Picha: treni za Dar - Mwanza/Kigoma

Inavutia,waitunze tu sasa na marekebisho muhimu vitu vikianza kukongoroka!!!
 
Watanzania hawana Ustaarabu kabisa, watachubua kuta, watachafua rangi....
Hatuna ustaarabu kabisa, sie ni wachafu na waharibifu.
 
Hii ndiyo inanunaka Uchakachuaji sana wa zabuni yake.
 
Miaka ya nyuma mabehewa yaliyokuwa safi ni ya moshi na arusha
haya ya kigoma mwanza....duuuuh

Arusha-Moshi masaa, Kigoma Mwanza siku tatu,

mabehewa hayana maji,

abiria wengi mno kwa kukosa alternative transport means

Halafu unategemea usafi.
 
Watanzania hawana Ustaarabu kabisa, watachubua kuta, watachafua rangi....
Hatuna ustaarabu kabisa, sie ni wachafu na waharibifu.

Hivi wewe ni mkenya ?
 
Arusha-Moshi masaa, Kigoma Mwanza siku tatu,

mabehewa hayana maji,

abiria wengi mno kwa kukosa alternative transport means

Halafu unategemea usafi.
Nina maanisha yaliyokuwa yakitoka Dar kwenda miji ya Arusha na Moshi.
Mabehewa yote yalikuwa yanajazwa maji katika vituo fulani fulani.
ZAMANI.70's and Early 80's
 
Nina maanisha yaliyokuwa yakitoka Dar kwenda miji ya Arusha na Moshi.
Mabehewa yote yalikuwa yanajazwa maji katika vituo fulani fulani.
ZAMANI.70's and Early 80's

Nakubaliana na wewe, lakini kwa kuzingatia kwamba treni za Mwanza na Kigoma zilikuwa na abiria wengi mno, mpaka mtu unasimamia mguu mmoja kama jogoo kwa kukosa pa kuuweka wa pili, na ni safari ya siku tatu, usitegemee kuona usafi
 
Umenikumbusha safari yangu ya kutoka Dar kwenda Kigoma sekondari,safari ambayo sitoisahau katika maisha yangu.Chini hakuna pa kukanyaga,nyuma kuna abiria amekalia sit yangu ile sehemu ya kuegemea magoti amekita mgongoni kwangu,kushoto kuna mama ana watoto kama wanne hivi kwenye siti moja ,kulia kuna mama mwingine ana watoto wawili. Safari ya siku tatu,yaani ni nusu kaburi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…