Dr Matola PhD
Platinum Member
- Oct 18, 2010
- 62,610
- 112,369
Nchi imeshakuwa ya Kiswahili wala usishangae lolote. Bloger Michuzi anakuwa ndio mpiga picha wa Rais na yule Maro ana kazi gani? haya Mambo ya kupeana mapande hata kwenye taasisi nyeti ndio yametufikisha hapa.Asante kwa kunielewesha
Je itifaki inasemaje kuhusu hii bendera maana sijawai kuiona labda sign kwenye magari ya IKULU
mbandika picha ni vizuri ungeelezea na hali halisi ya alichozungumza rais wetu na jinsi ya huo umati ulivyofika hapo na ni % ngapi ya watu wa mjini igunga wamehudhuria
1. Mapokezi yake yalikuwa jana na alipokelewa na wananchi wachache na vijana wa bodaboda na bajaji walichukuliwa kwa ahadi ya kupewa tsh.5,000/= jambo ambalo ni aibu na pia hata hiyo fedha yenyewe hawakupewa.
2. Juhudi za kusomba watu zimeanza tangu jana na watu walifikishwa ma maloli kama 5 hivi na wote walilazwa chini katika ofisi za ccm chakula cjui kama walipata. Aibu ya pili hiyo.
3. Leo siku ya mkutano watu wamesombwa na malori yasiyopungua 20 kutoka maeneo yote ya vijijini.
Aliyoongea mengi yalikuwa yamejaa ushabiki wa kisiasa na sio ya kujenga umoja na mshikamano kwa watanzania.
Kuna kauli ambayo niliona haikufaa kwa kiongozi wa nchi kuizungumza.
** alisema ujenzi wa daraja ni ahadi ya serikali ya chama cha ccm na ipo katika ilani ya ccm sasa anashangaa imekuwa ni kigezo cha kuvuliwa ubunge kwa kafumu, itabidi sasa tuwe tunafanya kampeni za kibubu kwani ukiongea tu inakuwa kosa na hapo mbeleni itabidi tutafute namna ya kuepukana na hili(namna gani anajua yeye) kwa kauli hii naona anapingana moja kwa moja na sheria za nchi hii. Pia alisema dr. Kafumu amekata rufaa wanachosubiri ni uamuzi wa mahakama kama watashinda au la lakini wakishindwa wataingia kwenye uchaguzi na watashinda kwa kishindo kuliko uchaguzi uliopita. Hapa watu wengi waliguna. Hapa inaonyesha ccm kazi wanayo.
Labda kitu kinachonishangaza kwa nchi yetu inatakiwa tutenganishe ziara za serikali na chama rais anapofanya ziara za serikali na kuingiza mambo ya chama yanaleta sintofahamu kwa watu wengine. Wenzetu usa rais akishachaguliwa iwe ndani au nje ya nchi anapeperusha bendela ya taifa huku kwetu nimeshangaa kuona mitaa yote ikiwa imetapakaa bendera za kijani (ccm) nimeshindwa kuelewa hii ni ziara ya serikali au chama.
Rais Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utakaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga leo.
Rais Kikwete akisalimiana na mamia ya wananchi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo leo.
Mamia ya wakazi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo leo.
naona roho imekuuma kuona huo umati hahahaaaaaaaaKwanini Mheshimiwa Rais alibadili shati jamani? Au picha ni za siku tofauti?
kaka Michuzi unafanya vibaya kuchakachua picha za Rais
Kwanini usilete hali halisi ya mkutano? kwanini unachakachua picha
Huu mtindo utaauacha lini maana unadhalilisha chama chetu wewe huoni hizi picha kuwa ni tofauti?
Source:MICHUZI: JK AITEKA IGUNGA LEO
Nakala kwa Nape Nnauye, @Nnauye Jr, Mwigulu LM Nchemba W. J. Malecela, chama, Ritz
Huyu michuzi anaitaji kushughulikiwa la sivyo anaangamiza chama
picha ya kwanza kizungumkuti usingeiweka maana imepigwa gizani
kwanini inavivuli vya giza?
Huyu aliyeleta alishindwa kufanya photoshop vizuri?
Haya mambo ndio yanazalilisha chama chetu
Ikiwa Michuzi kakachua picha tuletee hizo zako ulizonazo; kumbuka kitu kimoja mh. Kikwete sio katibu wa chama ni Raisi wa JMT wananchi wa Igunga wamekwenda kushuhudia ni jinsi gani serikali iliyo chini ya chama makini CCM inavyoendelea na kazi yake ya kuwaondolea wananchi wa Igunga kero zinazowakabili.
Chama
Gongo la mboto DSM
Lohhh,
Wee ni jamaa wa home kama sikosei ila hizi propaganda zako zimenishinda kuvumilia. Ngoja nikuweke kwenye listi yangu ili nisivunje Computer. Samahani lakini na usichukulie PERSONAL.
Unamfahamu huyo unaebishana naye au ni speed za bangi ndio zinakupelekesha? huyo ni CCM kindakindaki na yupo front na siyo wewe Mkimbizi wa kiuchumi unayepractice siasa kwenye keyboard.Ikiwa Michuzi kakachua picha tuletee hizo zako ulizonazo; kumbuka kitu kimoja mh. Kikwete sio katibu wa chama ni Raisi wa JMT wananchi wa Igunga wamekwenda kushuhudia ni jinsi gani serikali iliyo chini ya chama makini CCM inavyoendelea na kazi yake ya kuwaondolea wananchi wa Igunga kero zinazowakabili.
Chama
Gongo la mboto DSM
kaka ni kwa sababu raisi mwenyewe hana hadhi tena hivyo anajiegemeza kwenye kitambaa kiitwacho bendera ndio tatizo la kandambili kukaa inapotakiwa kukaa kofia.tumekwisha sie nami nimoAsante kwa kunielewesha
Je itifaki inasemaje kuhusu hii bendera maana sijawai kuiona labda sign kwenye magari ya IKULU
Hivi hii bendera ya pili ni ya CCM au muungano?
Naomba mwenye kujua hii bendera aniambie
Kama sikosei itakuwa ni bendera ya Ikulu ile ambayo inakuwaga kwenye gari la rais, lakini sidhani kama kulikuwa na haja hiyo. Nchi inapelekwa kimagumashi tu.
Rais Kikwete akiwapungia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa Igunga katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utakaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga leo.
Rais Kikwete akisalimiana na mamia ya wananchi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo leo.
Mamia ya wakazi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo leo.