kishindo cha 2015
 
:mullet::mullet::mullet:BRAVOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO WANA CDM WOTE! TUJIANDAE KUELEKEA IKULU MWAKA 2015!!!!!!!!!!!!!:mullet::mullet::mullet:
 
Time table, ratiba ratiba! Jamen wakuu mlioko huko nyanda za ziwa tupen ratiba il tuijue route kamil ya Makamanda kama vp tujpange fresh na kuwahamasisha raia. Big up kwa pics ulzopost!
 
Back
Top Bottom